Waziri wa uchukuzi,
Mhe Harrison Mwakyembe
Kufuatia
ajali ya mabasi iliyoua takbriban watu 39 Musoma, Waziri wa uchukuzi,
Mhe Harrison Mwakyembe amefanya maamuzi kadhaa, kupunguza ajali za
barabarani. Ifuatayo ni kauli yake:
1.Tunaanza
na hawa waliopata ajali, nimeelekeza na najua vyombo vinavyohusika
Polisi pamoja na SUMATRA watatekeleza… kwanza kuzifungia kampuni za haya
mabasi ya J4 na Mwanza Coach wasijihusishe na usafirishaji wa abiria
tena, hatuwezi kuwa tunapata ajali za kijingajinga namna hiyo, nimeliona
eneo lenyewe liko wazi kabisa lakini ni watu tu wameamua, dereva wa
huku anamuona mwenzake na kusema mimi lazima anipishe’ – Dr. Mwakyembe
2.
Tumeelekeza Wafanye uhakiki wa madereva wao wote na tunahitaji picha
zao lakini vilevile tunahitaji mikataba ya kazi, hatutaki mabasi ya
kupeleka abiria yaendeshwe na watu tu kwa majaribio, nataka ushahidi wa
kila dereva kwamba amejiunga na hii mifuko ya akiba ya Wafanyakazi,
tuone kabisa mchango wa Mwajiri na mfanyakazi kila mwezi’
3.
Nimeagiza lazima tuangalie BIMA ya hiyo gari, unajifikiria mwenyewe tu
ukipoteza gari ulipwe kidogo gari yako lakini hufikirii kuhusu
binadamu…. bila comprehensive haendeshi mtu gari kuchukua abiria.
Tamasha
la Fiesta lililokua lifanyike Ijumaa hapa Musoma sasa imefahamika
litafanyika Jumapili ya kesho September 7 2014 ambapo pia imehamasishwa
kwa wingi watu kujitokeza ili mapato hayo yapelekwe kwa ndugu
waliopoteza watu na majeruhi ajalini. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz