Thursday, February 14, 2013

LIGI YA MABINGWA REAL YACHOMOA KWA MAN UTD

Real Madrid 1 Man United 1: 
Hang time: Cristiano Ronaldo scored against his former club with a 
well-executed header past David De Gea
Hang time: Cristiano Ronaldo scored against his former club with a well-executed header past David De Gea
Hang time: Cristiano Ronaldo scored against his former club with a 
well-executed header past David De Gea
Sir Alex Ferguson selected an attacking side, with Robin van Persie spearheading a front three of Rooney and Welbeck. 
But after an even first half, the away side found themselves on the back foot following the interval with United goalkeeper David de Gea making a number of strong saves to keep the tie level.
Hero: Manchester United stopper David de Gea turned in a fantastic 
display to keep the tie level
Hero: Manchester United stopper David de Gea turned in a fantastic display to keep the tie level
Head boy: Danny Welbeck scored the opening goal of the game from a 
Wayne Rooney corner
Head boy: Danny Welbeck scored the opening goal of the game from a Wayne Rooney corner
Danny Welbeck
.
Making his point: Sir Alex Ferguson selected an attacking line-up 
to face the Spanish giants
Making his point: Sir Alex Ferguson selected an attacking line-up to face the Spanish giants
Tough to watch: Jose Mourinho cut an animated figure on the 
touchline during the last-16 clash
Tough to watch: Jose Mourinho cut an animated figure on the touchline during the last-16 clash
Battle: Robin van Persie holds off the challenge from Alvaro 
Arbeloa as Fabio Coentrao slides in on Wayne Rooney (below)
Battle: Robin van Persie holds off the challenge from Alvaro Arbeloa as Fabio Coentrao slides in on Wayne Rooney (below)
Battle: Robin van Persie holds off the challenge from Alvaro 
Arbeloa as Fabio Coentrao slides in on Wayne Rooney (below)

It had 
to be him: Ronaldo is mobbed by his Real Madrid team-mates after scoring
 for the hosts
It had to be him: Ronaldo is mobbed by his Real Madrid team-mates after scoring for the hosts

Wednesday, February 13, 2013

Ligi ya mabingwa Ulaya leo balaa ni kati ya Real Madrid na Manchester United

Timu za Real Madrid ya Hispania na Manchester United ya Uingereza leo zitamenya vikali katika mechi ya Ligi ya mabingwa wa Ulaya.
Mechi hiyo itapigwa katika uwanja wa Santiago bernabeu nchini Hisppani ambapo mbali na kutafuta point tatu lakini zaidi kuweka heshima.

Zimbabwean Election Chief Mutambanengwe resigns


Zimbabwe’s election chief has resigned citing ill health.
Simpson Mutambanengwe resignation comes as Zimbabwe gears up for a crucial constitutional referendum and elections later this year.
Prime Minister Morgan Tsvangirai had been pushing for key reforms to guarantee free elections.
The poll will herald the end of the shaky coalition he formed with President Robert Mugabe after the 2008 election, which was marred by violence.
Justice Minister Chinamasa said that Mr Mugabe had accepted the resignation of Mr Mutambanengwe, a retired judge who took the post after the controversial 2008 poll, the state-owned Herald newspaper reports.

Serikali ya Tanzania yatoa ajira kwa waalimu wapya 26,537 kwa kipindi cha mwaka 2012/13


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa.(Picha na Maktaba).
Jumla ya waalimu 26,537 wameajiriwa na serikali kwa mwaka wa fedha 2012/13. Walimu wa ngazi ya cheti walioajiriwa ni 13,568. Kati yao walimu 13,527 wamepangiwa kufanya kazi katika shule za msingi zilizopo kwenye halmashauri na walimu 41 wamepangwa katika shule za msingi za mazoezi zilizopo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Jumla ya walimu wa sekondari na vyuo vyuo vya ualimu walioajiriwa ni 12,973 wakiwemo walimu walimu wa shahada 8,887 na wa stashahada ni 4,086.

BENKI YA NMB YATAHADHARISHA WATEJA WAKE

DAR ES SALAAM, Tanzania

MENEJIMENTI ya NMB imewaonya wateja wake na umma kwa ujumla kuwa imegundua kwamba kuna taasisi inayojitambulisha kama Tanzania Loans Society inadai kuwa mshirika wa benki hiyo katika kutoa huduma za kibenki.

Taasisi hiyo imedaiwa kuwa kwa kutumia mtandao wake wa intaneti imekuwa ikijinasibu kutoa mikopo ambayo fedha zake zimeidhinishwa na NMB kupitia kwa mameneja wa matawi.

Aidha, Tanzania Loan Society pia inadaiwa kueleza kwamba fomu za maombi ya mkopo na malipo ya usajili vinaweza kulipwa kwa  kutumia namba ya simu ya mkononi.

Menejimenti ya NMB imezidi kuwatahadharisha wateja wake na umma kwa ujumla kwamba haina ushirika au makubaliano yoyote na taasisi hiyo katika shughuli  zake.

Imeongeza kuwa, NMB hutoa mikopo yake kupitia matawi yake tu, na hakuna  namna yoyote ambayo inaweza kusababisha gharama za  maombi ya mikopo au mikopo kutolewa kupitia simu za mkononi.

Menejimenti hiyo imesisitiza  kuwataka  wateja na umma kwa ujumla kutojihusisha na taasisi  hiyo katika shughuli yoyote inayoihusu Benki ya NMB na kwamba haitahusika kwa namna yoyote  na matatizo yatakayojitokeza

ECOBANK YAKABIDHI ZAWADI KWA MSHINDI WA SHINDANO LA SHINDA NA BABKUBWA LEO


Zawadi iliyotolewa kwa mshindi
 Mkuu wa  Kitengo cha Sekta ya Umma wa Ecobank, Ndabu Swire akizungumza wakati wa hafala ya kutoa zawadi kwa mshindi wa Shindano la Babkubwa lililoendeshwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
 Waandishi wa habari wakiwa kazini.
 Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank, Enoch Osei-Safo akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa mshindi wa shindano la shinda na Babkubwa.
 Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, wafanyabiashara na wateja wakubwa wa Ecobank, Joyce Makui akizungumza wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa mshindi wa shindano la Shinda na Babkubwa
 Ipyana Mwakasaka akijaribu kifaa chake alichokabidhiwa mchana huu na Ecobank baada ya kuibuka mshindi katika shindano la Shinda na Babkubwa lililoendeshwa na benki hiyo.
 Ipyana Mwakasaka akijaribu kifaa chake alichokabidhiwa mchana huu na Ecobank baada ya kuibuka mshindi katika shindano la Shinda na Babkubwa lililoendeshwa na benki hiyo.
 Mkuu wa Ecobank, Enoch Osei-Safo (kushoto) akimkabidhi funguo ya gari aina Hyundai Tucson ix35 lenye thamani ya shilingi milioni 65 mshindi wa shindano la Shinda na Babkubwa, Ipyana Mwakasaka
 Ipyana Mwakasaka akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa zawadi yake.

HATIMAYE MAMA LULU NA MAMA KANUMBA WAPATANISHWA



Hatimaye mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba amepatanishwa na mama mzazi wa Lulu baada ya mlolongo mrefu na mgumu wa jitihada za kuwapatanisha kina mama hao wawili.

Chanzo chetu cha kuaminika  kimeripoti kwamba mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba alikua mzito kupatanishwa kwa sababu ya kukasirishwa na kitendo cha mama mzazi wa Lulu ambae hakuwahi kufika msibani wala kutuma salamu za pole kwa mama Kanumba.

MKUTANO WA TATU WA WADAU WA NSSF WAANZA RASMI LEO JIJINI ARUSHA

Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka akizungumza na kuzindua wimbo
maalum wa NSSF uliotungwa na Wasanii hapa nchini wajiitao All Stars,mbele ya wadau waliohudhuria mkutano wa 
tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa
AICC,jijini Arusha.Kauli mbiu ya mkutano huo kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akifafanua jambo kwa umakini  mbele ya  Wadau zaidi ya 1000 kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaondelea hivi sasa kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike.. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Crenscentius Magori akifafanua jambo mapema leo asubuhi wakati 
mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo Februari 13,ukiendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Meneja wa kanda na anaeshughulikia Idara mbalimbali za serikali kutoka
NSSF,Rehema Chuma akifafanua namna ya uendeshaji wa shirika hilo kwa  
wadau waliohudhuria mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa
AICC,jijini Arusha.
 Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe akichangia moja ya mada zilizokuwa sikitolewa kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Harold Sungusia akichangia moja ya mada zilizokuwa sikitolewa kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Mmoja wa wajumbe wa NSSF,Peter Sumbi aliyekuwa akifanya kazi shirika la Wildlife Fund akitoa ushuhuda wake,namna alivyopata ajali na kufanikiwa kupata fao lake la ajali kazini kutoka kwa shirika la NSSF na hatimaye kufaidi matunda kupitia mfuko huo.
Pichani ni Mwenyekiti wa wasataafu wa TAZARA,Injinia Mwl.Sango akitoa ushuhuda wake kuhusiana na namna shirika la NSSF lilivyowasaidia wastaafu wa shirika la TAZARA,kupitia mfuko wa pensheni na fao la kujitoa.
Sehemu ya Meza kuu ya mkutano huo.
Sehemu ya Wabunge waliopo kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Mifuko ya Jamii nchini wakiwa kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya watendaji wakuu wa NSSF wakiwa mkutanoni.
 Meneja Mahusiano wa PPF,Lulu Mengele na  Meneja Mahusiano wa SSRA,Sarah Kibondewakifuatilia yanayojiri ndani ya mkutano huo unaoendelea hivi sasa.
 Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini (CHADEMA),Mh Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu akiwa sambamba na Mbunge wa Arumeru Mashariki,Mh Joshua Nasari (CHADEMA) na Wadau wengine wakifuatilia yanayojiri hivi sana kwenye mkutano wa NSSF.
Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali wakifuatilia yanayojiri ndani ya mkutano wa NSS unaoendelea hivi sana ndani ya ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
 Mbunge wa jimbo la Ludewa,Mkoani  Njombe,Mh. Deo Filikunjombe (CCM) akiwa na baadhi ya Wabunge Wenzake wanaohudhuria mkutano huo wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ndani ya mkutano huo ambao umewakutanisha wadau zaidi ya 1000 kutoka sehemu mbalimbali jijini Arusha.
Mwenyekiti wa kikao cha awamu ya kwanza cha Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Bwa.Daudi Msangi akitoa utaratibu kwa Wanachama na wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano huo unaoendelea ,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,kulia kwake ni  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akizungumza jambo na  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crenscentius Magori mapema leo asubuhi kabla ya kuanza kwa mkutano wa shirika hilo.
Wadau.
 Mkutano ukiendelea.  Picha zote na Othman Michuzi

MILLARD AYO AFUNGUKA JUU YA AJALI MABAYA ILIYOWAHI KUMTOKEA MAISHANI.

 Millard Ayo
--
SEHEMU YA KWANZA.

Kama ilivyo kawaida kwa wataalamu wa masuala ya habari na kijamii wa mtandao wa MO BLOG unaotisha kwa sasa, Mhariri Mkuu wa Mtandao huo Lemmy Hipolite na Meneja Mipango Zainul Mzige ‘hamad’ uso kwa uso na mtangazaji maarufu wa Radio na Televisheni hapa nchini Millard Ayo.

MO BLOG:  Kitu kingine ambacho MO BLOG ingependa kufahamu ni kuondoka kwako ITV, fununu zinasema kuwa ulikuwa ni mtiti, ni ya kweli haya?

MILLARD AYO: Ningependa watu wakifahamu ni kuwa mimi sina ugomvi na ITV wala sikuondoka kwa ugomvi.

Kwanza kufanya kwangu kazi ITV naamini Mungu alikuwa anaona na alipanga ndio maana hata hivi sasa kuna uwezekano kuwa nafasi nyingine nilizo nazo maishani kwangu nisingezipata, pengine hata ‘Clouds’ wasingeniona na wasingenifuata.

ITV ndio ilimtambulisha Millard Ayo.

ITV niliondoka vizuri ndio maana nitawaheshimu na nitazidi kuwatangaza vizuri popote nitakapokwenda.

Kwa sasa hapa ‘Clouds Radio’ nafanya show yangu ya ‘Amplifaya’ ambayo ina sehemu inayohusisha Blogs, Facebook na Twitter.

Katika kipengele hicho nasoma sana habari zao wanazo zi’tweet’ na nasema nimezitoa ITV.Kusoma zaidi bofya na Endelea......>>>>>

Prof Muhongo atoa leseni ya madini chunya

pro 
0634e
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akikabidhi leseni ya uchimbaji madini kwa Bw. Roman Lyaruu kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya dhahabu katika Kijiji cha Itewe wilaya ya Chunya. Mhe. Waziri alisisitiza wachimbaji wa madini kulipa kodi zote zinazotozwa na Mamlaka za Serikali ikiwemo mrabaha wa asilimia nne.

Pengo- Sitarajii kuwa Papa


ASKOFU wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, amesema hafikirii kuwa Papa. Kauli ya Pengo ameitoa jana nyumbani kwake, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotaka kujua mtazamo wa Kanisa baada ya Papa Benedi
ct XVI, kutangaza kujiuzulu ifikapo Februari 28 mwaka huu.

Akijibu swali la mwandishi wa gazeti hili bila kueleza kwa kina, Pengo alijibu: “Sifikirii kuwa Papa, na hili halina mjadala.” Akizungumzia alivyochukulia suala la kujiuzulu kwa Papa Benedict XVI, Pengo alisema wamepokea kwa mshangao na mshituko.
Alifafanua kwamba ingawa jambo hilo si mara ya kwanza kwa Papa kujiuzulu, lakini hali kama hiyo iliwahi kutokea karne sita zilizopita. Mwaka 1415, Papa Gregory XII alijiuzulu katika mpango wa kumaliza mgogoro uliokuwepo wakati huo kati ya makadinali wa Nchi za Mashariki kugombea kiti hicho.
“Ni wazi kuwa kitu kinatokea baada ya miaka 600 ni kitu cha kushangaza na kujiuliza na maswali yanapita vichwani mwa watu, lakini hili si jambo la kwanza kutokea. Papa ameweka wazi sababu zake kuwa anajisikia kupungukiwa nguvu si za kiakili wala ugonjwa fulani,” Pengo alisema yeye anaona hatua iliyochukuliwa na kiongozi huyo wa juu wa Kanisa Katoliki, ni jambo la unyenyekevu alionao, kwa kuona ukweli ndani ya nafsi yake.
Viongozi ving’ang’anizi “Ni mfano kwa viongozi wanaong’ang’ania madaraka. Wanakaa madarakani kwa muda mrefu pamoja na kutokuwa na faida kwa watu wao na wakati mwingine hawatambui hilo, wanazidi kuona uongozi ni haki yao na kuona bila wao nchi haipo. Nadhani wanapaswa kujifunza kwa Baba Mtakatifu,” alisema.
Vipi Afrika?
Alipoulizwa kuwa haoni wakati umefika kwa Afrika kutoa Papa, Pengo alisema hisia hizo ni za kisiasa zaidi ya imani ya kidini, kwani Papa huchaguliwa kwa msingi wa Roho Mtakatifu kupitia makadinali na si kwa kujuana.
“Kumchagua Papa ni shughuli inayokwenda na tafakari nzito, na sala na tunafanya tukiwa mbele za Mungu, ni jambo linalofanyika mbele ya msalaba na kila mmoja anaweka kura yake kwa kueleza dhamira yake na Kristo ndiye atahukumu siku ya mwisho,” alisema.
Alisema kutamka kuwa wakati umefika wa kuwa na Papa kutoka Afrika au Muitaliano, ni kumwekea masharti Roho Mtakatifu na kuwa nje ya imani ambayo Roho Mtakatifu ndiye anayetenda kazi.
“Endapo itatokea akachaguliwa Papa kutoa Afrika, basi Roho Mtakatifu atakuwa ameona kuwa ni wakati wa Afrika, hiyo kazi tunamwachia Roho Mtakatifu atende kazi,” alisema.
Alisema hatua ya Papa kujiuzulu si jambo la kutia shaka, bali ni la kujenga imani na kuwa kamwe Kanisa halitasambaratika kwa sababu misingi ya Kanisa haimtegemei mtu mmoja, bali anayechaguliwa anaongoza kwa matakwa ya Mungu.

Tukuyu hapoooooooooo!!


Hii ni mandhar safi ya mji wa Tukuyu     ( Picha na Keny Pino)

sasa Kyela

Safari haikuishia hapo haooo hodi hadi mjini Kyela nako tulikutana na mandhari nzuri na ya kuvutia.
Add caption


Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...