Wednesday, May 15, 2013

SISTER WA BANDIA, MTUMISHI WA MAHAKAMA WAKAMATWA KWA MATUKIO TOFAUTI

sister 03484
Mwanamke - anayejiita Sister Phylis Wanjiru Kamau, raia wa Kitui nchini Kenya akiwa ofisi za kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa, baada ya kukamatwa

sister 2 72758Taarifa za kipolisi, za kukamatwa kwa Sister Feki Phylis Wanjiru Kamau.
 JESHI la polisi mkoa wa Iringa limemkamata mwanamke Phylis Wanjiru mwenye umri wa miaka 44 aliyevalia mavazi ya kitawa wa masister wa kanisa Kathoriki, ambapo baada ya kupekuliwa amekutwa na baadhi ya vielelezo vilivyobaini kuwa ni tapeli.

Wanjiru ambaye ni raia wa nchi ya Kenya amekamatwa na jeshi la polisi baada ya masister wenzie kubaini kama si mmoja wao, kutokana na kushindwa kufanya baadhi ya masuala  ambayo ni msingi wa utawa wao.


Akizungumzia mkasa huo, kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda amesema mwanamke huyo kabila laKe ni Muwembu wa nchini Kenya amekamatwa katika nyumba  za masista zilizopo Ipogolo mjini Iringa.

WALIONASWA WAKIFANYA MAPENZI NA MBWA HUKO MOMBASA WAACHIWA KWA DHAMANA...!!


 

Washukiwa wa ukahaba, wasichana 11 na mzungu kutoka Uswizi, waachiliwa kwa dhamana. Awali iliripotiwa kuwa wasichana hao walibambwa wakifanya ngono na mbwa.  Ripoti mpya zinasema suala la mbwa kuhusika na si kweli, na nyumba waliyokamatwa haina hata mbwa.

ANGALIA VIDEO HAPO CHINI......

WABUNGE WA CCM WANUSURIKA "KUCHAPANA MAKONDE" BAADA YA KUZINGUANA BUNGENI...!!


WABUNGE wa CCM, jana walizua tafrani nje ya Ukumbi wa Bungebaada ya kukasirishwa na kitendo cha mwenzao wa Nkasi Kaskazini, Ali Keisy kupinga Bajeti ya Wizara ya Ujenzi wakati akichangia hotuba ya wizara hiyo.
Katika mchango wake, Keisy alisema haungi mkono hoja kwa sababu Barabara ya Sumbawanga hadi Kanazi-Mpanda mpaka Kibaoni haijajengwa kwa kiwango cha lami.

Alisema zilitengwa Sh27 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo lakini mpaka sasa Wachina waliopewa zabuni ya ujenzi huo wamekosa fedha na wameamua kuuza kokoto.
 
Mara baada ya Bunge kuahirishwa, Keisy akiwa nje ya ukumbi huo alifuatwa na Mbunge wa Urambo Mashariki, Profesa Juma Kapuya, Omary Nundu (Tanga Mjini), Mendrady Kigola (Mufindi Kusini) na Rita Kabati (Viti Maalumu) na kumzonga.
 
Baada ya wabunge hao kumzonga, Profesa Kapuya ambaye amewahi kuwa waziri serikalini alihoji kitendo cha mbunge huyo kupinga bajeti... “Kwa nini umekataa kuunga mkono hoja? Ulikuwa unalidanganya Bunge wakati unachangia si kweli huko Rukwa hakuna barabara, barabara mnazo.”

Ngassa asaini Yanga miaka 2


Mrisho Khalfan Ngassa.

Na Saleh Ally
KIUNGO mwenye kasi, Mrisho Khalfan Ngassa, amerejea Yanga na kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea tena timu hiyo.
Ngassa alianza kupata umaarufu mkubwa akiwa na Yanga kabla ya kuondoka na kujiunga na Azam FC kwa kitita cha jumla ya Sh milioni 98 na kuweka rekodi mpya ya usajili.

