Tuesday, September 17, 2013

MWANAMUZIKI WA TAARAB AHMED MGENI AFARIKI DUNIA LEO ALFAJIRI

 
Mwimbaji wa kundi la Zanzibar Njema Mordern Taarab Ahmed Mgeni amefariki dunia leo alfajiri (September 17) katika Hospitali ya Mnazi mmoja, Kisiwani Zanzibar alikolazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua.

Akiongea katika kipindi cha Leo Tena ya Clouds Fm mkurugenzi mwenza wa Zanzibar Njema Modern Taarab Ally Ngereja amesema msiba uko Amani Fresh, Zanzibar ambapo ni kwa baba yake na atazikwa leo (September 17) saa kumi jioni.

Marehemu aliwahi kutamba na nyimbo nyingi ikiwemo sitetereki inayofanya vizuri mpaka sasa.

KESI YA SHEIKH PONDA, AKOSA DHAMANA, KESI YAHAIRISHWA HADI OKTOBA 1

ponda_26617.jpg
Sheikh Ponda Akishuka kwenye basi la Magereza tayari kuingia Mahakamani Kusikiliza kesi yake inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro. Sheikh Ponda alishatikiwa katika Mahakama Hiyo akikabiliwa na Mashtaka Matatu Ambayo inadaiwa aliyatenda Mkoani Morogoro katika Mkutano Hadhara mwezi uliopita. Kesi hiyo imearishwa tena Mpaka Tarehe 01.10.2013. Sheikh Ponda amenyimwa Dhamana na amerudishwa Rumande.

WATUHUMIWA WA MAUAJI YA BILIONEA ERASTO MSUYA WAKUTWA KWA SANGOMA

Jeshi la polisi mkoa wa kilimanjaro linawashikilia watu wanne zaidi wakidaiwa kuhusika na mauaji ya mfanyabiashara bilionea wa madini ya tanzanite Arusha Erasto Msuya 43 wawili kati yao walikutwa kwa mganga wa kienyeji (sangoma) wakifanyiwa zindiko ili wasikamatwe na vyombo vya dola.

Pia jeshi limenikiwa kunasa bunduki aina ya SMG yenye namba za usajili KJ10520,inayoaminika kutumika katika mauaji hayo.Msuya aliuawa kwa kupingwa risasi zaidi ya 10 kifuani Augost 7mwaka huu,katika eneo la mijohoroni wilayani Hai.

Akizungumza na waandishi wa habari jana,kamanda wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Robert Boaz aliwataja watuhumiwa kuwa ni Sadiki Jabiri 32 mkazi wa Dar es Salaam na Lang'angata wilayani Hai .

KINANA AMPONZA BALOZI WA CHINA... CHADEMA KUMSHITAKI KWENYE MAHAKAMA YA KIMATAIFA

http://3.bp.blogspot.com/-tB-YS2RGEHk/UjfrTKmUq2I/AAAAAAAAl3k/wO2eYdRF-0M/s1600/1.png
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kitamshitaki Balozi wa China nchini, Lu Younqing Umoja wa Mataifa (UN) kwa kukiuka Mkataba wa Vienna (Vienna Convention) wa mwaka 1964 ambao unaeleza uhusiano wa kibalozi kati ya nchi na nchi.

Aidha, kimesema kitaiandikia barua Serikali ya China ili kutaka ufafanuzi kama imemtuma Balozi wake kufanya kazi ya uenezi siasa kwenye vyama.


Tukio la Balozi huyo kuhudhuria mkutano wa hadhara wa CCM lilitokea Septemba tisa mwaka huu kwenye mkutano wa chama hicho uliofanyika Wilaya ya Kishapu Shinyanga, ambapo Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana alimtambushisha balozi huyo huku akiwa amevaa sare za chama hicho.


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri kivuli wa mambo ya nje ambaye pia ni Mbunge wa Nyamagana Jijini Mwanza, Ezekiel Wenje alisema Chadema wameamua kuchukua hatua hizo ili kukomesha vyama vya siasa kutumia mabalozi kama wawakilishi wa vyama vyao kwa kufanya uenezi kwenye mikutano ya siasa.

