Monday, May 20, 2013

HUYU NDIE BINTI ALIYETOROKEA UINGEREZA AKIKWEPA KUTOMASWA NA MFALME MSWATI


Msichana mdogo ameomba hifadhi ya ukimbizi nchini Uingereza baada ya kukataa kwa dharau harakati za ndoa za wake wengi za Mfalme Mswati III wa Swaziland na kugoma kujiunga kwenye nyumba harimu ya wake 13.

Tintswalo Ngobeni, mwenye umri wa miaka 22, alitimkia Uingereza kutoka taifa hilo la kusini mwa Afrika akiwa na umri wa chini ya miaka 18 baada ya kuvuta hisia za mfalme huyo milionea, mtawala maarufu mkandamizaji kwa maisha yake ya anasa.

Ikiwa ni sehemu ya mila za Swazi, Mfalme Mswati III, mwenye umri wa miaka 45, anaruhusiwa kuchagua mke mpya kila mwaka.

Tintswalo, ambaye sasa anaishi mjini Birmingham, alikuwa na umri wa miaka 15 tu wakati Mfalme huyo alipofanya harakati zake baada kumuona kwenye jumba la kifalme la mke wake wa nne, LaNgangaza. Binti huyo alisema 'alitishika' pale alipogundua dhamira zake za ndoa.


Aliongeza: "Alianza kunipigia simu kwenye shule ya bweni. Aliniuliza kama ningetaka kuwa sehemu ya familia ya kifalme. Ilinibidi kukaa kimya kuhusu mashaka yangu lakini nilifahamu sikutaka kuolewa naye na kujitolea maisha yangu kwa mfalme huyo.


"Wake zake wamewekwa kwenye majumba yao, wakizingirwa na walinzi, na hakika hawawezi kwenda kokote isipokuwa tu mfalme akisema hivyo. Kitu pekee wanachofanya ni kwenda Marekani mara moja kwa mwaka, wakati mfalme huyo anapowapatia posho kwa ajili ya manunuzi."

Tintswalo alikuwa amelazimishwa kuachana na maisha ya starehe kwenye shule moja ya bweni huku shangazi yake, ambaye alikuwa mlezi wake mkuu, akisuka mipango ya kutorokea Uingereza kuungana na mama yake, ambaye alihamia mjini Birmingham miaka mitano kabla, akimtoroka mume wake mnyanyasaji.


"Sikuwa na jinsi," alisema. "Hakuna aliyewahi kumwangusha mfalme huyo au kuthubutu kumdharau, hivyo nikatoweka tu."

Tangu kuwasili nchini Uingereza, Tintswalo amekuwa sauti ya upinzani dhidi ya utawala kandamizi za Swazi, ambapo vyama vya upinzani vya siasa vimefungiwa na wanaharakati wamekuwa wakikamatwa mara kwa mara au kushambuliwa.

Hatahivyo, shughuli kuu za Tintswalo, ikiwamo maandamano ya kila wiki nje ya ubalozi wa Swazi mjini London akiwa na kikundi cha Swazi Vigil, zimesikika kwa mamlaka hizo nchini kwake na sasa anaamini yuko kwenye hatari kubwa zaidi kuliko ilivyowahi kutokea.

Alisema: "Hivi karibuni nilipata taarifa kwamba watu wametumwa kutoka Swaziland kuja kunikamata, jambo ambalo hakika linanitisha mno. Kama nikirejea, nitakamatwa au mbaya zaidi huku pale kuna watu ambao wanateseka, kupigwa au kuuawa kwa kujihusisha na siasa."
  
Tintswalo sasa anaishi katika mashaka ya kuweza kurejea nchini Swaziland, baada ya ombi lake la kwanza la hifadhi ya kisiasa nchini Uingereza mwaka 2007 kukataliwa mwaka 2011.

Mwezi uliopita, alikamatwa na kupelekwa kwenye kituo cha kushikilia wahamiaji baada ya miezi 18 ya kuripoti kila wiki katika mamlaka hizo.
Hatahivyo, baada ya shinikizo kutoka TUC na ofisi ya Mbunge wa Birmingham kupitia chama cha Labour, Roger Godsiff, Tintswalo aliachiwa na sasa amekata rufaa wizara ya Mambo ya Ndani.
Godsiff alisema juzi: "Tumefurahishwa mno wanasheria walifanikiwa sana katika kuwezesha kutazamwa upya kwa kesi ya Ngobeni."

Baba huyo wa watoto 27, Mfalme Mswati III alikuwa mgeni kwenye harusi ya William na Kate na pia kwenye sherehe za Miaka 50 ya Malkia wakati wa majira ya joto mwaka jana.

Mke wa sita wa mfalme huyo alitoroka kutoka kwenye jumba hilo harimu mwaka jana, akielezea miaka kadhaa ya 'machungu na udhalilishaji wa kimwili' uliofanywa na mume wake. 
  
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani alikataa kuzungumzia chochote.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...