Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo yaNje na Ushirikiano wa Kimataifa, Edward Lowassa, amemtahadhalisha kujiepusha na kauli za kuunga mkono ushoga.
Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Alisema jana kuwa ushoga na hai za ndoa kwa watu wa jinsia moja vinaweza `kuiharibu’ ziara yake hapa nchini.
Mapema wiki hii, Rais Obama alikaririwa akizungumzia masuala hayo yanayotajwa kuwa ni moja ya haki za msingi za binadamu, alipokuwa Senegal, lakini akapingwa.
“Watanzania hawatalikubali na wataendelea kushikilia uhuru na heshima walizojengewa tangu awali, kwamba ushoga na ndoa za jinsia moja havikubaliki,” alisema.
Akiwa Senegal, Rais Obama alitaka serikali za Afrika kutoa haki kwa mashoga kama inavyotoa kwa raia wengine.
"Ninachotegemea, I pray and hope (ninasali na kutegemea) kwamba kuhusu mashoga na ndoa za jinsia moja, Rais Obama hatarudia kauli aliyoitoa kule Senegal,” alisema.
Aliongeza, "ninasema hivi kwa sababu Tanzania hatuamini katika ushoga, na endapo utawalazimisha Watanzania, watakukatalia na kushikilia uhuru na heshima waliyojengewa toka awali."