Friday, March 13, 2015

GAVANA ANUSURIKA KIFO KENYA

 Gavana Ali Roba wa kaunti ya Mandera
Mwanasiasa mmoja wa Kenya amenusurika shambulizi lililotekelezwa na kundi la Al shabaab.
Ali Roba ,ambaye ni gavana wa mji ulio mpakani wa Mandera alikuwa akisafiri kuelekea mjini humo wakati msafara wake ulipovamiwa.
Jaribio hilo sio la kwanza kuhusu maisha ya mwanasiasa huyo ambaye amekuwa akiongoza kampeni dhidi ya kundi hilo katika eneo hilo.
Wapiganaji hao tayari wamekiri kutekeleza shambulizi hilo na kusema wamefanikiwa kuwaua wanajeshi wanne,kuchoma magari mawili na kutoroka na jengine.
Kufikia sasa polisi wa Kenya hawajathibitisha matamshi hayo ya kundi hilo.
Al shabaab
Tukio hilo lilitokea katika barabara ambapo watu 28 waliokuwa wakisafiri katika basi walivamiwa na kuuawa miezi minne iliopita.
Barabara hiyo iko karibu na mpaka na Somali. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

ALGERIA TIMU BORA AFRIKA

Algeria imesalia katika nafasi ya kwanza katika orodha mpya ya timu bora barani Afrika
Algeria imesalia timu bora barani Afrika katika orodha ya FIFA ya mwezi March licha ya kushindwa katika kinyang'anyiro cha kombe la mataifa bingwa ya Afrika na Ivory Coast.
''The Desert Foxes'' walitupwa nje ya mashindano hayo na The Elephants ya Ivory Coast katika hatua ya robo fainali.
Hata hivyo ushindi huo wa ''The Elephants'' huko Equatorial Guinea, mabingwa hao waliwapiku kwenye orodha hiyo mpya iliyotolewa Alhamisi.
Algeria wameorodheshwa katika nafasi ya 18 duniani huku Ivory Coast ikiorodheshwa ya 20 duniani .
Black stars ya Ghana ni timu ya tatu kwa ubora barani lakini imeorodheshwa katika nafasi ya 24 duniani.
Tunisia ni ya nne barani Afrika lakini ya 25 duniani.
Senegal inafunga orodha ya tano bora barani Afrika.
Mabingwa wa kombe la mataifa ya Afrika Ivory Coast
Timu hiyo hata hivyo imeorodheshwa katika nafasi ya 36 duniani. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Kwa mara ya Kwanza wenyeji wa kombe la mataifa bingwa ya Afrika Equatorial Guinea wameondolewa katika nafasi kumi bora barani afrika licha ya kumaliza katika nafasi ya nne kwenye kipute hicho cha mwaka huu.
Orodha ya nafasi kumi bora barani Afrika.
1 (18). Algeria
2 (20). Ivory Coast
3 (24). Ghana
4 (25). Tunisia
5 (36). Senegal
6 (38). Cape Verde
7 (41). Nigeria
8 (44). Guinea
9 (47). DR Congo
10 (49). Cameroo

CHAMBERLAIN KUKAA NJE MWEZI MMOJA

 Alex Oxlade-Chamberlain hatokuwepo kwa mwezi mmoja
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger atalazimika kujikuna kichwa baada ya kupata habari kuwa kiungo chake cha kutegemewa Alex Oxlade-
Chamberlainhatakuwepo kwa takriban majuma tatu hadi nne zijazo kutokana na jeraha nyuma ya goti.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Kulingana na kocha huyo,Chamberlain alipata jeraha hilo katika mechi ya kukata na shoka ya FA dhidi ya wapinzani wao wa jadi Manchester United jumatatu iliyopita.
Kujeruhiwa kwake ni pigo kwa azimio la Arsenal kuimarisha matokeo yao katika ligi kuu ya Uingereza ambapo sasa wanashikilia nafasi ya tatu .
Alex Oxlade-Chamberlain alichangia pakubwa katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester united katika FA
Aidha Arsenal wanajiandaa kwa mechi ya marudio ya mkondo wa 16 bora katika ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya ambapo wameratibiwa kuchuana dhidi ya Monaco juma lijalo.
Winga huyo alikuwa amerejea mwishoni mwa mwezi Februari baada ya kukaa mwezi mmoja nje kufuata jeraha lengine la kiuno.
Wenger hata hivyo alipata afueni katika safu ya ulinzi baada ya kurejea kwa Gabriel aliyejeruhiwa katika mechi ngumu dhidi ya QPR mnamo Machi tarehe 4.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

FORLAN ATUNDIKA DARUGA KIMATAIFA

IMG_20150312_202943
Mshambuliaji wa zamani wa klabu za Manchester United, Atletico Madrid, Intermilan Diego Forlan jana ametangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Uruguay baada ya kuichezea timu hiyo tangu mwaka 2002.
Forlan,35, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Cerezo Osaka ya nchini Japan amekuwa msaada mkubwa kwa timu ya taifa ya Uruguay na mwaka 2010 aliiwezesha timu hiyo kushinda nafasi ya 3 kwenye michuano ya kombe la dunia iliyofanyika huko nchini Afrika kusini huku yeye akibeba tuzo ya mchezaji bora wa mashindano hayo baada kuonesha kiwango bora.
“Ninawashukuru kwa wote walionipa ushirikiano tangu naanza kuichezea timu ya taifa mwaka 2002, ninaamini timu itaendelea kufanya vizuri na nimechukua uamuzi huu ili kutoa kwa nafasi kwa wachezaji wengine ambao ninatumaini wataisadia timu hii” alisema Forlan.
Mchezaji huyo aliyepata sifa nyingi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupiga mipira ya adhabu mpaka anatangaza kustaafu tayari ameshaichezea timu ya taifa ya Uruguay michezo 112 na kufunga magoli 36. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Thursday, March 12, 2015

KONTENA LALALIA BASI, LAUA WATU 42, LAJERUHI 23

Basi la Majinja likiwa limeangukiwa na kontena na kusababisha vifo katika eneo la Changalawe mafinga.

Watu 42 wamepoteza maisha na wengine 23 kujeruhiwa baada ya lori la mizigo kugongana na basi na kontena lililokuwa limebebwa kuangukia gari hilo la abiria, katika ajali ya aina yake iliyotokea eneo la Mafinga Changalawe mkoani Iringa.
Watu 37 waliokuwa kwenye basi hilo la kampuni ya Majinjah Express lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam, walifariki papo hapo na wengine watano kufariki wakiwa Hospitali ya Mafinga. Dereva wa basi na wa lori hilo la kampuni ya Cipex, pia wamefariki.
Shuhuda mmoja wa ajali hiyo, Nyasio Pascal, aliyekuwa akiendesha basi la Saibaba, alisema aliliona lori hilo likijaribu kukwepa mashimo kwenye barabara hiyo ambayo ni nyembamba, na mara likaanza kuyumba kulia na kushoto baada ya kukanyaga shimo na ndipo lilipolifuata basi na kugongana nalo.
Alisema kontena lililokuwa limebebwa na lori hilo, liliangukia juu ya basi na kulikandamiza, jambo ambalo lilisababisha vifo vya watu wengi na pia kuzuia watu waliokuwa karibu na ajali kuokoa watu waliojeruhiwa hadi tingatinga lilipowasili. Hata hivyo, alisema mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja, alinusurika kwenye ajali hiyo bila ya kudhurika. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

NENO KUTOKA YEREMIA 32:27 LILILOPO KWENYE KAMPUNI YA MAJINJA SPECIAL

Yeremia 32 : 27
"Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza?"

ZITTO KABWE KUIBUKIA KIGOMA KESHO

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe  

Siku moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza kumvua uanachama, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kesho atatua jimboni kwake kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara.
Uamuzi wa kumfukuza Zitto (pichani) ulifikiwa juzi ikiwa ni muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi aliyofungua Januari 2, 2014, dhidi ya Bodi ya Wadhamini na katibu mkuu wa Chadema, iliyokuwa imeshikilia uanachama wake.
Mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ndiye alitangaza kutimuliwa kwa Zitto akisema ni kutokana na kufungua kesi mahakamani, kinyume na Katiba ya Chadema kipengele cha 8 (a) (x). Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO MARCHI 12, 2015


..
. 


. 
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

CHEYO AKARIBISHA 'WAGENI' KUWANIA URAIS UDP

Mwenyekiti wa UDp, John Cheyo. 

Mbunge wa Bariadi  Mashariki na Mwenyekiti wa Chama cha UDP, John Cheyo  amesema wanakaribisha wanachama wa chama chochote cha siasa nchini kuwania nafasi ya urais kupitia chama hicho.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam, kiongozi huyo alisema chama hicho bado hakijateua mgombea  urais hivyo milango iko wazi kwa wanasiasa ambao wako tayari kujiunga na chama hicho kwa lengo la kuwania urais.
“Hiki chama ni cha watanzania wote hivyo tunatoa rai kwa mtu yeyote  aliye tayari kuwa mwanachama wetu milango ya kuwania urais kupitia chama hiki ipo wazi’’ alisema Cheyo
Alisema  yeye bado hajaamua kuwania nafasi hiyo kwa sasa muda ukifika atasema lakini kwa sasa ni mapema kutoa tamko kwamba atawania wadhifa huo.
Aliongeza kwamba  anasikitishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuwahamasisha watu wasipigie kura Katiba inayopendekezwa, kwani kufanya hivyo ni sawa na kuwanyima haki wananchi.
‘’Raia wote wana haki ya kupiga kura sasa ikiwa Ukawa wanatembea kila kona ya nchi kuwahamasisha wananchi kuacha kuipigia kura katiba hiyo ni kosa,’’ alisema Cheyo
Pia Kiongozi huyo wa UDP alisema tume ya uchaguzi ndio yenye majibu ya mashine zinazotumika kuandikisha wapiga kura  kwenye daftari la kudumu, (BVR) kwamba zinafaa au hazifai.
Alisema anashangazwa sana na baadhi ya watu hususan wanasiasa na wasomi wanaojitokeza na kusema mchakato wa kuandikisha wapiga kura usimamishwe kwa sababu zao mbalimbali . Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

IS WANATUMIA GESI YA KLORINI IRAQ



Wapiganaji nchini Iraq
Shirika la Utangazaji -BBC- limepata ushahidi unaoonyesha wapiganaji wa wa Islamic State wanatumia gesi ya Klorini.
Gesi hiyo huwekwa kwenye silaha za kemikali katika vita nchini Iraq.
Serikali ya Iraq imesema kiasi kidogo cha kemikali kimekuwa kikitumika katika mabomu yanayolenga majeshi yake ambayo yamekuwa yakiwaondoa wapiganaji Islamic State katika mji wa Tikrit.
Katika picha video ambayo BBC imeoneshwa na kikosi cha kuharibu mabomu nchini Iraq imeonekana mlipuko wa bomu ukiwa na moshi wa rangi ya chungwa ukipaa angani.
Bomu hilo lilikuwa na kiasi kidogo cha Klorini ambayo huenda hutumika kama sumu kwenye maeneo ya wazi.
Kumekuwa na taarifa za wapigani wa Islamic State kutumia gesi ya klorini tangu walipoanza harakati zao. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

UMOJA WA MATAIFA WALAUMIWA KUHUSU SYRIA

Hali ya uharibifu nchini Syria
Ripoti ya mashirika zaidi ya ishirini ya misaada ya kibinadamu na yale ya kutetea haki za binaadamu yamelishutumu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kutetea raia walio katikati ya vita nchini Syria.
Ripoti hiyo imezishutumu nchi zenye nguvu kubwa ya ushawishi duniani kwa kushindwa kutumia nguvu zao kuandaa maazimio ya kusaidia uhuru wa huduma za misaada ya kibinadamu kwa waathirika.
Ripoti ya masharika hayo ni ya kuadhimisha miaka minne ya vita nchini Syria ambavyo vinaendelea hadi hivi sasa.
David Milband ambaye ni Rais wa Shirika la kimataifa la Uokoaji International Rescue Committee amesema kuna ongezeko dogo la misaada inayotolewa kuwasaidia raia wa Syria. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