Lakini Ngassa ameamua kusaini tena mkataba wake mpya Yanga wakati akiwa chini ya klabu ya Simba ambao ni watani wakubwa wa Yanga.
Simba na Yanga zinakutana Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa mwisho kufunga msimu, huku Yanga wakiwa wamepania kulipa kisasi cha mabao 5-0.
Mechi hiyo ndiyo itakuwa ya mwisho kwa Ngassa ambaye mkataba wake umesainiwa bila kuwa na tarehe, Championi Jumatano limeshuhudia na lina uhakika asilimia mia.
“Mkataba na Ngassa kila kitu kimekamilika kama unavyoona, hapa tunachosubiri ni kuisha kwa msimu na mara moja atatua na kuanza kazi Jangwani,” alisema mmoja wa viongozi ambao huhusika na masuala ya usajili Yanga.

Kuziona Simba, Yanga Sh.5,000

Wachezaji wa Yanga wakijifua kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba jana kwa ajili ya mechi yao kukamilisha ratiba dhidi ya Simba.
Wakati kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga itakayochezwa Jumamosi kimetajwa kuwa ni Sh.5,000, makocha wa timu hizo walioko kambini Zanzibar wamezidi kutambiana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka nchini (TFF) jana, kiingilio hicho cha chini kitakuwa ni kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo idadi yake ni 19,648.

Taarifa hiyo ilitaja viingilio vingine kuwa Sh. 7,000 kwa upande wa viti vya rangi ya bluu, Sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, VIP C kiingilio ni Sh. 15,000, VIP B itakuwa Sh. 20,000 wakati VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja itapatikana kwa Sh. 30,000. 

"Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo huo utakaoanza saa 10 kamili jioni," ilisema taarifa hiyo na kuongeza kwamba mwamuzi wa mechi hiyo atakuwa Martin Saanya kutoka Morogoro ambapo atasaidiwa na Samuel Mpenzu wa Arusha, na Jesse Erasmo kutoka Morogoro. Mwamuzi wa akiba atakuwa Hashim Abdallah wa Dar es Salaam.

DR. SLAA AMKIMBIA NAPE NNAUYE KATIKA OFISI ZA ITV


Katika tukio lisilo la kawaida ambapo kituo cha Matangazo cha ITV kiliandaa mjadala wa kujadili hali ya kisiasa nchini na masuala mbalimbali ya kitaifa ambapo kwa busara za watendaji wa ITV waliwaalika wasemaji wakuu wa mjadala huo kuwa Viongozi waandamizi wa Vyama vya Siasa wakianza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahaman Kinana naKatibu Mkuu wa CDM Ndugu Slaa. 
Kutokana na hudhuri wa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana ambapo amesafiri kuelekea Dodoma kwenda kuhudhuria kikao cha kamati kuu jana na kubanwa na majukumu mengine muhimu ya kichama na kitaifa, alimuagiza Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, ndugu Nape Nnauye kumuwakilisha katika mjadala huo wa viongozi wa vyama vya siasa katika kujadili hali ya kisiasa na mustakabali wan chi yetu. Baada ya kufika katika Ofisi za ITV zilizopo mikocheni asubuhi ya Leo, Nape pamoja na Slaa walikutana na Nape kueleza kuwa atamuwakilisha Katibu Mkuu wake katika mazungumzo hayo ambapo baada ya kusikia kauli hiyo, Dr Slaa alianza kuhamaki na kudai kuwa hawezi kuongea na Nape kwa sababu anamtaja vibaya kwenye mikutano yake. Hata busara zilipotumika za kumsihi apungumze munkari na kumtaka kuangalia umuhimu wa mazungumzo hayo na kipindi hicho kwa watanzania, bado Slaa aligoma na kuondoka katika ofisi za ITV

Baada ya tahamaki hiyo, mijadala ya pembeni ya mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa kimsingi Slaa anamuogopa Nape katika mijadala ya kisiasa, nahii ni kutokana na uwezo wa Nape katika kujenga hoja na kuzilinda na kuzitetea hoja hizo...

