Wednesday, January 07, 2015
ZIARA YA MH. RIDHWANI KIKWETE JIMBONI KWAKE CHALINZE
Ridhiwani
akihutubia wananchi katika Kitongoji cha Chalinze Mzee wakati wa ziara
ya kuwashukuru wananchi na kusikiliza kero zao pamoja na kuwashuru kwa
kumchagua, pia alisema atatumia unasheria wake kuwasaidia baadhi ya
wakazi wa jimbo hilo wanaonyimwa haki zao za msingi ikiwemo kuporwa
ardhi.
Mkazi
wa Chalinze, Bibi akitoa malalamiko yake mbele ya Mbunge Ridhiwani
Kikwete ya kudhulumiwa shamba lake na watu wasiojulikana.
Mkazi
wa Chalinze Methodius Kaijage, akiuliza swali kuhusu alama za x
zilizowekwa kwenye nyumba zao kwa ajili ya upanuzi wa barabara ambazo
alidai ni takribani miaka kumi imepita bila kupewa fidia hivyo
kusababisha kukosa maendeleo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
UTATA WAJITOKEZA KIFO CHA MESHACK YEBEI
hali
tata imezidi kujitokeza juu ya kifo cha Meshack Yebei, anayetajwa kuwa
shahidi katika kesi inayomkabili Naibu Rais wa Kenya William Ruto.
Shahidi huyo alitarajiwa kutoa ushahidi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC dhidi ya naibu Rais wa Kenya.Lakini mwishoni mwa wiki mwili wa Yebei ambao ulionekana kuunguzwa kiasi ,ulikutwa umetupwa kando ya mto huko Eldoret Magharibi mwa nchi hiyo.
Familia ya Yebei wanashuku kwamba chanzo cha mauaji hayo ilikuwa ni kumzuia ndugu yao asiweze kutoa ushahidi wake katika mahakama ya ICC huko The Hague. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
SHELL YAKUBALI KULIPA FIDIA NIGERIA
Kampuni kubwa ya mafuta ya Shell imekubali kulipa dola milioni 80 kama fidia.
Kampuni hiyo ya Uholanzi imewapa fidia wakazi wa jamii ya Bodo katika eneo la Niger Delta walioathiriwa na uvujaji wa mafuta.Mawakili wa wavuvi 15,600 wa Nigeria wamesema wateja wao watapokea dola za Kimarekani 3,300 kila mmoja kutokana na hasara iliyosababishwa na uvujaji wa mafuta hayo.
"Kiasi kilichobaki cha dola milioni 30 zitatumika kwa ajili ya shughuli za jamii ya Bodo ambayo iliathirika vibaya kutokana na matukio mawili ya kuvuja mafuta mwaka 2008 na 2009".
Mawakili hao wamesema mafuta hayo yaliharibu maelfu ya hekta za mikoko kusini mwa Nigeria.
Fidia hiyo imesemekana kuwa kuwa kubwa kuwahi kuliko zote zilizowahi kulipwa nchini Nigeria, na hivyo kumaliza mvutano wa kisheria uliodumu kwa miaka mitatu. Wanaharakati wanasema kampuni ya Shell ililazimika kukiri kosa hilo mapema zaidi.
Matukio yote mawili ya kuvuja kwa mafuta yametokea katika bomba hilo hilo la Trans Niger Pipeline, linaloendeshwa na kampuni ya Shell, ambalo linachukua mafuta kutoka visima vyake(Shell) kwenda kituo cha mwisho cha kusafirisha mafuta hayo nje kilichopo pwani ya Bonny. Bomba hilo linasafirisha mapipa 180,000 ya mafuta kwa siku. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
KASEJA, YANGA GIZA NENE
IPO misemo mingi ambayo huashiria
kutokea kwa jambo liwe nzuri au baya, moja ya misemo hiyo ni ule usemao
dalili ya mvua ni mawingu.
Msemo huu unaweza ukawa na na
maana kubwa hivi sasa kwa golikipa wa timu ya Dar es salaam Young
African, Juma Kaseja ambaye hivi sasa inaonekana hana mawasiliano mazuri
na uongozi wa timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani
jijini Dar es salaam.
Mchezaji huyo mwenye heshima
kubwa nchini mwishoni mwa mwaka uliopita aliachwa katika kikosi cha timu
hiyo kilichoelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya mapinduzi,
lakini isitoshe jina la Kaseja halijaonekana kwenye orodha ya wachezaji
wa timu hiyo iliyotumwa shirikisho la soka barani Afrika CAF kwa ajili
ya ushiriki wa kombe la shirikisho.
Matukio hayo yote yameibua
maswali mengi kwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo juu ya hatma ya
mlinda mlango huyo, hatua iliyotufanya tumtafute afisa habari na
mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro kutaka kufahamu kinaga ubaga
kinachoendelea kati ya Kaseja na Yanga..
