Maswahiba wawili wakitoka safari marehemu Kanumba na Ray
MWIGIZAJI, mtayarishaji na muongozaji mahiri wa filamu Swahiliwood Vincent Kigosi ‘Ray the Greatest’ hivi karibuni aliangusha bonge la sherehe ya siku yake ya kuzaliwa na kuwakaribishwa rafiki zake na wadau wa filamu katika moja ya Hotel, siku hiyo pia aliweza kumkumbuka swahiba yake marehemu Kanumba na kuhisi uenda angekuwepo siku hiyo.
“Ni
siku ambayo nimesheherekea siku yangu ya kuzaliwa na ndugu zangu wa
karibu na wasanii wenzangu, ni siku ambayo nimekumbuka mambo mengi sana
katika maisha yangu, mara nyingi swahiba wangu marehemu Kanumba siku
kama ya leo ningekuwa naye katika sherehe kama hii, lakin ndio mambo ya
Mungu huwezi kulaumu kilichobaki ni kumuombea Mwenyezi Mungu ampumzishe
kwa amani Amen,” alisema The Greatest.
Katika sherehe hiyo iliyopambwa na vinywaji na malaji kibao
ilijumuisha wasanii nguli katika tasnia ya filamu kama Bonge la bwana,
JB, Maya, Odama, Chikoka na wasanii wengine kibao huku kukiwa na michezo
kadha wa kadhaa ni jambo jema kwa marafiki kukumbuka katika matukio
kama hayo.
CHANZO FILAMU CENTRAL
No comments:
Post a Comment