Eneo la
tukio la ajali hiyo.
Mashuhuda
wakishuhudia ajali hiyo, gari likiwa mtaroni.
Kushoto ni
gari ya Stive yenye namba za usajiri T 779 BZL na (kulia) ni gari
lililohusika na ajali hiyo lenye namba za usajiri T 584 BQV.
Huu ndiyo
waya wa umeme uliosababisha ajali hiyo.
Askari wa
usalama barabarani, akipima ajali hiyo.
Askari
akimkunja Stive na kumpakia katika gari lao ili kuondoka naye kumpeleka
kituoni Mabatini.
Gari la
Stive likiwa limebondeka kwa mbele lilikogongana na gari jingine.
Gari
husika na ajali likiwa limetumbukia mtaroni.
Baadhi ya
warembo walikuwa na Stive katika gari lake ambao ni miongoni mwa
washiriki wa Movie hiyo, wakiwa eneo la tukio.
**********
Movie
mpya ya Msanii wa kuigiza sauti za Viongozi Stive Nyerere, iliyokuwa
ianze kurekodiwa leo imeingia dosari baada ya msanii huyo kupata ajali
na kuswekwa lupango katika kituo cha Polisi cha Mabatini, asubuhi hii.
Msanii huyo amepata ajali hiyo maeneo ya karibu kabisa na kituo
cha Mabatini, wakati akiwa na msafara wa wasanii wenzake wanaoshiriki
katika Movie hoyo, wakati wakielekea kuanza kurekodi.
Wasanii hao pamoja na Stive, walikuwa wakitokea katika Kambi yao
iliyokuwa maalum kwa maandalizi ya kuanza kurekodi ikiwa ni pamoja na
kufanyia mazoezi katika kambi hiyo iliyodumu kwa wiki kadhaa.
Ajali hiyo ilikuwa kama hivi:- Wakati Stive akiwa na baadhi ya
washiriki wa movie yake katika gari lake na wakiwa katika mwendo
kuelekea eneo la kushuti sini zao, ghafla aliona gari aina ya funcargo
ikiwa imesimama mbele yake huku katikati ya barabara akiwapo jamaa
aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo.
Baada ya kushindwa kusimama kwa ghafla ndipo alipoigonga gari hiyo
kwa nyuma na gari hiyo kutumbukia mtaroni.
Mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Fundi
umeme aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo ili kuweza kuondoa
waya wa Umeme uliokatika na kulala katikati ya barabara huku ukiwa na
moto, ili kuepusha madhara zaidi.
Baada ya ajali hiyo, walifika askari Polisi wakiambatana na askari wa
usalama barabarani, ambapo alianza kupima ajali hiyo huku madereva
wakijibizana na fundi aliyesimamisha magari, ambapo majibizano hayo
yaliingiliwa kati na mmoja kati ya askari waliofika eneo hilo.
Katika majibizano hayo baina ya fundi, Askari na madereva wote
wawili, ndipo kulitokea kupishana kauli baina ya Stive na Askari huyo,
aliyediriki kumuita Stive mjinga, ambapo Stive alishindwa kuvumilia na
kuamua kumjibu na ndipo alipokunjwa 'Tanganyika Jeki' na kukokotwa hadi
katika gari walilokuja nalo askari hao na kumpakia na kisha kuondoka
naye kuelekea katika Kituo cha Mabatini.
credits:
Sufiani Mafoto