Sunday, April 14, 2013
TAMKO LA CHADEMA KUHUSU NJAMA ZA KUKICHAFUA ZINAZOFANYWA NA GENGE LA VIONGOZI WAKUU WA CCM NA VYOMBO VYA DOLA
Ndugu waandishi wa habari;
LEO
tumewaita hapa ili kuwaomba mtufikishie ujumbe kwa Watanzania, kwamba
nikiwa mwanasheria na mtu ambaye nimepata ujuzi wa kazi za ushushu,
nimefanya uchunguzi matukio haya ya utekaji na utesaji na kugundua mambo
mengi mno.
Uchunguzi huu
nimeufanya kabla na baada ya kukamatwa kwa Mkurugenzi wetu wa Ulinzi na
Usalama, Willifred Muganyizi Lwakatare, ambaye hivi sasa anashitakiwa
mahakamani kwa tuhuma za kupanga ugaidi.
Nimefanya hivyo
kwa kuangalia maslahi mapana ya taifa langu na chama changu. Katika
uchunguzi wangu huo, nimegundua mambo mengi ikiwamo kuwapo kwa genge la
watu ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaopanga mipango
hii ya kishetani na kisha kuwasingizia watu wengine.
Angalieni mfano huu: Unaoitwa na polisi
na Mwigulu Nchemba, “mkanda wa Lwakatare” unadaiwa uliwasilishwa jeshi
la polisi Desemba mwaka jana. Lakini jeshi hilo halikumkamata yoyote
wala kumhoji, hadi pale Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom
Kibanda, alipovamiwa na kuumizwa.
Aidha, Nchemba amedai kumiliki video
ile Desemba mwaka jana, lakini rekodi hiyo iliwekwa kwenye mitandao ya
kijamii (YouTube na Jamii Forum) baada ya kutekwa kwa Kibanda. Hapa mtu
makini anaweza kujiuliza, hiki kimelenga nini?
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA Taarifa kwa Vyombo vya Habari
14
Aprili, 2013
Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha
Meja Jenerali Rashid Mnalihinga Makame (mstaafu) ambaye amefariki dunia
tarehe 14 Aprili, 2013 saa kumi na mbili na nusu asubuhi, katika
Hosptali ya TMJ.
Pamoja
na nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika Jeshini na Serikalini, Meja
Jenerali Rashid Mnalihinga Makame (mstaafu) alikuwa Mkuu wa JKT wa
tano. Kama mnavyofahamu umuhimu wa JKT, yeye ni miongoni mwa Makamanda
walioleta tija kubwa katika kuwalea Vijana wa Kitanzania na kuwajengea
nidhamu na uzalendo.
Mpango
wa Mazishi unafanywa, mtajulishwa baadae juu ya wapi na lini atazikwa
Meja Jenerali Rashidi Mnalihinga Makame (Mstaafu). Msiba upo nyumbani
kwake Mikocheni, karibu na nyumbani kwa Hayati Mwl J.K Nyerere.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI
ROHO YA MAREHEMU
Meja
Jenerali Rashidi Mnalihinga Makame (MSTAAFU) AMINA.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao
Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP
9203, Simu: 0764-742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Chadema yatishia kujitoa mchakato wa Katiba Mpya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kitajitoa
katika mchakato wa Katiba Mpya endapo mambo muhimu mawili hayatapatiwa
ufumbuzi hadi kufikia Aprili 30, mwaka huu.
Wakati Chadema wakisema hayo, Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), limesema uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba uliomalizika siku tatu zilizopita katika maeneo mbalimbali nchini haukuwa huru na ni batili, huku likipendekeza urudiwe katika maeneo yote yaliyokumbwa na kasoro.
Katika hoja zake, Chadema kimesema kinataka kufutwa kwa uteuzi/uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Wilaya ya Katiba uliofanywa na Kamati za Maendeleo za Kata na badala yake wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya wachaguliwe moja kwa moja na wananchi wa Kata husika bila kuchujwa na Kamati za Maendeleo za Kata (WDC).
Wakati Chadema wakisema hayo, Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), limesema uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba uliomalizika siku tatu zilizopita katika maeneo mbalimbali nchini haukuwa huru na ni batili, huku likipendekeza urudiwe katika maeneo yote yaliyokumbwa na kasoro.
Katika hoja zake, Chadema kimesema kinataka kufutwa kwa uteuzi/uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Wilaya ya Katiba uliofanywa na Kamati za Maendeleo za Kata na badala yake wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya wachaguliwe moja kwa moja na wananchi wa Kata husika bila kuchujwa na Kamati za Maendeleo za Kata (WDC).
Msimamo huo ulitolewa na Msemaji Mkuu wa
Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe wakati akisoma hotuba yake ya
makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2013/14 huku akiitaka
Serikali kuwasilisha muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba ili
maeneo kadhaa yafanyiwe marekebisho.
MWANAMKE ANUSURIKA KUUAWA NA PADRI AMBAYE NI MPENZI WAKE HUKO KIBAHA......!!
( picha na maktaba)
Bi Celestina
Ananius(35) amenusurika Kuuawa na Padri wa kanisa katoliki parokia ya Hombolo iliyoko Dodoma kwa jina
la Celestine John Nyaumbana ambaye kwa Sasa anaishi kwenye Makazi ya Katoliki Mbezi kwa
ajili ya Masomo.
Dada huyo
anasema amekuwa katika mapenzi na padri huyo tangia akiwa Fratel, akawa
Shemasi na sasa ni padri na suala hilo ni siri yao na wazazi wa pande
mbili hadi wamezaa mtoto anaitwa Agnes (3).
Bi Celestina ambaye anaishi Dodoma alikuja Dar kumfuata Mpenzi wake huyo ili ajue hatima ya huyo mtoto wao....
Sasa wakati wapo Dar padri huyo alimuomba mpenzi wake huyo watoke kidogo kwenda kutembea maeneo ya Kiluvya...
Walipofika huko wakati wapo katikati ya
pori padri huyo alishuka kwenye gali na kumshambulia dada huyo kwa
madhumuni ya kumuua na kupoteza ushaidi ila hakufanikiwa kumuua .....
Taarifa za Polisi Mkoa wa Pwani zinaonyesha kuwa Mwanamke huyo aliokolewa na Wasamalia wema na kukimbizwa Hospitali ya Tumbi Kibaha kwa matibabu!!!
source: Police Kibaha na Wapo radio kipindi cha Patapata
MAJID MJENGWA NAYE AKAMATWA NA POLISI AKIHUSISHWA NA SAKATA LA KIBANDA.....!!
Majid Mjengwa.
MWANDISHI wa safu katika magazeti
mbalimbali nchini, Majid Mjengwa amekamatwa na polisi kwa tuhuma za
kuhusika na tukio la kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri
Tanzania (TEF), Absalom Kibanda.
Habari zilizoufikia mtandao huu jana mchana na baadaye
kuthibitishwa na polisi zinasema Mjengwa alikamatwa muda wa asubuhi na
kwamba alikuwa akihojiwa na makachero wa jeshi hilo hadi alasiri
kuhusu tukio la kuteswa kwa Kibanda.
Msemaji Mkuu wa Polisi Advera Senso alisema kwamba:
“Ni kweli kwamba tunaye, tunaendelea kumhoji, tunachoomba ni
kwamba mtupe nafasi ili tufanye kazi yetu na kukiwa na jambo lolote
tutawajulisha.”
Saturday, April 13, 2013
ANGALIA PICHA IKIWAONYESHA ODINGA AKIWA NA KENYATTA IKULU NA WALIOKUA WAGOMBEA WENZA WAO
Picha: L-R:
Uhuru, Ruto, Raila, Kalonzo katika Ikulu ya Nairobi leo, Aprili 13, 2013
RAIS wa Kenya,
Uhuru Kenyatta na na Naibu wake William Ruto, leo wamekutana na
kushauriana na wakuu wa chama cha CORD Raila Odinga na Kalonzo Musyoka
waliowatembelea Ikulu Nairobi kuwatakia heri.
PADRI ALIYEOA KWA SIRI AFUNGWA JELA MIEZI 6 ...!!!
KUSHOTO:
Padri William akimbusu mkewe, Beverley. KULIA: Kanisa la Mt. Clara
ambamo Padri huyo alibambwa akifanya uchavu wake kwa binti wa miaka 17.
Padri mmoja wa kanisa Katoliki ambaye alifunga ndoa kwa siri amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela jana kwa kumsumbua msichana mdogo kwa kile jaji alichoelezea 'uvunjifu mkubwa wa uaminifu'.
William Finnegan, akifahamika kama 'Fadha Bill', alimpapasa binti huyo mwenye miaka 17 chini na kulazimisha kumbusu kwa nguvu katika Kanisa Katoliki la Mt Clara mjini Bradford siku ya Jumapili ya Pasaka mwaka jana.
Jaji Roger Thomas alisema kwamba Padri huyo mwenye miaka 60, alikiri wakati wa kesi hiyo kwamba alifunga ndoa kwa siri miaka 14 iliyopita.
Pia alitumia maneno makali kwa wanaparokia wa Finnegan ambao walikuwa upande wake licha ya mashitaka hayo, akisema: "Pengine baadhi yao wanaweza kuamini kesho jua litachomoza magharibi kesho kama akisema hivyo."
YUSUPH MLELA AMTUNDIKA MIMBA MWANAFUNZI NA KUMLAZIMISHA AITOE....!!
Kwa mujibu wa chanzo kimoja kilichopo chuoni hapo, Mlela alidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na denti huyo kwa muda mrefu ambapo mashosti wote wa Salha, walikuwa wakimtambua kama shemeji yao hadi alipodaiwa kumpa kibendi.
“Unajua shemeji yetu (Mlela) alikuwa anakuja sana hapa chuoni lakini baada ya kuambiwa yule Salha ana ujauzito wake, aliruka viunzi na kusema hahitaji mtoto, atoe mimba.
“Salha alipokataa ndipo Mlela alipoamua kukata mguu kabisa, tukawa hatumuoni,’’ kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa Mlela kuhusiana na ishu hiyo, alimkana mwanafunzi huyo na kusema hamtambui na wala chuo anachosoma hakijui.
“Huyo msichana simjui hata hicho chuo chenyewe cha Tandika sijawahi kufika huko, kama huyo binti ana ushahidi auweke hadharani,’’ alisema Mlela.
MWENYEKITI WA CHADEMA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA JELA KWA WIZI WA MIL. 1.2
Mwenyekiti wa chadema, mtaa wa Isamilo kaskazini B wilayani Nyamagana Philbert Bulinjiye amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kujipatia shs milioni 1,250,000 kwa njia ya udanganyifu.
Hukumu hiyo, imetolewa na hakimu Vaineth
Mahizi wa mahakama hiyo, kufuatia kesi ya jinai namba 196/2012, iliyofunguliwa
na Vedasto Mavubhi ambaye alimtuhumu mwenyekiti huyo kuchukua kwake
kiasi hicho cha fedha, kwa ajili ya kumuuzia kiwanja.
Hakimu
Mahizi katika hukumu yake, alidai ameridhika na ushahidi uliotolewa na
upnade wa mlalamikaji, mashahidi pamoja na wazee wa baraza hivyo
kumhukumu mwenyekiti kwenda jela.
Alisema
mwenyekiti huyo pamoja na Balozi Robert Byagaye wanastahili kutumikia
kifungo hicho cha mwaka mmoja jela kutokana na kutiwa hatiani.
"kitendo
kilichofanywa na viongozi hawa, kuwaibia raia wanaowaongoza kiutapeli
kwa kuwadanganya kuwauzia kiwanja na kisha kutafuta mtu bandia kwa madai
kuwa kiwanja hicho kiko katika mtaa wanaouongoza, ni udanganyifu" Alisema
hakimu na kuongeza kuwa Mwenyekiti huyo amehukumiwa kifungo hicho ili
iwe fundisho kwa viongozi wengine matapeli.
SHAA AJILINGANISHA NA AKINA DIAMONDA & OMMY DIMPOZ
MSANII
wa muziki wa kizazi kipya nchini, Sara Kaisi ‘Shaa’ amejinasibu kuwa
kiwango alichonacho sasa hakina tofauti na wasanii wengine wakali kama
Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na Nassib Abdul ‘Diamond’.
Shaa akifanya vitu vyake.
Shaa
aliyabainisha hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akifanya mahojiano
na mwandishi wa habari hii aliyekuwa akitaka kufahamu kiwango cha
fedha anachokipata katika shoo zake mbalimbali anazofanya.
“Hivi sasa kama mtu anaweza kumchukua Ommy ama
Diamond kwa dau hilo analowapa, basi anaweza pia kunichukua mimi kwa
shoo zake kwa kiwango cha nyota hao wawili, kwani uwezo ninao,”
alisema.
Aliongeza kuwa ili kudumu
katika fani ya muziki wa kizazi kipya, kunatakiwa kuongeza ubora wa
kazi kwa kufanya kazi na wadau mbalimbali wa muziki wa ndani na nje ya
nchi.
Shaa
alisema kwa sasa wimbo wake wa ‘Lover Lover’ unaendelea kufanya vema
katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini na Afrika Kusini, ambako
video ya wimbo huo inachezwa zaidi.
MBUNGE ATAKA KILIMO CHA BANGI KIHALALISHWE TANZANIA
MBUNGE wa Nkasi,Ally Kessy (CCM) ametoa mpya bungeni baada ya kuuliza
swali la kuitaka serikali ihalalishe kilimo cha bangi ili kujipatia
fedha za kigeni.
Akiuliza swali la nyongeza jana, Kessy
alisema kwa kuwa zao la tumbaku limekuwa likipigwa marufuku dunia
nzima, lakini limendelea kulimwa na kuchangia pato la mataifa
mbalimbali ikiwemo Tanzania, kwanini serikali isihalalishe kilimo cha
bangi kama ilivyo kwa tumbaku ili kuchangia pato la taifa?
Swali hilo liliibua vicheko kwa wabunge
wote, akiwemo Spika na Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula, Adam Malima.
Hata hivyo, Waziri Malima akijibu swali hilo alisema kuwa
pingamizi dhidi ya zao la tumbaku duniani limepungua na zao hilo sasa
ni moja ya mazao makubwa ya biashara.
Kuhusu bangi kuhalalishwa kuwa zao la biashara, Waziri
Malima alisema kuwa katika nchi zingine imeruhusiwa kuwa moja ya zao la
biashara na linachangia pato la taifa.
“Hapa nchini bado
bangi haijaruhusiwa kuwa zao la biashara, lakini kama utafiti
utafanyika na kubaini kama linaweza kupata soko la kuingizia pato
taifa, tutaliangalia hilo,” alisema.
Friday, April 12, 2013
MKE WA MTU ANASWA LIVE AKIFANYA MAPENZI NDANI YA GARI
KUFUATIA
vitendo vya usaliti wa ndoa, uasherati, ufuska na ukiukwaji wa maadili
ya Kitanzania kwa wanandoa, wiki iliyopita Ijumaa iliendelea na
Operesheni Fichua Maovu kwa kuzunguka jijini Dar usiku wa manane na
kunasa tukio la mke wa mtu akifanya uzinzi ndani ya gari.
Kabla ya kufanya operesheni hiyo, waandishi walitaarifiwa kwamba Wilaya ya Kinondoni jijini Dar ndiyo inayoongoza kwa wake na waume za watu kufanya vitendo vya ngono kwenye magari.
Maeneo
yaliyodaiwa kwamba wazinzi hao hupenda kuyatumia ni Coco Beach, Leaders
Club, Mlimani City na sehemu kubwa ya vitongoji vya Sinza na Mwenge,
Dar.
Subscribe to:
Posts (Atom)