Raha kwa Barca: David Luiz amewaambia Chelsea kuwa anataka kutimkia Barcelona
Taarifa hizi ni kwa mujibu wa gazeti la Mundo Deportivo
Gazeti
ka Hispania la Mundo Deportivo jana lilieleza kuwa Barcelona
wameshatuma ofa ya kwanza ya pauni milioni 25 ambayo Chelsea walicheka
sana, ingawa pesa hiyo inayoonekana ndogo imekubaliwa na mchezaji na
kuonesha nia ya kusepa zake darajani.
Msimamo
wa Luiz umewapa moyo Barca, na sasa wanajiandaa kupandisha dau hadi
kufikia pauni milioni 31, japokuwa itakuwa imepungua pauni milioni 12
kwa kiasi ambacho Chelsea wanahitaji.
Beki
wa Barca ambaye anatoka na Luiz nchini Brazil, Dani Alves amepiga
kampeni kubwa ili asajiliwe na Barca, lakini amekiri kuwa kocha Jose
Mourinho hawezi kumuachia kirahisi Mbrazil mwenzake.
Ripoti kutoka nchini Hispania zinaeleza kuwa beki wa kati wa Chelsea, David Luiz amevunja ukimya na kumuambia meneja wake Jose Mourinho kuwa anataka kuihama klabu yake na kujiunga na Fc Barcelona.
Beki huyo raia wa Hispania ni miongoni mwa wachezaji wanaowindwa na kocha wa Barca, Gerardo Martino majira haya ya kiangazi na lengo lake likiwa ni kupata mlinzi mzuri wa kati kuimarisha ukuta wake uliogeuka kuwa uchochoro msimu uliopita.
Luiz ameichezea Chelsea kwa miaka miwili na nusu akisajiliwa kwa ada ya pauni milioni 25 kutoka Benfica na kuonesha kiwango cha juu na kuwa miongoni mwa mabeki wa bora ligi kuu nchini England.