Watu 14 wameuawa jana usiku katika shambulizi la bomu lililotekelezwa na Boko Haram
Watu 14 wameuawa jana usiku katika shambulizi la bomu lililofanyika kwenye jumba moja la starehe katika mji wa Maroua Kaskazini mwa Cameroon.
Siku chache baada ya kutokea kwa mashambulizi mawili ya bomu katika mji mkuu wa eneo hilo kulingana na habari kutoka kwa maafisa wa usalama.
Afisa mmoja wa jeshi lililopelekwa katika eneo hilo kupambana na Boko Haram ndiye aliyetoa habari hiyo kwa siri.
Shambulizi hilo lilifanyika saa mbili kasorobo jana usiku saa za Afrika Mashariki wakati mwanaume mmoja alirusha bomu ndani ya baa katika wilaya ya Ponre kulingana na afisa huyo wa jeshi ambaye hakutaka kutajwa.
Wakazi walijaribu kumfuata lakini aliwarushia grunedi kuwafukuza.