Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Bw. Akashambatwa
Mbikusita-Lewanika,(Pichani) hatimaye ameachia ngazi baada ya kuendesha
kampeni kali ya miezi kadhaa kutaka aendelee kuongoza Mamlaka hiyo kwa
miaka mingine mitatu.
Hatua
hiyo ya kuachia ngazi imekuja baada ya Bodi ya Wakurugenzi na Baraza la
Mawaziri la Mamlaka hiyo kuonyesha dhahiri kutotaka Mzambia huyo
aendelee na uongozi wa TAZARA kutokana na utendaji wake mbovu na uongozi
mbaya uliowabagua wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kwa misingi ya utaifa
wao.
Habari
za ndani za Mamlaka hiyo zimesema Bw. Akashambatwa ambaye kipindi chake
cha uongozi kiliisha tarehe 22 Januari, 2013 kiliongezwa kwa maombi
maalum ya Serikali ya Zambia kwamba Serikali hiyo ilihitaji muda mrefu
kidogo kumpata mbadala wake, licha ya Serikali ya Tanzania
kutoridhishwa na utendaji wake.
Katika
kikao chake cha tarehe 20 Februari, 2013 jijini Lusaka, Zambia, Baraza
la Mawaziri lilijadili kwa siri na kwa kirefu suala la mtendaji Mkuu
huyo ambaye inasemekana aliombewa tena na Serikali ya Zambia kipindi cha
nyongeza, ombi ambalo inadaiwa lilipingwa vikali na ujumbe wa Serikali
ya Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
Taarifa
za uhakika ndani ya Wizara ya Uchukuzi zinasema Serikali ya Tanzania
haikumtaka Mtendaji Mkuu huyo kwa sababu kadhaa zikiwemo :uwezo mdogo,
ubadhirifu, kuchochea ubaguzi kati ya Watanzania na Wazambia, ukaidi na
uchochezi. Inadaiwa kuwa Mtendaji Mkuu huyo alizuia kuanzishwa kwa mradi
wa usafiri jijini Dar es Salaam bila sababu yoyote ya msngi na kuishia
kusambaza taarifa za uongo na uchochezi Zambia na magazeti mbalimbali
nchini.
Tarehe
25 Februari, 2013 Gazeti la kila siku la Zambia, Zambia Daily Mail,
liliripoti tukio hilo la kuachia ngazi kwa kiongozi huyo ambaye
anajulikana sana nchini Zambia kama mfanyabiashara na kiongozi wa kimila
(chief),
Gazeti
hilo lilinukuu barua ya Bw. Akashambatwa ya tarehe 22 Februari, 2013
kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Ujenzi, Ugavi na
Mawasiliano ya Zambia, akielezea kuwa hakuna faida ya kuomba kurefushwa
kwa mkataba wake wakati vyombo vikuu vya uongozi vya TAZARA, Bodi ya
Wakurugenzi na Baraza la Mawaziri, havionyeshi kumkubali.
Kuondoka kwa Bw. Akashambatwa kwenye uongozi wa TAZARA kunatarajiwa kupokewa na wafanyakazi wa TAZARA kwa nderemo na vifijo.