Tuesday, January 03, 2017
PLUIJM AKARIBIA KUPEWA MIKOBA YA UKOCHA AZAM FC
Mabingwa watetezi wa Kombe la Kagame, Azam FC wamebakiza hatua chache kukamilisha mpango wa kumkabidhi timu hiyo aliyekuwa kocha wa zamani wa Yanga, Hans Pluijm.
Habari za kuaminika kutoka vyanzo makini ndani ya Azam zilithibitisha kuwa tayari Azam imekuwa na mazungumzo ya kina na kocha huyo Mdachi ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa ufundi Yanga.
Awali, Azam ilipanga kumpa timu hiyo kocha wa Majimaji, Kally Ongala ambaye amewahi kuitumikia klabu hiyo kama kocha msadizi, lakini wakabadilisha mawazo kutokana na kocha huyo kuwa na uzoefu mdogo na michezo ya kimataifa.
Mwenyekiti wa Azam, Nassoro Idrissa ‘Father’ amesema Pluijm ni kocha wa kiwango cha juu na amethibitisha hilo nchini kwa kuipa Yanga mataji manne tofauti, hivyo watafurahi kama atafanya nao kazi. Tangaza biashara
yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow
instagram @jambotz.
Sunday, January 01, 2017
KHERI YA MWAKA MPYA 2017
Uongozi wa Jambo Tz Blog unawatakia kheri ya mwaka mpya 2017 na fanaka tele, Mwenyezi Mungu awabariki na kuwalinda siku zote. Pia tunaomba maoni na ushauri wenu ili tuweze kuboresha katika upashanaji wa habari. HAPPY NEW YEAR.
Saturday, December 31, 2016
SERIKALI NA UPINZANI WAAFIKIA MWAFAKA DRC
Wapatanishi
wanaojaribu kutatua mzozo wa kisiasa huko Jamhuri ya Kidemocrasi ya
Congo wamesema serikali ya nchi hiyo na vilevile washirika kutoka
makundi ya upinzani sasa wameafikia mwafaka.
Maaskofu kutoka
kanisa katoliki waliokuwa wakiendesha kikao hicho cha majadiliano
wanasema makubaliano ni kwamba rais Joseph Kabila anaweza kusalia
madarakani kwa mda wa mwaka mmoja, lakini ni sharti uchaguzi ufanyike
ndani ya kipindi cha miezi 12.
Sharti jingeni ni kuwa rais Kabila asiwanie tena kiti cha urais katika uchaguzi huo.
Mwafaka huo unatarajiwa kutiwa saini hii leo.
Mda
wa utawala wa rais Kabila umemalizika mwezi huu lakini kutong'atuka
kwake kumesababisha maandamano yaliyokumbwa na ghasia ambapo watu zaidi
ya 40 wamefariki.
TRUMP AMONGEZA PUTIN KWA KUTOLIPIZA KISASI
Rais mteule wa
Marekani Donald Trump amempongeza mwenzake wa Urusi Vladmir Putin kwa
kutowafukuza wanadiplomasia wa Marekani ,licha ya Marekani kufanya hivyo
kujibu madai ya kuingilia uchaguzi wa Marekani.
Bwana Trump alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter: Hatua nzuri ya kusubiri, nilijua kwamba yeye ni mwerevu sana!.
Moscow imekana madai yoyote ya kuingilia uchaguzi wa Marekani kupitia udukuzi.
Lakini
katika hatua moja ya mwisho ya uongozi wa rais Obama ,Marekani iliagiza
kuondoka kwa wanadiplomasia 35 wa Urusi kufikia siku ya Jumapili
mchana. Lakini Putin alikataa kulipiza kisasi.
Mvutano huo unafuatia madai kwamba Urusi ilidukua
kampeni ya chama cha Democrat na mgombea wake Hillary Clinton na kutoa
habari kupitia mtandao wa Wikileaks ili kumsaidia Bwana Trump kushinda
uchaguzi .
Mashirika kadhaa ya Marekani ikiwemo lile la FBI na
CIA yamesema hayo yalitendeka ,lakini Trump amekuwa akipuuzilia mbali
madai hayo akisema ni ya ''ujinga''. Hatahivyo amesema kuwa atakutana na maafisa wa ujasusi nchini Marekani ili kuelezewa hali halisi. Serikali ya Obama ilitangaza kisasi hicho siku ya Alhamisi.
Sunday, December 25, 2016
JAMBO TZ INAWATAKIA KHERI YA CHRISTMAS WATU WOTE DUNIANI
Jambo Tz inawatakia heri ya Christmas🎄 wakristu na watu wote duniani. Tusherehekee kwa amani na utulivu.
Like page yetu ya facebook/jambotz
Thursday, December 22, 2016
UWEZO WA WANAWAKE KUPATA MIMBA WASHUKA TANZANIA
Viwango vya wanawake kuweza kupata mimba nchini Tanzania vimepungua hadi 5.2 kwa kila mwanamke nchini Tanzania mwaka 2015/2016 kutoka 6.2 kwa kila mwanamke miaka ya 1991/92, kulingana na utafiti wa afya nchini humo
Kulingana na gazeti la The Citizen la nchini Tanzania, utafiti huo uliofanywa na kutolewa na Afisi ya kitaifa ya Takwimu nchini humo NBS wiki iliopita unaonyesha kushuka kwa viwango vya uwezo wa kushika mimba miongoni mwa wanawake .
Kwa mfano mwaka 1996 ripoti hiyo inaonyesha watoto 5.8, mwaka 2004/05} ni watoto 5.7 mwaka 2010 ni watoto 5.4.
WAJUMBE WAIDHINISHA USHINDI WA TRUMP
Wajumbe wa jopo la wateule wanaoamua ushindi wa rais wa Marekani, wamemwidhinisha Donald Trump kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba 8, mwaka huu.
Hatua hiyo imezima juhudi za dakika za mwisho za kutaka kumzuia Trump kuingia ikulu ya White House Januari 20.
Baada ya ushindi huo, Trump ameahidi ‘kufanya kazi kuunganisha nchi yake na kuwa rais wa Wamarekani wote’.
Hatua hiyo imezima juhudi za dakika za mwisho za kutaka kumzuia Trump kuingia ikulu ya White House Januari 20.
Baada ya ushindi huo, Trump ameahidi ‘kufanya kazi kuunganisha nchi yake na kuwa rais wa Wamarekani wote’.
RAIS WA GAMBIA ASEMA HANG'ATUKI MADARAKANI NG'OO............!!!
Rais wa Gambia Yahya Jammeh ameonya kuwa atakataa jaribio lolote la viongozi wa kieneo kumlazimisha kuondoka madarakani licha ya kushindwa katika uchaguzi na mfanyibiashara Adama Barrow.
Akihutubia wanachama wa muungano wa Bar Afrika nchini humo Bw Jammeh alisema: ''Waje wajaribu kuniondoa.wanasubiri nini? mimi ni mtu mpenda amani lakini haimaanishi kwamba sitalitetea taifa langu, kwa ujasiri na uzalendo na kuibuka mshindi''.
Amesema kuwa alikataa wito wa muungano wa viongozi wa mataifa ya Magharibi ECOWAS akiwemo rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia kuondoka nchini Gambia.
Saturday, December 10, 2016
RAIS DR. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA DANGOTE IKULU DAR ES SALAAM
Rais Magufuli alivyokutana na Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo
Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika kikao cha pamoja na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote
kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia
jambo na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara
Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kumaliza kwa kikao chao Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
mara baada ya kumaliza kikao chake na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha
Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko
Dangote akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 10 Desemba 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa
Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.
Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemhakikishia mfanyabiashara huyo
kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa
wawekezaji wote nchini katika kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya
Viwanda. Tangaza biashara yako hapa. Pia like
page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.
Friday, December 09, 2016
Tuesday, November 01, 2016
WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE KUANZA MITIHANI LEO, WAZIRI AONYA UDANGANYIFU
Wanafunzi wa kidato cha nne wakimsikiliza naibu waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo mara baada ya kukagua maandalizi ya mtihani wa kidato cha nne unaofanyika Leo.
Naibu waziri ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiagana na wanafunzi wa shule ya sekondari Msalato mara baada ya kuzungumza nao.
Naibu
waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),
Selemani Jafo, amefanya ziara kwenye shule mbalimbali mjini Dodoma
kuangalia maandalizi kwa ajili ya mtihani wa kidato cha nne unaoanza Leo
nchini.
Katika
ziara yake kwenye Shule ya sekondari Jamhuri, Kiwanja cha ndege na
Msalato, Jafo amewaonya walimu na wanafunzi hao nchini kuepukana na
vitendo vya udanganyifu.
Akizungumza
na walimu na wanafunzi katika shule hizo, Jafo amesema katika mtihani
huo hawatarajii kuwepo na udanganyifu kwa kuwa wamejifunza kupitia
mtihani wa darasa la saba ambapo kumekuwepo na tabia ya walimu kujificha
chooni ili kuwasaidia wanafunzi.
Amesema shule zitakazofanya fanya hivyo zitakuwa zimepoteza thamani yake. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow
instagram @jambotz.
Subscribe to:
Posts (Atom)