Thursday, July 23, 2015
YANGA SC YAZINDUKA, YAWAPIGA 3-0 TELECOM, MSUVA NA TAMBWE WAKOSA PENALTI
Yanga imerejea katika michuano ya Kagame baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Telecom ya Djibout katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jana.
Katika mechi yake ya kwanza ya michuano hiyo, Yanga ilianza kwa kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Gor Mahia huku mshambuliaji wake Donald Ngoma akilambwa kadi ya nyekundu.
Malimi Busungu ndiye shujaa baada ya kufunga mabao mawili huku Geofrey Mwashuya, akifunga bao la tatu.
BENTEKE AHAMIA LIVERPOOL RASMI
Christian Benteke
Timu ya Livepool imekamilisha kumsajili rasmi mshambuliaji mwenye asili ya Jamuhuri ya Kidemokrasia wa kongo Christian Benteke kutoka Aston Villa kwa kitita paundi milion 32.5.
Benteke alikubali mkataba wa muda mrefu na kuwa mchezaji wa pili kununuliwa kwa gharama kubwa huko England.
Mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji ameifunga magoli 49 katika mechi 101 alizocheza kwenye timu yake ya zamani ya Aston Villa.
Wednesday, July 22, 2015
KURA ZAANZA KUHESABIWA BURUNDI
Rais Pierre Nkurunziza
Shughuli ya kuhesabu Kura imeanza nchini Burundi kufuatia uchaguzi wa urais ambao umeshutumiwa na wengi nchini humo na hata kimataifa.
Rais Pierre Nkurunzinza anatarajiwa kupata ushindi mkubwa kwa muhula wa tatu huku upinzani ukisusia kabisa kura hiyo.
Huku hayo yakijiri Marekani na Uingereza wamekashifu kura hiyo wakisema kuwa haikuwa ya huru na haki.
Marekani kwa upande wake imependekeza kugawana madaraka huku ikitishia kuchukua hatua dhidi ya Burundi iwapo muafaka hautapatikana.
Tuesday, July 21, 2015
UCHAGUZI UMEEANZA NCHINI BURUNDI
Uchaguzi wa urais umeanza Burundi
Baada ya ghasia na maandamano ya miezi kadhaa, hatimaye raia nchini Burundi sasa wamefika katika vituo vya kupiga kura ili kumchagua rais wao.
Watu wawili wameuwawa usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu Bujumbura.
Foleni zimeonekana katika vituo vya kupigia kura
KESI YA RAIS WA ZAMANI WA CHAD YAAHIRISHWA HADI SEPTEMBA
Rais wa zamani wa Chad arejeshwa kortini
Kesi ya kihistoria dhidi ya Kiongozi wa zamani wa Chad Hissene Habre iliyokuwa imerejeshwa mahakamani leo nchini Senegal sasa imeahirishwa hadi mwezi Septemba.
Mahakama imetoa muda huo kwa wakili wapya wa kiongozi huyo wa zamani wa kimla kujiandaa kwa kesi inayomkabili ya makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu, ukatili na uhalifu wa kivita.
Bwana Habre ambaye amekataa kuitambua mahakama hiyo alikataa kuzungumza mahakamani huku akiwashauri wakili wake wasimwakilishe mahakamani.
KITIMTIM MICHUANO YA KLABU BINGWA ULAYA
Michuano ya Klabu Bingwa Ulaya inaendelea tena hii leo kwa timu zile zinacheza round ya kwanza ambapo Dila Gori ya Geogia itakuwa na kibarua kigumu itakapoumana vikali na Partizan Belgrade ya Serbia.
Huku FC Pyunik ya Armenia ikikutana uso kwa uso na Molde ya Norway.
Milsami ya Boldova itapimana nguvu na Ludo Bulgaria.
Mechi nyingine za Klabu Bingwa barani Ulaya hapa chini
Dila Gori v Partizan Belgrade 13:30
FC Pyunik v Molde 15:00
Milsami Orhei v Ludo Razgd 16:00
HJK Helsinki v FK Ventspils 17:00
Maccabi Tel Aviv v Hibernians FC 18:30
Lincoln Red Imps v FC Midtjylland 19:00
Vardar v Apoel Nic 19:00
Zalgiris v Malmö FF 19:10
Crusaders FC v Skenderbeu Korce 19:45
Monday, July 20, 2015
NCHIMBI AENGULIWA KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA UBUNGE...!!!
Dr. Emmanuel Nchimbi
KAMATI ya Siasa ya chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Songea Mjini imetupilia mbali fomu ya mgombea UBUNGE Dr. Emmanuel Nchimbi kwa madai kuwa fomu hiyo haikuwa na vigezo na kusababisha kushindwa kuijadili baada ya mgombea kutokuwepo kwenye kikao hicho.
Akizungumza asubuhi ya leo ofisini kwake katibu wa CCM wa Wilaya hiyo Juma Mpeli alisema kuwa mpaka jana majira ya saa kumi jioni fomu za kugombea ubunge jimbo la Songea Mjini zilipokelewa tisa (9) lakini fomu moja ya Dr. Nchimbi ilikuwa imechukuliwa na mmoja wa wakazi wa Songea na ikalejeshwa siku hiyo hiyo ikiwa imejazwa.
Alisema kuwa fomu hiyo ya mgombea ilishindikana kujadiliwa kwa kuwa mgombea mwenyewe Dr. Nchimbi hakuwepo kwenye kikao ambacho wagombea wote waliitwa kujadiliwa kadri ya maelezo waliyoyatoa kwenye fomu ya kugombea ubunge kwenye jimbo hilo.
MAN U KUTOONGEZA WASHAMBULIAJI
Kocha Mkuu wa Manchester United Louis Van Gaa
Kocha mkuu wa Manchester United Louis Van Gaal ametamba kuwa hatanunua mwingine kwani alio nao kwa sasa wanatosha wakiongozwa na Wayne Rooney.
Pamoja na Wayne Rooney washambuliaji wengine waliobaki ni Javier Hernandes Chicharito, na James Wilson baada ya mshambuliaji mpachika magoli Robin Van Persie kujiunga na Fenerbahce ya Uturuki hivi karibuni na Radamel Falcao mkopo wake kumalizika.
Van Gaal anatarajia kumtumia Rooney kama mshambuliaji pekee pale mbele ambapo atasaidiwa na Mephis Depay aliyesajiliwa wakati wa majira ya joto kutoka PSV Eindhovenya Uholanzi.
Van Gaal anatamba kuwa Depay anaweza kuwa mshambuliaji wa katikati tofauti na alivyokuwa akitumika wakati alipokuwa PSV.
Saturday, July 18, 2015
WAZEE WA KIMILA MONDULI WAMUANGUKIA LOWASSA
Wazee wa kimila wa jamii ya wafugaji wa Kimaasai (Malaigwanan) kutoka Wilaya ya Monduli wamemuomba waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kubaki na kuendelea kuwa kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa sababu ndicho kilichomlea na anakijua.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Monduli kwa niaba ya Malaigwanan, Mzee Joseph Mesopiro kutoka Kata ya Sepeko wilayani humo alisema viongozi wa mila wanakusudia kutuma ujumbe maalumu kwa Lowassa kumshauri asihame CCM kama baadhi ya watu aliowaita wapambe wanavyomshauri.
“Sote Monduli tumesononeka kwa jinsi vikao vya chama vilivyomtendea mbunge wetu. Bado tunampenda kama ambavyo tunakipenda chama chetu. Tunaamini ataendelea kubaki CCM na kupigania ushindi wa chama katika uchaguzi ujao,” alisema Mzee MMesopiro
TUNAWATAKIA EID MUBARAKA WATU WOTE
Leo ni sikukuu kubwa sana duniani... ina maana kubwa sana kwa waislam na watu wote duniani.
Kwakulijua hili Jambo Tz tunachukua nafasi hii kuwatakia sikukuu njema watanzania wote na dunia kwa ujumla.
OBAMA KUTOTEMBELEA KIJIJI CHA BABA YAKE
Barack Obama
#ObamainKenya ndilo neno linalotawala mitandao ya kijamii nchini Kenya huku rais huyo akitarajiwa kulitembelea taifa hilo.
Hata hivyo wakaazi wa kijiji cha Kogelo ambapo babaake Obama alizaliwa na kulelewa sasa hawatalazimika kufanya maandalizi ya aina yoyote kufuatia ziara hiyo baada ya balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec kusema kuwa rais huyo hatozuru kijiji cha Kogelo.
''Ana mda mchache sana kwa hivyo basi atakuwa nairobi pekee'', alisema bwana Godec akizungumza na runinga ya KTN.
Bibiye Obama Sarah Obama alikuwa amejiunga na wakaazi wa Kogelo akimtaka Obama kuwatembelea kulingana na ripoti za kituo cha habari cha Capital fm.
Friday, July 17, 2015
MSAIDIZI WA NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA AJIUNGA NA CHADEMA
Bw. Jumanne Juma Msunga.
MSAIDIZI wa Naibu Katibu Mkuu wa (CCM) Bara, Jumanne Juma Msunga ametangaza rasmi kuhama CCM na kujiunga na CHADEMA, kwa madai kuwa CCM ni chama cha kudhulumu haki za wanachama wake.
Akitangaza uamuzi wake huo jana mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi za CHADEMA Mkoani Singida, Msunga alisema ameamua kujinga na CHADEMA, huku akidai kuwa CCM haikutenda haki katika mchakato mzima wa kumpata Mgombea wa nafasi ya Urais.
Alisema CCM haina shukrani kwani imejaa dhuluma kwani katika mchakato huo baadhi ya Wagombea walikatwa bila kujieleza mbele ya kamati husika.
WATU ZAIDI YA 40 WAFA KATIKA MLIPUKO NIGERIA
Wapiganaji wa Boko haram
Wafanyakazi wa uwokoaji Nigeria wanasema katika eno la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo katika mji wa Gombe watu arobaini wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya milipuko kutokea kwenye soko katika eneo hilo.
Mlipuko wa kwanza umetokea nje ya kwenye maegesho nje ya duka la viatu, na kufuatiwa na mlipuko mwingine muda mfupi baadae.
Mmoja ya wafanyakazi wa uokoaji miongoni mwa waliouwa ni wanawake na watoto.
Mashuhuda wa tukio hilo amesema hali ni mbaya kwenye mitaa ya Gombe.
WANAJESHI WANNE WANAMAJI WAUAWA MAREKANI
Mtu mwenye silaha amewaua askari wanne wa jeshi la wanamajiwa Marekani katika shambulio lililofanywa kwenye majengo mawili ya jeshi hilo katika mji wa Chattanooga, Tennessee.
Wanajeshi hao wote waliuawa katika jengo moja. Maafisa nchini humo wameyaita mauaji hayo kuwa ni Shambulio la ndani.
Shirika la Upelelezi la Marekani FBI linalochunguza mauaji hayo, limesema halijajua bado kilichosababisha shambulio hilo.
Subscribe to:
Posts (Atom)