Mapigano yanaendelea katika mji
uliopo kazkazini magharibi wa Tal Afar nchini Iraq ambapo wapiganaji wa
kiislamu wamekuwa wakikabiliana na vikosi vya serikali tangu jumatatu.
Wanamgambo wa ki sunni kutoka kundi la Jihad la ISIS wanaudhibiti mji huo ambao uko katika barabara inayoelekea Syria.Kwengineko kuna makabiliano makali katika mji wa Baiji ambapo wapiganaji wamekizunguka kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta.
Uzalishaji wa mafuta katika kiwanda hicho umesitishwa na hivyobasi kusababisha ununuzi wa mafuta katika maeneo mengine ya taifa hilo kwa hofu ya kupotea kwa bidhaa hiyo.
Watu wanaomuunga mkono kiongozi wa dhehebu la Shia Muqtada Al Sadr sasa wanaelekea katika mji mkuu wa Baghdad.
No comments:
Post a Comment