HATMA YA DHAMANA YA PONDA LEO...!!!

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro, leo inatarajiwa kuamua iwapo Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shekhe Ponda Issa Ponda, anastahili dhamana au la, kutokana na kesi inayomkabili.  
Shekhe Ponda alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Agosti 19 na kusomewa mashitaka matatu ya uchochezi yanayomkabili. Upande wa mashitaka ulidai mahakamani hapo kuwa utaleta mashahidi 15 na vielelezo vitatu, ili kuthibitisha mashitaka hayo. 
Baadhi ya vielelezo vitakavyotolewa mahakamani hapo ni pamoja na DVD mbili, kibali kilichotolewa Agosti mosi cha kongamano la Kiislamu, kutoka kwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Morogoro (OCD) na Hati ya Hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. 
Kesi hiyo ya jinai namba 128 ya mwaka 2013, iko mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa Morogoro, Richard Kabate. Shekhe Ponda katika kesi hiyo, anatetewa na mawakili watatu wakiongozwa na Wakili Juma Nasoro, wakati upande wa mashitaka, ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Benard Kongola.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE SEPTEMBA 17, 2013

DSC 0094 87348
DSC 0095 5e40c
DSC 0096 f0fee

LIVERPOOL YABANWA YATOKA SARE NA SWANSEA CITY 2 - 2

StevenGerrard_5fee6.jpg
katika mechi hiyo Swansea City ndiyo walikuwa wakwanza kuanza kupata bao lililofungwa na Jonjo Shelvey dakika ya pili tu ya mchezo, lakini katiuka dakika ya 4 tu Daniel Sturridge alisawazisha nae Victor Moses akaipatia liverpool goli la pili kunako dakika ya 37. Bahati ikawa kwao Swansea City kwa kupata goli la pili kupitia kwa Michu katika dakika ya 63 na kuufanya mchezo kuisha kwa sare.

SERIKALI YAPINGA KESI YA WAZIRI MKUU PINDA


Kesi inayomkabili waziri mkuu Mizengo Pinda na mwanasheria mkuu wa serikali imetajwa mahakamnai kwa mara ya kwanza ambapo wamewasilisha pingamizi la awali dhidi ya kesi ya kikatiba waliyofunguliwa na kituo cha msaada wa kisheria na haki za binadamu kwa kushirikiana na chama cha wanasheria Tanganyika.


Katika kesi hiyo namba 24 ya mwaka 2013, LHRC na TLS,wanadai kuwa Pinda alivunja katiba kutokana na kauli aliyoitoa bungeni hivi karibuni wakidai kuwa ni amri kwa vyombo vya utekelezaji wa sheria kuwapiga wananchi wakati wa vurugu.
 
Hata hivyo Pinda na mwanasheria mkuu kwa pamoja katika majibu yao ya madai hayo, wamewasilisha pingamizi la awali ambapo pamoja na mambo mengine wamedai kuwa walalamikaji na watu walioorosheshwa katika kesi hiyo hawana mamlaka kisheria kufungua kesi hiyo.
 
Kesi hiyo inasikilizwa na jopo la majaji watatu likiongozwa na jaji kiongozi, Fakihi Jundu akisaidiana na jaji Dk Fauz Twaib na jaji Augustine Mwarija ambapo upande wa wadaiwa uliwakilishwa na mawakili wa serikali wakuu watatu, Nickson Mtingwa, Sarah Mlipana na Alesia Mbuya.

PAROKO ANSELMO MWANG'AMBA: NILIMWONA ALIYENIMWAGIA TINDIKALI’

padriParoko wa Parokia  ya Roho Mtakatifu Cheju Zanzibar, akisaidiwa na Frateri, Richard Haki kupumzika kitandani baada ya kuzungumza na waandishi katika katika Wodi ya Kibasila iliyopo katika Hosipitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijni Dar es Salaam jana.Picha Salim Shao 
…………….
Dar es Salaam/Zanzibar.
Padri wa Parokia ya Mpendae ya Kanisa Katoliki Zanzibar, Anselmo Mwang’amba amesema kuwa alimwona mtu aliyemwagia tindikali na kumsababishia majeraha na kueleza kuwa anashangaa kuona polisi hawajamkamata hadi sasa.

Akizungumza jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kwenye Wodi namba 16, Kibasila alipolazwa, Padri Mwang’amba alisema baada ya kumwagiwa tindikali, alimwona mtu huyo akikimbia kuelekea katika nyumba moja jirani.

“Kwa kuwa mimi nilikuwa na taharuki na maumivu, sikuweza kuendelea kumfuatilia, ila dereva aliyenikimbilia kunipa msaada aliniambia kwamba alimwona mhusika akikatiza kwenye uchochoro hadi alipoingia kujificha kwenye nyumba iliyopo jirani na eneo hilo,” alisema.

Alisema majeraha aliyoyapata wakati akitokea katika duka la huduma za mawasiliano ya mtandao la Shine Shine saa 10.15 jioni, ambayo yanamsababishia maumivu makali, hayawezi kumfanya aikimbie Zanzibar, kwa kuwa hata Yesu Kristo wakati alipokuwa katika kazi za utumishi duniani alipata mateso makali kuliko yake.

Monday, September 16, 2013

WAMALAWI WAMIMINIKA KATIKA OFISI ZA UHAMIAJI JIJINI DAR KWAAJILI YA KUJIORODHESHA UHALALI WA KUISHI TANZANIA


Raia wa Malawi wakiwa katika foleni ya kuingia kujiandikisha katika Idara ya Uhamiaji, Mkoa wa Dar es Salaam jana kuhusu zoezi linaloendelea la kuwatambua wahamiaji haramu jijini Dar es Salaam. Mamia ya wakazi hao walimiminia katika ofisi hizo leo kujiorodhesha ikiwa ni agizo la Rais Jakaya Kikwete.
Akina mama na watoto wakisubiri kujiorodhesha.
Ofisa wa Uhamiaji akiwaelekeza jambo Raia wa Malawi. Credits: Father Kidevu Blog

MSANII DR.CHENI ALAMBA DILI NONO ZA SIMU MPYA ZA PANTECH....!!!




Dr. Cheni   Muigizaji maarufu wa filamu Swahiliwood Muhsin Awadh(Dr.Cheni) ameteuliwa kuwa balozi wa simu mpya aina ya Pantech ambazo zimeanza kuingia nchini. Muigizaji huyo amesainishwa deal hilo la mwaka mmoja ambapo atakuwa katika matangazo na promotions za simu hizo. Akizungumza na Millardayo Dr. Cheni alisema "Simu inaitwa Pantech, ni simu mpya kabisa na ina operating system ya Android version mpya. Ukizingatia sasa hivi internet ndiyo kila kitu kwenye simu za mkononi, Pantech inatumia 4G na LTE kwenye connection ya internet. Kitu kingine kizuri ni kwamba simu hii ina uwezo wa kujichaji na nguvu za jua. Sasa jua letu hatutalichukia tena na pia ina camera nzuri ambayo inaitwa Spy camera yenye uwezo wa kupiga picha mbali sana"

Star huyo wa filamu za Nipende Monalisa, Jesica na Majanga aliendelea kwa kusema " Majukumu yangu hasa ni kuhakikisha simu hii watu wanatambua uwepo wake. Matangazo na promotion zinapofanyika nitakuwa na shiriki kikamilifu kabisa. Wamenipa mkataba wa mwaka mmoja kwa sasa na swali lako la thamani ya mkataba wangu naomba niweke kapuni kwasasa, ila millardayo.com itakuwa ya kwanza kujua thamani yake muda wa kuweka wazi ukifika. Ninachoweza kukwambia hivi sasa ni bei tu ya simu hizi ambayo ni Tsh 250,000 tu"

Wasanii wengi wakiwemo wa filamu siku hizi wanaanza kufaidi umaarufu wao baada ya kampuni mbalimbali kuanza kufanya nao kazi katika matangazo ya bidhaa zao kama mabalozi, wiki iliyopita Yobnesh Yusuph(Batuli), Rose Ndauka, Slim Omar na Single Mtambalike(Richie) walisainishwa mkataba wa kuwa mabalozi wa wa soko la hisa la Dar es salaam/ Dar es salaam Stock Exchange(DSE), King Majuto na JB ni baadhi ya wasanii wengine wa filamu ambao nao wana mikataba na makampuni katika kutangaza huduma na bidhaa za makampuni hayo. Katika mkutano na media........................

