Ulinzi mkali leo umewekwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Dodoma ili kuzuia wafuasi wa Chadema waliokwenda kusikiliza kesi inayomkabili mgombea ubunge wa jimbo la Dodoma mjini Benson Kigaila na kusababisha lango la kuingilia lifungwe.
Kigaila
na wenzake 10 wanakabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kumpiga na
kumjeruhi polisi, kufanya maandamano bila ya kibali na pamoja na kutoa
lugha za matusi katika kituo cha polisi makosa ambayo watuhumiwa hao
waliyakana yote.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi katika
Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, James Karayemaha, Wakili wa Serikali
Beatrice Nsana amesema kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa yote
Septemba 25 mwaka huu majira ya jioni.
Nsana amesema
kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba mahakama ipange tarehe
ya kuanza kusikilizwa ambapo mahakama imekubali na kupanga Oktoba 12
mwaka huu huku dhamana ikiwa wazi.
Mara baada ya
kutimizwa kwa masharti ya dhamana kwa washitakiwa wote, viongozi hao
waliondoka chini ya ulinzi mkali wa polisi na kusindikizwa hadi katika
ofisi za kanda za chama hicho ambako Kigaila alizungumza na waandishi wa
habari. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.