DAWA za kienyeji za Kimasai zinadaiwa kusababisha kifo kwa
mkazi wa Moshi Vijijini, Restituta Alen baada ya kuzinunua kutoka kwa
mfanyabiashara na kunywa.Mfanyabiashara wa dawa hizo, Lanyani Lukumay anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mwanamke huyo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz
alisema tukio hilo lilitokea Septemba 30 saa 9.30 alasiri eneo la
Marangu wilayani Moshi Vijijini.
Kwa mujibu wa Kamanda, Lukumay alimuuzia dawa za miti shamba mteja wake kisha kuzinywa na alifariki muda mfupi baadaye.
Hata hivyo haikufahamika ugonjwa uliokuwa ukimsumbua.
“Lukumay anauza dawa za asili ya Kimasai, ambazo ni baadhi ya
mitishamba na vitu vingine, inadaiwa siku ya tukio alimpa dawa mteja
wake huyo ambaye uchunguzi wa awali unaonesha alifariki baadaye,
tunamhoji kujua chanzo cha kifo,”alisema.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa ya
Mawenzi. Polisi inafuatilia kufahamu iwapo dawa za mtuhumiwa huyo
zinatambuliwa na mamlaka zilizopo na kama anatambulika kuendesha
biashara anaifanya kienyeji.
Pamoja na tukio hilo la kifo, pia polisi
imetoa taarifa juu ya mtoto mchanga wa kike anayekadiriwa kuwa na umri
wa kati ya miezi sita na saba aliyekutwa amekufa akiwa katika dampo
lililopo Kata ya Njoro, Manispaa ya Moshi. Polisi imeomba wananchi
kushirikiana na polisi kubaini wahusika wa tukio hilo
No comments:
Post a Comment