Suala
la baadhi ya wafadhili wa TZ kubana au kuchelewesha fedha walizoahidi
kusaidi bajeti ya nchi linaendelea kuiumiza serikali.
Waziri Mkuu
wa nchi hiyo, Mizengo Pinda, amesema umefika wakati sasa kwa Tanzania
kujitegemea kwa mapato ya ndani kwa asilimia 100 badala ya kuegemea kwa
wahisani ambao amedai wanakuwa na maslahi yao katika kusaidia.Hivi karibuni wahisani wamesitisha kutoa fedha hizo kuishinikiza Tanzania kuchukua hatua dhidi ya upotevu wa mabilioni ya fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania katika mazingira yanayodaiwa kuwa ya rushwa.
Kiongozi huyo mwandamizi wa serikali ya Tanzania ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kurejea kutoka ziara ya ughaibuni ambako alihudhuria mikutano katika nchi mbali mbali akishughuli maswala kadhaa ikiwa ni pamoja na uwekezaji. Asante kwa kutembelea blog hii, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz