Timu ya taifa ya Uganda
Cape Verde wametua kileleni mwa orodha ya Fifa ya uchezaji kandanda barani Afrika ya mwezi Machi. Huo ni ufanisi mkubwa kwa taifa hilo linalojumuisha visiwa kadha vidogo kaskazini magharibi mwa Afrika.
Wamefanikiwa kuwapita mabingwa wa Afrika wa mwaka 2015 Ivory Coast ambao wameshuka hadi nambari mbili. Cameroon pia wameimarika, na kuingia katika orodha ya 10 bora na kuwaondoa Guinea.
Licha
ya kushinda Kombe la Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo wameshuka nafasi moja hadi nambari 58. Miongoni
mwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Uganda inaongoza ikiwa nambari
67, ikifuatiwa na Rwanda (85), Kenya (103), Tanzania (125), Burundi
(129) na Sudan Kusini (140). Like page yetu ya facebook Jambo Tz.