Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) limesema kuwa mgao wa umeme unaoendelea nchini umesababishwa na kushuka kwa uzalishaji wa umeme katika mabwawa ya maji kwa asilimia 81.3.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema leo jijini dar es Salaam kuwa uwezo wa juu wa mitambo yote ya kuzalisha umeme wa maji ni megawati 561, lakini kwa sasa uzalishaji wote wa umeme wa maji ni megawati 105 ambazo ni sawa na asilimia 18.7.
Kuhusu umeme wa gesi, TANESCO walisema kuwa uwezo wa kuzalisha umeme kupitia Kampuni ya Pan Africa ulishuka kutoka megawati 340 hadi kufikia megawati 260. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.