Kikao cha kutathmini uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani cha Chama cha Wananchi (CUF), kimekusudia kumwandikia barua ya malalamiko Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ), Jenerali Davis Mwamunyange wakidai wanajeshi walishiriki kuleta hofu.
Hata hivyo, jeshi hilo limekana madai ya CUF likisema ni uzushi.
Madai hayo yalitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alipozungumza kwa simu na mwandishi wetu kuhusu uamuzi wa kikao hicho kilichofanyika jana Unguja chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad na kuhudhuriwa na wajumbe 14.
Alidai kikao hicho kilichojadili mwenendo mzima wa uchaguzi kuanzia kampeni, kilifikia uamuzi wa kuandika barua ya malalamiko kwa Jenerali Mwamunyange wakidai wanajeshi walionekana wakizunguka mitaani katika jimbo, siku ya kuamkia uchaguzi na siku ya kupigakura.