UBALOZI wa Tanzania, nchini Kenya umesema raia wake moja alijeruhiwa juzi wakati wapiganaji wa Kikundi cha Al Shababu walipoteka jengo la Westgate mjini Nairobi. Taarifa iliyotumwa na Ubalozi wa Tanzania jana, ilimtaja raia huyo kuwa ni Vedastus Nsanzugwanko ambaye ni Meneja katika Taasisi ya Kimataifa ya Child Protection, inayofadhiliwa na Shirika la Kuhudumia Watoto Ulimwenguni, (UNICEF).
Taarifa hiyo,ilisema Nsanzugwanko amejeruhiwa kwa risasi na magruneit katika miguu yake yote miwili na amelazwa hospitali ya Aga Khan.
“Anaendelea kupatiwa matibabu, huku hali yake inaendelea vizuri, hata hivyo ubalozi unaendelea kufuatilia kwa lengo la kupata taarifa zaidi endapo kutakuwapo na Watanzania wengine katika tukio hilo,
“Majeruhi huyu bado yuko hospitali na hatujaweza kumpiga picha,” ilisema taarifa hiyo,”ilisema taarifa hiyo.
Katika hatua nyingine, Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya kwa kushirikiana na Uongozi wa Chama cha Watanzania wanaoishi Kenya (TWA), umeandaa utaratibu maalumu utakaowezesha Watanzania waishio Kenya kujitokeza kwa ajili ya kutoa damu.
Wakati huo huo, Umoja wa Mabalozi wa Nchi za Afrika ulikutana na uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje kwa lengo la kuwasilisha salamu za rambirambi kutoka kwa wakuu wa nchi zao. Taarifa zinasema wajumbe hao walikutana na Rais Uhuru Kenyatta na kutoa
No comments:
Post a Comment