Serikali yakana madai ya Lipumba, haina mpango wa kumuongezea muda Kikwete


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba(Pichani) amedai kuwa amenasa taarifa za siri za kuwapo kwa mipango ya kuongeza muda wa Serikali ya sasa kukaa madarakani, limeandika gazeti la Mwananchi
Profesa Lipumba alisema hiyo inatokana na wasiwasi kuwa mchakato wa Katiba Mpya hautaweza kukamilika mwaka 2014 hivyo kutokuwa rahisi kwa uchaguzi kufanyika mwaka 2015.
Akizungumza Dar es Salaam jana, wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la CUF, Profesa Lipumba alisema kuwa Serikali inataka kuongezewa muda wa kukaa madarakani kwa miaka miwili ikimaanisha kuwa Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete itakaa madarakani hadi mwaka 2017.

KINANA AMTAKA MBUNGE WA IRINGA AMUOMBE RADHI HADHARANI, VINGINEVYO WATAMALIZANA MAHAKAMANI.....!!!



Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Omar Kinana, kupitia kwa wanasheria wa LAW OFFICES OF ERIC S. NG'MARYO wa Moshi amemuandikia Mbunge wa Iringa Ndugu Peter Msigwa agizo la kumtaka amuombe radhi kwa matamshi ambayo kinana anadai ni ya uongo kwamba,


 HII NI SEHEMU  YA  BARUA  HIYO: 

"Nakuandikia kwa maagizo niliyopewa na mteja wangu, Ndugu Abdulrahman Kinana, kufuatia matamshi yako ya uwongo ambayo yamemkashifu, kumfedhehesha na kumshushia hadhi, Matamshi hayo uliyoyatoa mchana wa tarehe 21 April, 2013 katika mkutano wa hadhara wa kisiasa uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mbugani, Wilaya ya Nyamagana,   jijini Mwanza.


Mkutano huo ulihudhuriwa na watu wengi. Pamoja na watu hao walikuwepo pia waandishi wa habari, wakiwepo wanahabari wa magazeti, radio televisioni. Habari zenye Maneno yako ya Kashfa zimeenea nchi nzima na duniani kote kwa njia ya habari elektoniki, ikiwepo mitandao ya kijamii. 


Habari hizo zinaendelea kusomwa hadi sasa, na zitabaki kuwa kumbukumbu ya kudumu katika intaneti na kwenye hifadhi nyingine za habari"

BABY MADAHA: NAMTAFUTA MWISHO NAMIBIABABY MADAHA: NAMTAFUTA MWISHO NAMIBIA



LICHA ya Mwisho Mwampamba kuwa mume wa ndoa wa Meryl Shikwambane, msanii wa filamu na muziki Bongo, Baby Madaha amesema anajiandaa kwenda nchini Namibia wanapoishi wanandoa hao kwa lengo la kujumuika na Mwisho na kula bata.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Baby alisema bado ana uhusiano wa kimapenzi na Mwisho na kwamba yeye ndiye alimwalika aende Namibia wakafurahie penzi lao

“Nakwenda Namibia kwa Mwisho wangu. Simwogopi huyo Meryl, kwanza yeye ndiye aliyeingilia penzi langu. Mimi ndiye wa kwanza kuwa na Mwisho, hivyo ni halali yangu.

“Mwisho mwenyewe ndiye aliyeniambia niende na amesema nitafikia hotelini, nitafurahi naye kwa muda wote nitakaokuwa huko, mambo mengine mwenyewe ameshayapanga na atajua cha kufanya.”

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 15, 2013

DSC 0001 aebb0

DSC 0002 30fba
DSC 0003 9d5d6

LEMA AMKANA FROLA BAHATI ALIYEDAI KUWA AMEMBAKA..... ADAI KUWA ANATAFUTA UMAARUFU KWA NGUVU TU...!!

Bidada mmoja wa London amefanikisha nia yake ya kutaka kujulikana kwa nguvu, jana media nyingi zimeamua kumrusha sala ambayo ameisali kwa muda mrefu sana, 

"Ombi langu kwa CHADEMA na my friends mbunge Lema, please msifanye makosa ya kumjibu huyo bidada huyo, binafsi namjua sana tena kwa karibu sio mzima anahitaji kupimwa akili, alikuja hapa Dar akawa hana pa kufikia nikampa alipoondoka akaenda kunitukana kwenye blogu yake kuliko maelezo, nashangaa sana hajasema na mimi nilitaka kumbaka, mpuuuzeni huyo sio mzima anahitaji kupimwa akili!!,

Itikadi tofauti lakini siku zote ninasimamia ukweli tu!! Kama inabidi nitakuja mahakamani kutoa ushahidi wangu kwamba huyo bidada sio mzima shida yake ni umaarufu tu kwa nguvu!!, Lema na CHADEMA msimjibu in the public au media please nawaombeni sana, on this i am with you 100%, nasema tena mbele ya mungu wangu kwamba bidada huyo sio mzima anahitaji kupimwa akili! Word!”

JK KUONGEZEA MUDA WA KUKAA MADARAKANI

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba amedai kuwa amenasa taarifa za siri za kuwapo kwa mipango ya kuongeza muda wa Serikali ya sasa kukaa madarakani.



Profesa Lipumba alisema hiyo inatokana na wasiwasi kuwa mchakato wa Katiba Mpya hautaweza kukamilika mwaka 2014 hivyo kutokuwa rahisi kwa uchaguzi kufanyika mwaka 2015.


Akizungumza Dar es Salaam jana, wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la CUF, Profesa Lipumba alisema kuwa Serikali inataka kuongezewa muda wa kukaa madarakani kwa miaka miwili ikimaanisha kuwa Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete itakaa madarakani hadi mwaka 2017.


Hata hivyo, madai hayo ya Profesa Lipumba yamepingwa vikali na Serikali na viongozi wake watatu waandamizi ambapo walijibu walipoulizwa kwa maandishi na mwandishi wetu mjini Dodoma wanakohudhuria kikao cha Bunge.


Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alijibu: “Mchakato wa Katiba upo ‘on track’ (unakwenda vizuri) hatuna sababu ya kufanya hivyo.”

Tuesday, May 14, 2013

AJALI TENA WILAYANI RUGWE MKOANI MBEYA JIONI YA LEO MMOJA AHOFIWA KUFA MAJERUHI MWINGINE APELEKWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA

AJALI MBAYA IMETOKEA LEO JIONI MAENEO YA KANYEGELE KIWIRA WILAYANI RUNGWE ENEO HILO MAALUFU KWA JINA LA UWANJA WA NDEGE LORI LILILOKUWA NA SHEHENA YA CHUPA LIKITOKEA DSM KUELEKEA NCHINI MALAWI LILIKATIKA BLEKI NA KUPAA KUINGIA MSITU NDANI YA LORI HILO KULIKUWA NA DEREVA PAMOJA NA TINGO WAKE MASHUHUDA WA AJALI HIYO WAMESEMA HUWENDA MMOJA AMEFARIKI ILA MWINGINE HALI YAKE INASEMEKANA NI MBAYA 


MKUU WA WILAYA RUNGE AKISIMULIWA NA MOJA WA MASHUHUDA WA AJALI HIYO

AFANDE SELE, AKAANGUA KILIO JUKWAANI

                      MSANII mkongwe wa muziki wa bongo fleva  ambaye mpaka sasa anashikilia taji la mkali wa mashairi nchini Seleman Msindi'Afande Sele a.k.a Dume la Simba juzikati alizua taharuki kubwa kwa mashabiki waliofulika ndani ya kiwanja kipyacha Tanzanati Complex baada ya kuangua kilio jukwaani.Baada ya kuona hali hiyo waandaji wa shoo hiyo walipata jukwaani kwa kushirikiana na mabaunsa ambao kwa pamoja walimbembeleza msanii huyo bila mafaniki hali iliyosababisha baadhi ya mashabiki hasa wa kike nao kumsapoti kwa kuangua vilio vilivyovuma ukumbi mzima.

HATIMAYE BINTI ANAYEDAI KUBAKWA NA MBUNGE AMTAJA KUA NI MH LEMA, CHEKI PICHA




Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...