Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964, Zanzibar.
Ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi Aprili 26, 1964, na Aprili 27, 1964 viongozi hao walikutana katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Dalaam kubadilishana hati za Muungano.
Sheria za Muungano ilitamka kwamba, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zililazimika, kuwa dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jina ambalo lilibadilishwa Oktoba 28, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia sheria ya Jamhuri ya Muungano, sheria namba 61, ya mwaka 1964.