Tigo
Tanzania imezindua kifurushi kipya cha Blackberry ambacho kitawapa
wateja fursa ya kutumia mitandao ya kijamii kwa bei nafuu zaidi
kijulikanacho kama Blackberry Social Plan.
Kifurushi
hiki kitawawezesha wateja wa Tigo kutumia mitandao ya kijamii kama
Twitter, Facebook, Whatsaap na mingineyo ipasavyo kwa gharama nafuu
zaidi. Watumiaji wanaweza kujiunga na kifurushi cha siku, wiki au mwezi
kutokana na matumizi yao.
Ndg.
William Mpinga, meneja wa chapa ya Tigo alisema kuwa “Mitandao ya
kijamii imezidi kuja juu baada ya watumiaji kuongezeka maradufu na
kuitumia kwa matumizi mbalimbali kama kutafuta habari, kutumiana ujumbe
n.k. Mitandao hii hupatikana kiurahisi sana bila gharama yeyote hivyo
kuifanya idadi ya watumiaji kukua kwa kasi kubwa sana. Watumiaji wa
kifurushi cha blackberry watanufaika na huduma mbalimbali muhimu ambazo
zitawasaidia kujiendeleza kibiashara na kikazi kwa kuwaweka karibu na
wafanyabiashara au wafanyakazi wenzao pamoja na wateja wao. Huduma kama
BBm na Whatsapp zitawawezesha kujadili mambo mbalimbali kama vile wako
mahali pamoja hivyo kupunguza haja ya mikutano ya kila mara. Watumiaji
wataweza kufanya haya yote wakiwa majumbani kwao, au kwenye mizunguko
yao mbalimbali.”
Mr.
Mpinga aliendelea kwa kusema kuwa “tuliamua kuzindua kifurushi hiki
ili kuwapatia wateja wetu huduma mbadala juu ya kifurushi cha Blackberry
na hivyo kuongeza thamani ya huduma zetu.”
Kutumia
huduma hii mteja inabidi ajiunge kwa kutuma ujumbe kwenda 15518 wenye
neno BBS1 kutumia kifurushi cha siku, BBS7 kutumia kifurushi cha wiki,
na BBS30 kutumia kifurushi cha mwezi. Gharama za siku ni shilingi 499,
za wiki shilingi 2,999 na za mwezi shilingi 11,999. Kwa kutumia
kifurushi hiki wateja wataweza kutumia mitandao ya kijamii ipasavyo
kabisa.
No comments:
Post a Comment