SUGU: "NDUNGAI ALIAMURU ASKARI WANIPIGE BUNGENI..."



NI kauli iliyotolewa na Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’
 Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema tukio la kupigwa ngumi na askari ndani ya Ukumbi wa Bunge lilisababishwa na  amri ya Naibu Spika, Job Ndugai na wala siyo askari.
Aidha Sugu alisema ilikuwa vigumu kuvumilia konde alilopigwa na askari wakati akitolewa nje kwenye vurugu zilizotokea bungeni hivi karibuni, ndiyo maana aliamua kulipiza kisasi kwa kutaka kumpiga ngumi na si kichwa kama anavyodai  askari.
‘Sugu’ alitoa kauli hiyo  wakati akiwahutubia wakazi wa Chunya Mjini kwenye mkutano wa hadhara ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, Dk Willibrod Slaa ambapo viongozi hao wapo ziarani  mkoani Mbeya  wakifanya  mikutano na wananchi kwa lengo la kuwaeleza ukweli wa kilichomtokea Sugu na  wabunge wengine bungeni hivi karibuni.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 16, 2013

DSC 0389 3dbb0
DSC 0390 e0ea2

MBOWE, LIPUMBA NA MBATIA WAMBANA JK

mbowe 23301
Mshikamano wa vyama vya upinzani katika kupinga Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa 2013 umehamia nje ya Bunge na sasa vyama hivyo vimetangaza kuanza kampeni ya kuuhamasisha umma kudai maridhiano kabla ya kuendelea na mchakato wa Katiba Mpya.
Jana wenyeviti wa vyama hivyo; James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Freeman Mbowe (Chadema) na Profesa Ibrahim Lipumba (CUF) walikutana na waandishi wa habari na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kutosaini muswada huo kuwa sheria, hadi pale kutakapokuwa na maridhiano ya pande zote husika.
Walisema muungano wao ni mwanzo wa kuunganisha umma wa Watanzania kufanya uamuzi wa kunusuru walichokiita "utekaji madaraka na mamlaka ya nchi kutoka kwa wananchi" hivyo wanaitaka Serikali kurekebisha kasoro zinazojitokeza katika mchakato huo.
Akitoa tamko la pamoja kwa niaba ya viongozi wenzake, Profesa Lipumba alisema wanachopigania ni kuurejesha mchakato wa Katiba Mpya mikononi mwa umma, kwa maelezo kwamba suala hilo kwa sasa limehodhiwa na CCM.
"Rais Kikwete asisaini muswada huu, aurejeshe bungeni ufanyiwe marekebisho yenye kujenga kuaminiana na mwafaka wa kitaifa kwenye mchakato wa mabadiliko ya Katiba. Hatutakwenda kumwona ila aurejeshe bungeni,"alisema Lipumba na kuongeza:

Sunday, September 15, 2013

KESI YA MASOGANGE HUKO AFRIKA KUSINI NA HII NDIYO RIPOTI YA KINACHOENDELEA.

Mapema Dar es salaam jana Waziri wanchi ofisi ya waziri Mkuu sera na uratibu wa shughuli za Bunge Wiliam Lukuvi alisema Serikali inafuatilia kwa karibu kesi zinazowahusisha Watanzania waliopo nje ya  nchi wanaotuhumiwa na biashara ya dawa za kulevya wakiwemo wanamichezo na wasanii mbalimbali.

Alisema ilikuthibitisha hali hiyo timu ya watendaji  imetumwa nchini Afrika kusini hivi karibu ili kukutana na kina Masogange kujua undani wa kesi yao na imethibitika kuhusika kweli na tuhuma hizo ambapo inasadikiwa jana  kesi yao imesomwa rasmi na kusubiri hatua zaidi za kisheria.
Akizungumzia  taarifa za kukamatwa kwa mwanamichezo Kaniki na Matumla Lukuvi alisema taarifa  hizo zitatolewa ufafanuzi zaidi na Serikali baada ya kupokea taarifa za kiofisi kutoka nchini  Ethiopia.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...