Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amesema tofauti za itikadi za kisiasa zisitumike kuwagawa Watanzania, bali ziwe chachu ya kufanikisha maendeleo.
Ole Sendeka aliyasema hayo jana, wakati wa kuaga mwili wa mama yake Raheli Sendeka kwenye ibada iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Engarenarok jijini Arusha.
Alisema baada ya kutokea kwa msiba huo, viongozi wa kwanza kufika nyumbani kwake kumpa pole walikuwa mbunge na diwani wa Chadema, hivyo amepata somo kuwa tofauti za kisiasa hazipaswi kuondoa umoja na upendo wa Watanzania. Alisema mbunge wa kwanza kufika nyumbani kwake Ngarenaro jijini hapa ni wa Siha mkoani Kilimanjaro (Chadema), Dk Godson Mollel na diwani wa Ngarenaro (Chadema), Issaya Doita.
Alisema yeye ni mkuu wa mkoa anayetokana na CCM, lakini viongozi hao wa Chadema walikuwa wa kwanza kufika na kumpa pole japo pia wengi wa CCM wameshiriki ipasavyo kwenye msiba huo.
“Hata mbunge wangu wa Jimbo la Simanjiro, James Ole Millya (Chadema) ameshiriki kikamilifu kwenye msiba huu na pia gari la diwani wa Loiborsiret, Ezekiel Lesenga Mardadi wa Chadema nililitumia kwenda hospitalini Mount Meru,” alisema Ole Sendeka.
Alisema kuwa Rais John Magufuli amekuwa akizungumza mara kwa mara kuwa ni kiongozi wa Watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa na viongozi kwa ujumla wao wanapaswa kumuunga mkono.
Mwanasiasa huyo alisema sifa za mama yake zilikuwa nyingi, lakini alimkumbuka kwa kumuunga mkono aende shule kusoma kwa kuwa miaka ya 1970 ilikuwa vigumu kwa watoto wa jamii za kifugaji kusoma kisha kukubaliwa na kuwa na heshima kama ilivyo hivi sasa.
“Mama aliniambia soma ili uje kuwa kama Edward Sokoine na alinisindikiza hadi shuleni Orkesumet na kukaa nami kwenye chumba kimoja hadi nikazoea ndipo akarudi nyumbani na kuniacha shule,” alisema Ole Sendeka.
Akizungumza kwenye ibada hiyo, Mkuu wa KKKT Tanzania, Askofu Fredrick Shao aliwataka ndugu wa ukoo wa Ole Sendeka kutumia msiba huo kwa kuzidisha upendo ili kumuenzi mama yao.
Akitoa pole kwa niaba ya Serikali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene alitoa ushuhuda wa kifo cha mama yake miaka tisa iliyopita kilivyomtia uchungu.

No comments:
Post a Comment