Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU)
cha Dar es Salaam wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni jana.
Sakata la
kutupwa kwa viungo vya binadamu bila kufuata utaratibu jana liligeuka
sinema wakati maofisa wanne wa Chuo Kikuu cha Tiba na Teknolojia (IMTU),
walipofikishwa mahakamani Dar es Salaam.
Maofisa hao ambao ni maprofesa na wahadhiri wa
chuo hicho walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni
wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kushindwa kufukia viroba 83
vya miili ya binadamu.
Baada ya mashtaka hayo kusomwa na taratibu za
dhamana kukamilika huku mmoja wao akishindwa kutimiza masharti,
watuhumiwa hao walirejeshwa kizimbani na kufutiwa mashtaka hayo kwa amri
ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DDP) aliyewasilisha hati ya kutokuwa na nia
ya kuendelea na mashtaka hayo.
Hata hivyo, furaha waliyoipata washtakiwa hao,
Venkat Subbaiah (57), Appm Shankar Rao (64), Prabhakar Rai (69) na
Dinesh Kumar (27) ilikuwa ya muda tu, kwani polisi waliokuwapo
mahakamani hapo waliwakamata tena na kuondoka nao.
Hati ya mashtaka
Akiwasomea mashtaka, Mwendesha Mashtaka Mwandamizi
wa Polisi, Magoma Mtani alidai kuwa washtakiwa hao Julai 2014 katika
eneo la Mpigi Majohe, walishindwa kufukia viroba 83 vya miili ya
binadamu waliyoitumia kufundishia wanafunzi wa udaktari kinyume na
Kifungu cha 128 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 ya mwaka
2002. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz