Blandina Chagula ‘Johari’
STAA wa kitambo kwenye
filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amesema baada ya kukaa singo kwa
muda mrefu, sasa yupo tayari kuingia kwenye ndoa wakati wowote.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Johari amesema anatamani sasa naye aingie kwenye ndoa
kwa kuwa umri wake unamruhusu kufanya hivyo.
“Mimi ni mwanamke kamili, ni mtu mzima. Nimeshakuwa sasa, kwahiyo kiukweli nina
kiu ya mume. Mungu akinipa mume bora, nitaolewa. Sitaki kuzungumzia sana mambo
yaliyopita, lakini muhimu kwa sasa ni mume,” anasema Johari.
Kuhusu
sifa za mwanaume anayependa awe mumewe, Johari alisema: “Napenda mwanaume
mwenye upendo wa dhati kwangu na awe mtafutaji, pia aheshimu kazi yangu.
“Historia yangu ya mapenzi imenifundisha mengi, najielewa na kujitambua vizuri.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya Johari wa zamani na wa sasa. Kwanza nimekomaa
kiakili, nimekutana na vitu vingi na nimejua maisha ni nini. Nipo tayari
kufanya maisha na mwanaume serious.”