Wednesday, February 27, 2013
Rais Kikwete akagua Ukumbi Wa Mikutano wa Kimataifa jijini Dar es Salaam
MSANII AMTELEKEZA MTOTO STENDI YA UBUNGO
MREMBO aliyewahi kupamba video kadhaa za wasanii wa Bongo Fleva ukiwemo wimbo wa Kidato Kimoja ulioimbwa na J.I, anayekwenda kwa jina la Maya Silemwe, amedaiwa kumtelekeza mwanaye wa kumzaa aitwaye Junior Justine (3).
Akisimulia mkasa mzima ulivyokuwa, shangazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Monalisa, alisema wao kama familia wameumizwa sana na kitendo kilichofanywa na Maya.
KUTOKA IKULU,TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jaji na Balozi Mstaafu
Mheshimiwa Hamis Amiri Msumi kuwa Mwenyekiti wa BARAZA LA MAADILI.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, 26
Februari, 2013 jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi
Ombeni Y. Sefue, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Februari 18, mwaka
huu, 2013.
“Mwisho”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.
26 Februari, 2013
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.
26 Februari, 2013
Leo ni kilele cha maadhimisho ya kumbukumbu ya mashujaa wa vita vya majimaji nchini Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu.
Maadhimisho
ya vita vya Majimaji yenye lengo la kuwakumbuka mashujaa zaidi ya 67
walionyongwa Februari 27 mwaka 1906 na kuzikwa katika kaburi moja wakiwa
katika harakati za kuung’oa ukoloni wa Wajerumani yamafikia kilele leo
mkoani Ruvuma.
Maadhimisho
hayo yameandaliwa kitaifa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa
kushirikiana na mkoa wa Ruvuma yanafikia kilele leo katika makumbusho ya
Vita vya Majimaji mjini Songea.
Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu amesema wakazi wa mji wa
Songea na viunga vyake pamoja na wananchi kutoka mikoa ya jirani
wamejitokeza katika maadhimisho hayo.
Serikali ya Uganda yakusudia kuwanunulia wabunge wote toleo jipya la iPads kupunguza gharama za steshenari.
Chama
cha Forum for Democratic Change (FDC) kimepokea na kukubali mpango wa
serikali ya Uganda wa kununua toleo jipya kabisa la iPads kwa ajili ya
wabunge, lakini kimesema wabunge hao wakopeshwe na sio wapewe bure.
Msemaji
wa Chama hicho Wafula Oguttu ambae pia ni mbunge, amesema pendekezo la
kununua iPads halikataliwi lakini hakuna sababu ya kuwapa bure na badala
yake wapewe kwa mkopo.
Serikali ya Uganda imepanga kununua iPads za kisasa na kuwapatia wabunge kwa lengo la kupunguza gharama ya steshenari.
Uamuzi huo ulichukuliwa hivi karibuni na Kamati ya Bunge na unasubiri utekelezaji kwa Kamati ya Mikataba.
Benedict XVI to hold final papal audience in Vatican.
Crowds
have begun gathering in St Peter’s Square in the Vatican for the Pope’s
final general audience before his resignation on Thursday.
Papal audiences are normally held inside a Vatican hall in the winter.
But such is the level of interest that the event is being held outdoors and 50,000 tickets have been requested.
As many as 200,000 people may attend.
After Benedict XVI steps down on Thursday, he will become known as “pope emeritus”.
There has been no papal resignation since Pope Gregory XII abdicated in 1415.
The
surprise announcement of Benedict’s abdication has required the rules
of electing a successor to be changed to allow the next pope to be
chosen before Holy Week, which leads up to Easter.
On
Wednesday, the Pope, 85, will be making one of his last public
appearances – using his trademark white “popemobile” to greet pilgrims
in St Peter’s Square.
Waziri Mkuu afanya mazungumzo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kutoka Sweden.
Waziri
Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akifurahia jambo wakati wa
mazungumzo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw.
Ludovick Utouh (kushoto) na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali wa
Sweden Jan Lindahr Hjelmaker. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Tuesday, February 26, 2013
CRDB yawa benki pekee Tanzania kupata cheti cha Superbrands kwa miaka miwili mfululizo.
