UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
Academic Staff Assembly
Utangulizi
Wapendwa
waandishi wa habari. Tunaomba kupitia ninyi tuweze kuongea na
watanzania wenzetu kuhusu hali ya amani ilivyo nchini mwetu kufuatia
kila aina ya dalili ya watanzania kukosa uvumilivu wa kidini. Tunatambua
kuwa serikali yetu imefanya mambo mazuri mengi tu nchini, hilo hatuna
mashaka nalo; hata hivyo kama watanzania tunadhani kuna baadhi ya mambo
hayaendi sawa. Hivyo basi, tunaomba kuchukua nafasi hii kuelezea
wasiwasi wetu kuhusu migogoro hii ya kidini inayozidi kukua nchini.
Migogoro
hii ilianza kuvuka kama moshi lakini sasa inaanza kulipuka na kusambaa
zaidi. Tumeshuhudia uchomaji moto wa kanisa kule Mbagala, kumwagiwa
tindikali shekhe mmoja kule Zanzibar na Shekhe mwingine kuuawawa,
kuchomwa makanisa Zanzibar, kupigwa risasi viongozi wa kikristo kule
Zanzibar na pia mgogoro wa kuchinja huko Geita ambako tumeshuhudia
mchungaji mmoja akiuawa.
Mbali
na hayo, kuna matukio kadhaa kwenye shule zetu za sekondari yakihusisha
migogoro ya kidini kati ya wakristo na waislamu. Haya tumeshahudia
yakitokea sekondari za Bagamoyo, Ndanda, Kibiti, Ilboru na kwingineko.
Pia yapo malalamiko yasiyo rasmi kuhusu udini kwenye sehemu za kazi na
kwenye taasisi mbalimbali za serikali. Wapo wanaodai kuwa baadhi ya
taasisi binafsi, za kidini na hata za serikali zinazohudumia watanzania
wengi zimekuwa zikiajiri wafanyakazi kwa misingi ya kupendelea dini
fulani fulani. Jambo hili hata kama ni la kuzungumzwa tu, ni vema
likafanyiwa kazi maana hisia hizi zikipanuka hujenga chuki na
kusababisha watanzania wasielewane.
No comments:
Post a Comment