Kocha wa Yanga, Marcio Maximo
amesema mchezaji yeyote mwenye ubinafsi hana nafasi kwenye kikosi chake,
huku akishindwa kujua yupi wa kumuacha kati ya wachezaji wawili wa
kimataifa.
Akizungumza jana mara baada ya mazoezi ya timu
hiyo kwenye Uwanja wa Loyola, Maximo alisema hadi sasa hajaamua wa
kumuacha kati ya Emmanuel Okwi na Hamis Kiiza.
“Kwa sasa siwezi kusema ninayemuacha hadi Septemba
17, nitatangaza nitakayemuacha, ila wachezaji wabinafsi hawatakuwa na
nafasi katika kikosi changu.
“Nataka mchezaji anayejituma kwa moyo,
anayepigania maslahi ya timu kwanza na si kukimbilia maslahi yake peke
yake, tukiwa na umoja tunashinda pamoja, na kama tunapoteza tunaumia
pamoja,” alisema Maximo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Alisema wachezaji anaowahitaji kwenye kikosi chake
ni wale ambao wanajituma, wanajua wajibu wao uwanjani, anataka
wachezaji kucheza kitimu badala ya kumtegemea mtu mmoja.
Mbrazil huyo alisema anataka kuijenga timu hiyo
icheze kitimu zaidi kuliko kucheza kwa kumtegemea mchezaji fulani, kitu
ambacho kinaathari pindi mchezaji husika anapokosekana.
“Nimejifunza mengi hasa kupitia Kombe la Dunia na
kuona jinsi gani timu zilizokuwa zikiwategemea baadhi ya wachezaji
zilivyoathirika tofauti na zile, ambazo zilicheza kitimu,” alisema
Maximo na kuitolea mfano Ujerumani, mabingwa wa dunia.
Aidha, Maximo ambaye anakinoa kikosi cha timu hiyo
akisaidiwa na wasaidizi wake watatu, Mbrazil mwenzake Leonaldo Leiva na
Watanzania Salvatory Edward pamoja Juma Pondamali, ambaye ni wa makipa,
alisema kwa sasa anaingiza mfumo wa timu hiyo kucheza kitimu muda wote
kama ilivyo kwa Wajerumani.
Katika mazoezi ya jana, Maximo aliwapa mazoezi ya
kuwajengea pumzi wachezaji wake ikiwa ni kukimbia kwa spidi na mpira na
kumkabidhi mchezaji mwingine, ikiwa ni pamoja na kufanya ‘pushapu’,
kabla ya kuwapa mbinu za kufunga na kukaba.
Yanga inajiandaa kwa mashindano ya Kombe la Kagame
na Ligi Kuu Tanzania Bara, ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi
Septema, baada ya tarehe ya awali kubadilishwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment