Tuesday, March 20, 2018

KISA ABDUL NONDO, IGP SIRRO, DCI NA MWANASHERIA MKUU WAITWA MAHAKAMANI

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetoa wito wa kuwaita Mkrugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kufika mahakamani kesho Jumatanoo, Machi 21 kujibu kesi ya kutomfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo.

Taarifa za wito huo umetolewa na Wakili wa Mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Wakili Jebra Kambole ambaye ametoa taarifa hiyo fupi kupitia kwenye ukurasa wake maalum wa Twitter.

Kambole amesema “Wito umetolewa leo (jana Machi 19) Mahakama kuu mbele ya Jaji Samejikwamba DCI, IGP na AG wanapaswa kufika mahakamani 21/03/2018 kujibu kesi ya Abdul Nondo”.

TRUMP APENDEKEZA ADHABU YA KIFO KWA WAUZA UNGA

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa anataka kuweka adhabu kali ikiwemo adhabu ya kifo kwa wale watakaobaninika kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya. Hatua amesema ni kwa lengo la kukabiliana na ongezeko kubwa watumiaji ndani ya Marekani.
Katika hotuba yake aliyoitoa akiwa New Hampshire,wauzaji wa dawa za kulevya wamesababisha vifo vya maelfu ya watu, lakini cha ajabu baada ya kuhukumiwa kufungwa wanakaa muda mfupi tu gerezani jambo ambalo anasema haliridhishwi nalo.
Ameongeza kuwa tatizo hili linaweza kuondolewa kwa kutumia akili na kuwa imara pamoja na kutenga fedha. Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

"Mwezi oktoba tulitangaza tatizo hili kama janga la dharula kiafya ambalo limedumu kwa muda mrefu tangu kipindi kilichopita. Tumelifanyia kazi na bunge kuhakikisha tunatenga kiasi cha dola billion sita katika bajeti mpya yam waka 2018/2019 ili kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya,ambapo tutakuwa tumetenga kiasi kikubwa cha fedha kuwahi kutokea dhidi ya tatizo hili'.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MARCH 20, 2018 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

Monday, March 19, 2018

PICHA ZA RAIS MAGUFULI AKIENDESHA MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO



 Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018


 Sehemu ya Viongozi wa serikali na wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018

 Viongozi wa wa taasisi mbali mbali katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Ujumbe wa Umoja wa nchi za Ulaya (EU) katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018. Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

Sunday, March 18, 2018

RAIS MWANAMKE PEKEE AFRIKA AJIUZULU

Rais wa Mauritius, Ameenah Gurib-Fakim.

AMEENAH Gurib-Fakim rais wa Mauritius amejiuzulu urais baada ya kuelekezewa tuhuma za ufisadi kwa kutumia kadi ya malipo; awali alisema hatajiuzulu.
Baada ya kung’atuka madarakani kwa rais Sirleaf Johnson wa Liberia, huyu ndiye alikuwa mhimili wa wanawake Afrika kujishikilia kwa kusema "tuna Rais mwanamke" lakini sasa madai ya ufisadi yanaelekea kumtega.
Amehusishwa na kashfa ya kutumia kadi ya benki ambayo alikuwa amekabidhiwa na wahisani ya kufadhili ununuzi wa misaada kwa raia wake kujifaa yeye mwenyewe.
Kitita alichokigeuza kuwa chake ndani ya kadi hiyo kinasemwa kuwa makumi ya maelfu ya dola za Kimarekani.
Alijitetea kuwa hakufanya lolote baya na kwamba amerejesha pesa ambazo amedaiwa kujifaa nazo, hivyo basi kuweka swali wazi kuhusu "utarejesha nini ikiwa hukuiba".

Gurib-Fakim akiwa ni mwanasayansi tajika, alipaa hadi uongozi wa Mauritius mwaka wa 2015, ingawa ni wadhifa ambao hauna mamlaka yale ya viongozi wengine wa AfrikaTunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MARCH 18, 2018 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS



Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

Monday, March 12, 2018

CHAMA TAWALA NCHINI CHINA CHAIDHINISHA 'RAIS WA MAISHA'

Chama tawala cha National People's Congress nchini China, kimeidhinisha marekebisho ya kipengee cha katiba, ya kufutilia mbali uongozi wa mihula miwili kwa Rais wa nchi hiyo.

Hatua hiyo sasa imemfanya Rais Xi Jinping, kusalia mamlakani hata baada ya muhula wake wa pili kumalizika mnamo mwaka 2023 na kuendelea kuongoza kwa kipindi kisichojulikana.

Wakosoaji wameonya kuhusiana na hatari ya kuondoa muda wa mihula miwili ya uongozi wa Rais, ambayo ililetwa na Deng Xiaoping mwaka 1982.

Friday, March 09, 2018

TRUMP AKUBALI MUALIKO WA KUKUTANA NA RAIS WA KOREA KASKAZINI

Rais Donald Trump wa Marekani amekubali ombi la Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un la kutaka wakutane mapema ndani ya mwezi mei mwaka huu, na hivyo kuweka historia kufuatia kuwa kutokuwepo rais wa Marekani ambaye amewahi kuonana na kiongozi mkuu wa Korea kaskazini.

Hata hivyo mahala watakapokutana viongozi panasalia kuwa siri kwa sasa, na pia Marekani imesisitiza kuwa pamoja na kukubali ombi hilo la rais Kim Jong Un laini bado vikwazo vitasalia pale pale.

Tangazo hilo la kwamba rais Trump amekubali kukutana na Kim Jong Un, limetolewa na viongozi wa juu wa Korea Kusini uliofika mjini Washington kuwasilisha barua ya ombi hilo kutoka kwa Korea Kaskazini.

KENYATTA, ODINGA WAKUTANA IKULU, WAKUBALIANA JAMBO

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekutana na kiongozi wa muungano wa upinzani nchini humo Raila Odinga katika ofisi yake Jumba la Harambee, Nairobi.

Mkutano huo umefanyika muda mfupi kabla ya Bw Kenyatta kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson.

Marekani imekuwa ikihimiza kufanyika kwa mazungumzo na mashauriano kutatua mzozo wa kisiasa uliokumba taifa hilo baada ya uchaguzi uliojaa utata mwaka jana.

Thursday, February 22, 2018

MAANDAMANO YAWAPONZA CHADEMA, MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AWALIMA BARUA NZITO...!!!

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi 

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amekiandikia barua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akitaka kijieleza kwa nini asikichukulie hatua kwa kufanya maandamano Februari 16, 2018.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii leo Februari 22, 2018, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema barua hiyo ya msajili waliipokea jana na wanapaswa kuijibu kabla ya Februari 25, 2018.

Sunday, February 18, 2018

MTULIA, DR. MOLLEL WAREJEA BUNGENI UPYA

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni amemtangaza mgombea wa CCM, Mtulia Maulid kuwa Mbunge mteule wa jimbo hilo.

Mgombea huyo ameongoza kwa kura 30, 247 akifuatiwa na Mwalimu Salum wa CHADEMA kwa kura 12,353, Rajab Salum wa CUF kwa kura 1,943 na Ally Abdallah wa ADA-Tapea mwenye kura 97.
“Nashukuru waliojitokeza kufanya haki yao ya kidemokrasia, pia nawashukuru Tume ya Uchaguzi kwa umakini waliouonesha kuhakikisha tumefanya uchaguzi na kumaliza salama, kushindwa ndio kawaida ya ushindani.” Mtulia Maulid

Mkoani Kilimanjaro, NEC imemtangaza rasmi Dk Mollel kuwa mshindi wa uchaguzi katika jimbo la Siha baada ya kupata kura 25,611 huku akiwaacha mbali wapinzani wake, Elvis Mosi wa Chadema, Elvis Mosi aliyepata kura 5,905 na mgombea wa CUF, Tumsifueli Mwanri aliyepata kura 274 huku Mdoe Azaria wa Sau akiambulia kura 170.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI FEBRUARY 18, 2018 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS




Like page yetu ya facebook ya Jambo Tz tu-follow instagram @jambotz. YouTube channel @jambotz.

WAZIRI NCHEMBA AAGIZA WAKIMBIZI WA BURUNDI 32,000 KURUDISHWA KWAO

Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba amewaagiza UNHCR kuwaondoa wakimbizi 32,000 ambao wameomba kwa hiari yao kurudi katika nchi yao ya Burundi haraka tofauti na wanavyofanya sasa.

Waziri Dr Mwigulu ameyasema hayo wilayani Ngara alipotembelea kituo cha mapokezi ya wakimbizi cha Lumasi kujionea shughuli zinazoendela katika vituo vya mapokezi ya wakimbizi ambavyo serikaki ikishaagiza vifungwe mala moja.

Dr Mwigulu amesema shirika la kuhudumia wakimbizi Dunia UNHCR wao wanafanya kazi masaa 24 katika kuwapokea wakimbizi kuingia nchini lakini wanakuwa wazito pale wakimbizi wenyewe wanapotaka kwa hiari yao kurudi kwao baada ya kujiridhisha kuwa kuna amani nchini kwao.

Friday, February 16, 2018

HII HAPA LYRICS YA WIMBO MPYA WA PAPII KOCHA

Like page yetu ya facebook ya Jambo Tz tu-follow instagram @jambotz. YouTube channel @jambotz.

NIGERIA WAZINDUA NDEGE ISIYO NA RUBANI

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amezindua ndege inayojiendesha yenyewe bila ya rubani ambayo ni ya kwanza kutengenezwa nchini humo.

Kifaa hicho kilichotengenezwa na Taasisi ya Teknolojia ya jeshi la anga la Nigeria, kitatumika kupambana na wapiganaji pamoja na majambazi.

Mipango ya jeshi la nchi hiyo ni kutengeneza vifaa hivyo kwa wingi na pia uwezekano wa kuvisafirisha katika nchi nyingine.

Nigeria imekuwa ikikabiliwa na kitisho cha usalama, ikiwemo wapiganaji wa kiislamu walioko kaskazini mwa nchi hiyo, wapiganaji walioko katika eneo lenye utajiri wa mafuta, kusini mwa nchi na mapigano kati ya wafugaji na wakulima katika jimbo la kati mwa nchi hiyo

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...