BAYERN MUNICH, PSG ROBO FAINALI UEFA

Bayern Munich siku walipopambana na AC Roma
Timu ya Bayern Munich ya Ujerumani na Paris St. Germain ya Ufaransa zimesonga mbele katika hatua ya robo fainali ya Michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya kufuatia matokeo waliyayapata usiku wa kuamkia leo.
Wakicheza kwa kujiamini Bayern Munich ilidhihirisha kuwa ni moto wa kuotea mbali katika mashandano hayo baada ya baada ya kuwapa kichapo cha mbwa mwizi wapinzani wao Shakhtar Donetsk ya Ukrine cha magoli 7- kwa mtungi.
Magoli ya Bayern Munich yalitiwa kimiani na Thomas Muller, Jerome Boateng ,Franck Ribery,Holger Bastuber, Robert Lewandowski na Mario Gotze.
Nayo Paris St. Germain ya Ufaransa imesonga mbele hatua ya robo fainali baada ya kuwaondoa Chelsea katika mashindano hayo japo timu hizo zilitoka sare ya magoli mawili kwa miwili lakini magoli ya ugenini iliyoyafunga hapo jana ndio yaliyowanufaisha Paris St. Germain.
Hivyo mshindi katika mechi hiyo ilibidi kupatikana katika dakika thelathini za nyongeza baada ya dakika tisini za kawaida kumalizika huku timu zote zikiwa zimefungana goli moja kwa moja.
Wakiwa na matumaini ya kuingia robo fainali Chelsea ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli kupitia Gary Cahill katika 81 lakini Mlinzi wa zamani wa Chelsea David Luiz akafutilia ndoto hizo mbali baada ya kusawazisha goli hilo katika dakika ya 86.
Na hivyo hadi dakika 90 za kwanza zinamalizika Chelsea 1 na Paris St. Germain 1 na hivyo kulazimika kucheza dakika 30 nyingine ili kumpata mshindi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

CHELSEA WAONDOLEWA UEFA WAKIWAA KWAO...!!!

zlatan 1
Vinara wa ligi kuu ya England, Chelsea leo usiku wamejikuta wakiambulia majonzi baada ya kutolewa katika michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya na Wapinzani PSG huku wakiwa mbele ya mashabiki wao kunano Uwanja wa Stamford Bridge  baada ya kulazimishwa sare ya 2-2.
Licha ya PSG kucheza wakiwa pungufu kwa kipindi kirefu kufatia Nyota wake Zlatan Ibrahimovic kupewa kandi nyekundi ya moja kwa moja baada ya kumfanyia madhambi Oscar katika dakika ya 32 kipindi cha kwanza, hawakuweza kuvunjika Moyo zaidi waliongeza nguvu na kusaka ushindi hatimaye sasa Wametinga hatua ya Robo fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Ulaya kwa ngazi ya Vilabu.hazard  2
Chelsea ndio walianza kupata bao kupitia kwa Gary Cahill kunako dakika ya 80 kipindi cha pili kufatia kona iliyopigwa na mabeki wa PSG wakashindwa kuosha mbele ndipo mchezaji huyo akafumua shuti ambalo lilitinga kambani, Bila kukata tamaa Wafaransa hao (PSG) walikomaa na kujipatia bao la kusawazisha katika dakika ya 85 kupitia kwa David Luiz, ambapo hadi dakika 90 zinamalizika Chelsea ilikuwa imebanwa mbavu na PSG kwa kukubali sare ya 1-1.
Kama kawaida ziliongezwa dakika 30 ili kupatikana mbabe wa mchezo, Thiago Silva beki wa PSG  akanawa mpira katika eneo la 18 na muamuzi akawazawadia Chelsea Penati ambayo ilipigwa na Eden Hazard na kuipatia timu yake bao la 2 ikiwa ni dakia ya 95. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Wednesday, March 11, 2015

TAZAMA PICHA ZAIDI ZA AJALI YA BASI LA MAJINJAH LILILOANGUKIWA NA KONTENA ENEO LA CHANGALAWE MAFINGA MKOANI IRINGA...!!!




 Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

HII NDIO ORODHA YA ABIRIA WALIOANZIA SAFARI STENDI KUU MBEYA, NANE NANE, UYOLE NA CHIMALA NA BASI LA MAJINJAH SPECIAL


Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.


Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...