Wednesday, October 28, 2015

TOYOTA NDIO GARI MAARUFU ZAIDI DUNIANI


Sasa ni rasmi Toyota ndiyo gari maarufu zaidi duniani. Kampuni hiyo ya kutengeneza magari ya Japan imeipiku Volkswagen kutoka kwenye nafasi ya kwanza ya orodha ya makampuni yaliyouza idadi kubwa zaidi ya magari duniani mwaka huu.

Yamkini Toyota imeuza takriban magari milioni 7.5 katika kipindi cha miezi tisa ya mwaka huu. Wapinzani wao wa karibu Volkswagen kwa upande wao wameuza magari milioni 7.43. Nafasi ya tatu inashikiliwa na kampuni ya kutengeneza magari ya Marekani, General Motors.
GM iliuza magari milioni 7.2 katika kipindi hicho cha miezi 9 ya mwanzo wa mwaka huu. Wadadisi wanasema kuwa sakata ya udanganyifu iliyoikumba kampuni hiyo ya ujerumani itaathiri zaidi mauzo yake katika siku za hivi punde.


Volkswagen ilipatikana na hatia ya kupandikiza programu ya siri katika injini ya magari yake yanayotumia mafuta ya dizel ilikudanganya wachunguzi wa utendakazi wake kuhusina na kiwango cha hewa chafu inayotoa.

Licha ya kushikilia nafasi ya kwanza Toyota bado haijatimiza malengo yake ya kuuza idadi ya magari sawa na ilivyouzwa katika kipindi sawa na hicho mwaka uliopita.
Kampuni hiyo ya Japan iliipiku GM kwa mara ya kwanza mwaka wa 2008. Tangu hapo Toyota imekuwa ikiendelea kunawiri isipokuwa mwaka wa 2011 iliposhindwa kusafirisha magari baada ya dukuduku na hofu kuenea kuwa huenda miale ya sumu ya nyuklia ilikuwa imeenea kwenye magari yao.

Mwaka huo kimbunga kikubwa kiliikumba kisiwa chenye karakana za Toyota Kaskazini Mashariki mwa Japan na kuathiri utendakazi wake.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...