CHAMA Cha
Mapinduzi (CCM) kimesema kauli ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa kwamba kuna baadhi ya
watumishi wa vyombo vya dola wanaripoti kwake, kimesababisha baadhi ya
wananchi kukosa imani na vyombo hivyo.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Mkoa Maalum wa CCM Dar es Salaam baada ya kikao
chao kutathimini mambo na matukio mbalimbali yanayolitikisa taifa kwa
sasa.
Katika
taarifa yao iliyosainiwa na Katibu wa Wilaya ya Dar es Salaam (ya
kisiasa - CCM), Daniel Zenda ilisema kuwa Dk. Slaa amekuwa akitoa kauli
hizo mara kwa mara tangu wakati wa kampeni za urais mwaka 2010, lakini
hajaitwa kuulizwa wala kuchukuliwa hatua.
“Lakini
pia kauli ya Dk. Slaa imesababisha wananchi wakose imani na Idara ya
Usalama na zaidi kupoteza imani juu ya uwezo wa serikali kuwalinda na
kuwahakikishia usalama wa maisha yao, ambapo ni jukumu la kikatiba la
serikali,” ilisema taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment