Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za mitaa (LAAC) za
Mitaa, Kangi Lugola akizungumza wakati wa kikao cha kamati hiyo
kilichofanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mjumbe mwenzake, Omari
Nundu.
Licha ya Bunge
kuazimia kuwa wenyeviti wa kamati zake waliotajwa kuhusika kwenye kashfa
ya Akaunti ya Tegeta Escrow wavuliwe nyadhifa zao, hali imekuwa tofauti
katika vikao vya kamati hizo vilivyoanza jana baada ya baadhi yao
kuongoza vikao hivyo. Jana, Kamati Kuu ya CCM imeamua viongozi hao,
Andrew Chenge, William Ngeleja Na Profesa Anna Tibaijuka wafikishwe
Kamati ya Maadili ya chama.
Awali, walitakiwa kuachia ngazi na kamati zao
katika mabano ni Ngeleja (Katiba, Sheria na Utawala), Chenge (Bajeti) na
Victor Mwambalaswa (Nishati na Madini).
Kikao cha 16 na 17 cha Bunge kiliazimia kuwa
kamati husika za kudumu za Bunge zichukue hatua za haraka na kwa
vyovyote vile kabla ya Mkutano wa 18 wa Bunge unaoanza Januari 27,
kuwavua nyadhifa zao wenyeviti tajwa wa kamati husika.
Hata hivyo, jana, Ngeleja alisema anaendelea na madaraka yake, kwa kuwa hatua iliyopo sasa ni ya uchunguzi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.