Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba(Pichani) amedai kuwa amenasa taarifa za siri za kuwapo kwa mipango ya kuongeza muda wa Serikali ya sasa kukaa madarakani, limeandika gazeti la Mwananchi
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alijibu” “Njooni ofisini kwangu nitasema ni kitu gani.”
Profesa Lipumba amemwomba Rais Kikwete asilikubali wazo hilo akisema wananchi hawatakubali na taifa linaweza kuingia katika mtafaruku.
“Nitapenda kuona Rais Kikwete akikataa jambo hilo kwani litachafua taswira ya nchi. Hatua hii ni kinyume cha utawala bora,” alisema Profesa Lipumba.
Alisema Serikali haipaswi kuhofia uchaguzi kwa sababu ya Katiba kwani bado uwezekano wa kuandaa uchaguzi wa haki na huru unawezekana kwa utaratibu mwingine.
“Mchakato wa Katiba unaendelea, Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatuambia kwamba mwaka 2014 tutakuwa na Katiba Mpya, sasa CUF tunasema kwamba hata kama Katiba Mpya haitapatikana kwa kipindi hicho kuwe na Tume huru ya Uchaguzi,” alisema Profesa Lipumba.
Siku nne baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoa rasimu ya mwongozo kuhusu uundwaji wa Mabaraza ya Katiba, Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), limesema litafungua kesi mahakamani kutaka kusitishwa kwa mchakato mzima wa Katiba Mpya kwa madai kuwa uendeshwaji wake umejaa mizengwe, itikadi za vyama na rushwa. Limetaja sababu tano ambazo zimekiukwa.
Limesema kesi hiyo itasimamiwa na timu ya mawakili 10 watakaoongozwa na Mwanasheria wa masuala ya Haki za Binadamu, Dk Rugemeleza Nshala na itawasilishwa mahakamani siku saba zijazo kuanzia jana.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jukata, Deus Kibamba alitaja sababu hizo kuwa ni kutokufanyiwa marekebisho katika sehemu tatu za Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kama ilivyoahidiwa na Rais Kikwete, kuvurugwa kwa Uchaguzi wa Mabaraza ya Katiba, mchakato wa Katiba kukosa uongozi, kuminywa kwa demokrasia wakati wa mchakato huo pamoja na Jukwaa hilo kuzuiwa kuonana na Rais ili kueleza upungufu uliopo.
No comments:
Post a Comment