Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameitisha mkutano wa dharura wa marais wa nchi za Maziwa Makuu (ICGLR), kujadili hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa waalikwa kwenye mkutano huo ambao pia unatarajiwa kuhudhuriwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
Wakati hali ya usalama Mashariki mwa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikidhoofika, katika siku za karibuni,
uhusiano wa Tanzania na Rwanda umekuwa wa shaka hasa baada ya Rais
Kikwete kuishauri Serikali ya Rwanda kukaa na wapinzani ili kumaliza
mzozo uliolikumba eneo la Maziwa Makuu.
Rais Kikwete alitoa ushauri huo wakati
akiwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika
(AU), zilizofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mkutano wa leo
utafanyika kwenye Ukumbi wa Commonwealth Resort, Munyonyo katikati ya
Jiji la Kampala. Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.
Kwa mujibu wa taarifa Rais Museveni
ameitisha mkutano huo hasa kuzungumzia hatua ya Umoja wa Mataifa
kupambana na Kundi la Waasi wa M23.
Mbali na viongozi hao wa Tanzania na
Rwanda, viongozi wengine wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo wanatoka
Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Sudan, na Zambia.
No comments:
Post a Comment