Mkurugenzi
kutoka taasisi ya Superbrand, Jawad Jaffer akitoa maelezo kwa wageni
waalikwa juu ya kitabu cha orodha ya kampuni zilizotunukiwa hadhi ya
Superbrand.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB-Uendeshaji na huduma kwa wateja
Saugata Bandyopadhyay(kulia) akipokea cheti cha Superbrand kutoka kwa
mkurugenzi wa Superbrands ukanda wa Afrika Mashariki, Jawad Jaffer.
Baadhi ya wageni walio hudhuria tafrija hiyo.
Mkurugenzi
wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther
Mwambapa akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
CRDB-Uendeshaji na huduma kwa wateja Saugata Bandyopadhyay wakati wa
tafrija ya kupokea cheti cha Superbrand
Mkurugenzi
wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther
Mwambapa akizungumza na waandishi wahabari juu ya sababu zilizoipaisha
Benki ya CRDB hadi kutunikiwa cheti cha Superbrand kwa mara ya tatu
mfululizo pia mikakati ya benki hiyo katika kuboresha huduma zake ili
kuendeleza rekodi yake ya kupata cheti hicho kila mwaka.
WAZIRI WA MAMBO YA NJE YA NCHI WA OMAN AKUTANA NA RAIS WA ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimkabidhi zawadi ya Mlango wa Zanzibar, Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman,Yussuf bin Alawi Bin Abdullah,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe wake leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Ujumbe wa Serikali ya Watu wa Oman,ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman,Yussuf bin Alawi Bin Abdullah,(wa pili kulia) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe wake leo,kwa ajili ya Mazungumzo na Rais. Picha na Ramadhan Othman,IKulu.
Kocha wa Azam afungiwa na kupigwa faini kwa kuchojoa bukta.
Kocha
Mkuu wa Azam, Stewart John Hall (pichani) amefungiwa mechi tatu na
kupigwa faini ya sh. 500,000 kwa kushusha bukta yake na kumlalamikia
mwamuzi msaidizi wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya
timu yake na Kagera Sugar iliyochezwa Januari 26 mwaka huu Uwanja wa
Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Adhabu
hiyo imetolewa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) iliyokutana mwishoni mwa wiki kupitia ripoti za michuano
ya VPL na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2012/2013 inayoendelea
hivi sasa na kufanya uamuzi mbalimbali.
Naye
Kocha Msaidizi wa timu ya Mgambo Shooting, Denis Mwingira ametozwa
faini ya sh. 500,000 kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi kwenye mechi dhidi
ya Mtibwa Sugar iliyochezwa Oktoba mwaka jana katika Uwanja wa Manungu.
Ally
Jangalu ambaye ni Kocha Msaidizi wa Polisi Morogoro naye ameangukiwa na
rungu la Kamati ya Ligi kwa kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya
kutolewa kwenye benchi kwa kupinga uamuzi wa refa kwa sauti ya juu.
Alitenda kosa hilo kwenye mechi kati yao na Kagera Sugar iliyochezwa
Novemba 10 mwaka jana Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Matukio
ya aina hiyo kwa kocha Jangalu yamekuwa ya kujirudiarudia ambapo Oktoba
13 mwaka jana katika mechi dhidi ya Azam iliyochezwa mjini Morogoro
aliondolewa na mwamuzi kwenye benchi kwa kuchochea wachezaji wa timu
yake wacheze rafu.
Naye
Kocha wa timu ya Moro United inayoshiriki FDL, Yusuf Macho amepigwa
faini ya sh. 200,000 kwa kumtolea lugha chafu refa baada ya mechi dhidi
ya Transit Camp iliyofanyika Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Mabatini
mjini Mlandizi.
Pia
Kocha wa Burkina Faso, Hasheem Mkingie amepigwa faini ya sh. 200,000
baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kutoa lugha chafu katika mechi ya
FDL dhidi ya Mkamba Rangers.
Kiongozi
wa Majimaji, Joseph Nswila ambaye aliingia uwanjani baada ya mechi
dhidi ya Mlale JKT kumalizika na kuvamia waamuzi amefungiwa miezi sita.
Vilevile
timu ya Azam imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika
uwanjani kwenye mechi kati yao na JKT Oljoro iliyochezwa Novemba 7 mwaka
jana katika Uwanja wao wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Pia
Coastal Union imetozwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake
kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi namba mbili wakati wa mechi yao
dhidi ya Simba iliyochezwa Oktoba mwaka jana Uwanja wa Mkwakwani jijini
Tanga.
Nayo
klabu ya African Lyon imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa timu yake
kugoma kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo wakati wa mapumziko
katika mechi dhidi ya Coastal Union iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga, Oktoba 24 mwaka jana.
Timu
ya Burkina Faso ya Morogoro imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na
kuonesha vitendo vya ushirikina kabla ya mechi yao dhidi ya Mbeya City
iliyochezwa Oktoba 24 mwaka jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Faini
ya ushirikina ya sh. 200,000 pia imepigwa timu ya Pamba baada ya
kuonesha vitendo hivyo kwenye mechi yao dhidi ya Mwadui iliyochezwa
Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Nayo
Mkamba Rangers imepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya washabiki wake
kumtolea lugha chafu Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro
(MRFA), Hamis Semka na kumrushia chupa za maji mwamuzi wa mezani katika
mechi dhidi ya Mbeya City iliyochezwa mjini Morogoro.
Polisi
Dodoma imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na washabiki wake kuvamia
uwanjani na kutaka kuwapiga waamuzi katika mechi yao dhidi ya JKT
Kanembwa na kusababisha mipira miwili ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa
wa Dodoma (DOREFA) kupotea.
Pia
klabu kadhaa zimeandikiwa barua za onyo kwa timu zao kuchelewa kufika
uwanjani au kutofika kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match
meeting). Klabu hizo ni Coastal Union, JKT Ruvu, Toto Africans, Simba,
Green Warriors, Majimaji, Mkamba Rangers, Polisi Dodoma, JKT Kanembwa,
Moro United.
Mchezaji
Stanley Nkomola wa JKT Ruvu baada ya mechi dhidi ya Coastal Union
alikwenda jukwaani na kuanza kupigana na washabiki. Pia kipa wa timu ya
Transit Camp, Baltazar Makene baada ya mechi dhidi ya Tessema aliruka
uzio na kwenda kupigana na washabiki.
Kwa
vile masuala ya wachezaji hao ni ya kinidhamu yamepelekwa kwenye Kamati
ya Nidhamu inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu Alfred
Tibaigana kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.
MeTL GROUP yapokea tuzo ya ubora na thamani ya nembo ikiwa ni ishara ya kukubalika na walaji.
Mkurugenzi
kutoka taasisi ya Superbrands ukanda wa Afrika Mashariki, Jawad Jaffer
akitoa maelezo kwa wageni waalikwa juu ya kitabu cha orodha ya kampuni
zilizotunukiwa hadhi ya Superbrands wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti
vya tuzo za ubora na thamani ya nembo kwa makampuni bora 2013/14
iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa taasisi huru ya Superbrands Ukanda wa Afrika Mashariki Jawad Jaffer
akimkabidhi Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group
Hussein Dewji cheti cha tuzo ya ubora na thamani ya nembo kwa kampuni
zinazotoa huduma bora kwa walaji katika hafla fupi iliyofanyika leo
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Raha Aashiq Sharrif (Kulia) akiwa Mwakilishi wa
Masoko na Mauzo wa kampuni ya Raha Preetkamal Bansal ( wa pili kulia)
wakati wa hafla fupi ya Superbrands kukabidhi vyeti kwa makampuni bora
kwa mwaka 2013/14 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa ITV na Radio One Bi. Joyce Mhaville ( wa pili kulia)
aliyembatana na Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha IPP Bi. Joyce Luhanga (
wa tatu kulia) wakati wa hafla ya utoaji wa cheti cha tuzo ya ubora na
thamani ya nembo iliyoendeshwa na Taasisi ya Superbrands.
Mkurugenzi
wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji
akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Na.Mo Blog Team
Taasisi
huru ya Superbrands ambayo ni kubwa kuliko zote duniani, inayoratibu
ubora na thamani ya nembo kwa kampuni zinazotoa huduma bora kwa walaji,
leo imekabidhi vyeti vinavyotambuliwa kimataifa vya utambuzi wa ubora wa
bidhaa kwa kampuni zilizofanya vizuri nchini Tanzania kwa mwaka
2013/2014.
Tuzo za Superbrands ni miongoni mwa tuzo zenye thamani kubwa na zinazoleta heshima ya pekee ndani ya kampuni.
Hii
ni mara ya tatu kwa tuzo hizo kutolewa ndani ya Ukanda wa Afrika
Mashariki tangu kuanzishwa kwake yapata miaka mine iliyopita.
Uamuzi
na hatimaye utoaji wa tuzo husika unatoka baraza huru la wataalamu
waliobobea katika masuala ya biashara, lakini lengo hasa likiwa ni ni
kustawisha na kuhamasisha ari katika utoaji huduma zinazo zingatia
ubora.
MeTL imekuwa moja wapo kati ya Makampuni yaliyopokea vyeti vya tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya tatu hapa nchini.
Tigo yaongeza kifurushi cha ziada kwenye huduma za Blackberry!
Tigo
Tanzania imezindua kifurushi kipya cha Blackberry ambacho kitawapa
wateja fursa ya kutumia mitandao ya kijamii kwa bei nafuu zaidi
kijulikanacho kama Blackberry Social Plan.
Kifurushi
hiki kitawawezesha wateja wa Tigo kutumia mitandao ya kijamii kama
Twitter, Facebook, Whatsaap na mingineyo ipasavyo kwa gharama nafuu
zaidi. Watumiaji wanaweza kujiunga na kifurushi cha siku, wiki au mwezi
kutokana na matumizi yao.
Ndg.
William Mpinga, meneja wa chapa ya Tigo alisema kuwa “Mitandao ya
kijamii imezidi kuja juu baada ya watumiaji kuongezeka maradufu na
kuitumia kwa matumizi mbalimbali kama kutafuta habari, kutumiana ujumbe
n.k. Mitandao hii hupatikana kiurahisi sana bila gharama yeyote hivyo
kuifanya idadi ya watumiaji kukua kwa kasi kubwa sana. Watumiaji wa
kifurushi cha blackberry watanufaika na huduma mbalimbali muhimu ambazo
zitawasaidia kujiendeleza kibiashara na kikazi kwa kuwaweka karibu na
wafanyabiashara au wafanyakazi wenzao pamoja na wateja wao. Huduma kama
BBm na Whatsapp zitawawezesha kujadili mambo mbalimbali kama vile wako
mahali pamoja hivyo kupunguza haja ya mikutano ya kila mara. Watumiaji
wataweza kufanya haya yote wakiwa majumbani kwao, au kwenye mizunguko
yao mbalimbali.”
Mr.
Mpinga aliendelea kwa kusema kuwa “tuliamua kuzindua kifurushi hiki
ili kuwapatia wateja wetu huduma mbadala juu ya kifurushi cha Blackberry
na hivyo kuongeza thamani ya huduma zetu.”
Kutumia
huduma hii mteja inabidi ajiunge kwa kutuma ujumbe kwenda 15518 wenye
neno BBS1 kutumia kifurushi cha siku, BBS7 kutumia kifurushi cha wiki,
na BBS30 kutumia kifurushi cha mwezi. Gharama za siku ni shilingi 499,
za wiki shilingi 2,999 na za mwezi shilingi 11,999. Kwa kutumia
kifurushi hiki wateja wataweza kutumia mitandao ya kijamii ipasavyo
kabisa.
Khadija Kopa, Isha Mashauzi Watoana Kijasho DAR LIVE.
Malkia wa mipasho, Khadija Kopa, akionesha umahiri wake wa kutikisa nyonga.
Mashabiki wanaomfagilia Isha Mashauzi wakiwa wamevamia steji baada ya kuwadatisha.
Aziza Abul ‘Bonge’ wa TOT Taarab akikamua.
Malkia wa mipasho akiserebuka na mmoja wa mashabiki wake aliyepanda jukwaani kumtunza.
Wakali Dancers wakiwajibika jukwaani.
Shabiki akimtunza Malkia wa mipasho baada ya kukunwa na mipasho.
Isha Mashauzi akikamua.
Mashabiki wakijimwaya kwa raha zao.
WAKALI
wa miondoko ya muziki wa mwambao nchini, Malkia wa miondoko hiyo,
Khadija Kopa akiwa na Kundi la TOT Taarab na Isha Ramadhani ‘Mashauzi’
jana waliugeuza Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live kuwa uwanja wa
mapambano baada ya kushindana kutoa burudani kwa kuonesha makali yao na
kuwafanya mashabiki kila mmoja kumtaja mshindi wake.
Kabla ya wakali hao
kuanza kuhenyeshana jukwaani burudani hizo zilianza kwa kunogeshwa na
shoo kali ya washiriki wa shindano la Mic King linaloendeshwa ukumbini
hapo kila Jumapili. Baada ya washiriki hao wanaowania gari, kundi la
Wakali Dancers lilivamia jukwaa na kufanya vitu vyake pia.(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL )
SIMBA SC WAITISHA MKUTANO MKUU WA DHARURA
Msemaji wa klabu ya simba Ezekiel Kamwaga akizungumza na Waandishi wa Habari leo mchana
KIKAO cha
Kamati ya Utendaji ya Simba SC jana, kimefikia uamuzi wa kuitisha
Mkutano Mkuu wa dharula wa klabu hiyo, ambao ajenda yake itakuwa moja
tu, kujadili mwenendo wa timu katika mashindano mbalimbali inayoshiriki.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari mchana wa leo, makao makuu ya klabu, Mtaa wa
Msimbazi, Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga
amesema kwamba siku na mahali ambako Mkutano huo utafanyika vitatajwa
wakati wowote kuanzia sasa.
Aidha,
Kamwaga alisema kwamba hadi sasa hakuna kiongozi yeyote wa Simba SC
aliyejiuzulu na kwamba uongozi upo pamoja. “Hadi sasa hakuna kiongozi
yeyote wa klabu ya Simba aliyejiuzulu. Uongozi upo pamoja na mambo yote
yatajadiliwa kwenye mkutano huo wa dharula,”alisema.
Akiuzungumzia
mchezo wa marudiano, Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika,
Kamwaga alisema kwamba timu itaondoka Alfajiri ya Ijumaa kwenda Angola
kuwavaa wenyeji wao, Recreativo de Libolo.
Alisema mechi hiyo itafanyika Jumapili mjini Calulo, umbali wa kilomita 200 kutoka mji mkuu wa Angola, Luanda.
“Kwa mujibu
wa kanuni za CAF (Shirikisho la Soka Afrika) kama umbali wa mji ambao
inachezwa mechi unakuwa ni zaidi ya kilomita 200, timu mwenyeji
inatakiwa kumsafirisha mgeni kwa ndege, kwa hivyo ni matumaini yetu,
wenyeji wetu watakuwa tayari wametutayarishia ndege, kwa kuwa hatuwezi
kusafiri kwa basi kwa zaidi ya saa nne,”alisema Kamwaga.
Kamwaga
alisema kwamba, Mkuu wa msafara wa timu atakuwa Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu, Zacharia Hans
Poppe, wakati upande wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utawakilishwa
na Mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji pia, Muhsin Balhabou.
Kamwaga
alisema kikosi kamili cha Simba kitakachokwenda Angola kitatajwa
Alhamisi kwa kuwa leo ni mapema sana, kwani wanahofia anaweza kuumia
mchezaji yeyote wakati amekwishatajwa kuwemo kwenye safari.
Simba SC
ilifungwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza na Libolo wiki iliyopita
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na ili isonge mbele, inatakiwa kushinda
2-0.
Mwaka 1978,
Simba iliwahi kufanya maajabu ikitoka kufungwa 4-0 na Mufulira
Wanderers ya Zambia mjini Dar es Salaam katika michuano hiyo hiyo na
kwenda kushinda 5-0 ugenini, hivyo kusonga mbele.
Subscribe to:
Comments (Atom)