Muro amesema Kaseja kutohusishwa katika kikosi kilichopo Zanzibar na kilichotumwa CAF ni kujitakia mwenyewe.
Jerry Muro.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
SIMBA KUWASHA CHECHE ZANZIBAR LEO
ROBO fainali ya kwanza ya kombe
la Mapinduzi inapigwa leo majira ya saa 2:15 usiku uwanja wa Amaan
Zanzibar baina ya Simba na Taifa ya Jang’ombe.
Mechi hii imetabiriwa kuwa tamu
kutokana na kiwango kikubwa walichoonesha Simba katika mechi ya mwisho
ya makundi dhidi ya JKU ambapo walishinda goli 1-0.
Siku hiyo Simba waliuanza mchezo
kwa kasi katika vipindi vyote, wakicheza pasi za haraka haraka na
kutumia njia ya pembeni kuipenya ngome ya JKU.
Kocha Goran Kopunovic alitumia
muda mwingi kuwaelekeza wachezaji wake namna ya kucheza mpira ambapo
alisisitiza kwa ishara akiwataka wachezaji wapigiane pasi na kushambulia
kupitia mawinga na kukaba kwa uangalifu.
Kocha huyo ameonekana kupenda
kucheza mpira wa kasi muda wote na amekuwa akiwapa wachezaji wake
mazoezi magumu ya kuongeza nguvu na pumzi.
Robo fainali nyingine tatu
zitapigwa kesho uwanja wa Amaan ambapo majira ya saa 9:00 alasiri,
mabingwa watetezi, KCC ya Uganda watachuana na Polisi Zanzibar.
Azam fc watashuka dimbani katika robo fainali ya tatu majira ya saa 11:00 jioni kuonesha kazi na Mtibwa Sugar.
Hii itakuwa mechi kali kutokana
na ubora wa timu zote hususani Mtibwa Sugar wanaoongoza katika msimamo
wa ligi kuu Tanzania bara.
Robo fainali ya mwisho itawakutanisha Yanga na JKU majira ya saa 2:00 usiku. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
"KIWANGO CHA NGASSA KIMESHUKA, LAKINI NI MCHEZAJI MWENYE AKILI, LAZIMA ATARUDI KATIKA KIWANGO CHAKE" - PLUIJM
KOCHA mkuu wa Yanga SC, Mholanzi, Johannes Hans van der Pluijm anaamini Mrisho Ngassa atarudi katika kiwango chake cha zamani.
Pluijm alikiri wazi kuwa nyota
huyo ameshuka kiwango kwa sasa na ndio maana anaanzia benchi katika
mechi mbalimbali, lakini anaonesha juhudi kubwa mazoezini kitendo
kinachoonesha wazi ametambua alipo sasa.
“Kiwango cha Ngassa kimeshuka, lakini ni mchezaji mwenye akili, lazima atarudi katika kiwango chake”. Alisema Pluijm.
Kocha huyo anayependa soka la
kushambulia aliongeza kuwa kwasasa kikosi chake kimesheheni nyota wa
kiwango cha juu, hivyo inawalazimu wachezaji kufanya jitihada za
kumshawishi.
Moja kati ya mechi kubwa ambayo
Ngassa hakuanza chini ya Pluijm mwishoni mwa mwaka jana ni ile ya ligi
kuu soka Tanzania bara dhidi ya Azam fc iliyopigwa desemba 28 mwaka jana
uwanja wa Taifa ambapo timu hizo zilitoka sare ya 2-2.
Katika mechi hiyo, Ngassa
alichezeshwa dakika 7 tu kitendo kilishoashiria mchezaji huyo kipenzi
kwa Wana Yanga si mchezaji tegemeo tena katika kikosi cha Yanga. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
DROO YA KUPANGA MECHI KOMBE LA FA YAFANYIKA
Droo ya kupanga mechi za raundi ya 4 ya Kombe la FA imefanyika.
Katika mpangilio huo, vigogo Manchester United imepangwa kucheza na timu ya daraja la chini ya Cambridge United.Mabingwa Watetezi, Arsenal, watakuwa Ugenini kucheza na Brighton au Hove Albion ambayo ipo Daraja la chini ya Ligi Kuu England.
Chelsea itakipiga na Mill wall au Bradford City. Manchester City itapepetana na Middlesbrough
Southampton/Ipswich na Crystal Palace
Blackburn Rovers na Swansea City
Michezo ya raundi ya nne inatarajiwa kupigwa Januari 24 na 25.
NAKO kwenye kombe la mapinduzi
Baada ya kutojulikana kuwa nani atacheza na Simba katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Mapinduzi, sasa kila kitu kiko wazi. Simba itaivaa Taifa Jang'ombe katika mechi ya michuano hiyo hatua ya robo fainali hii leo usiku.
Mechi hiyo itachezwa saa 2 usiku kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Siku inayofuata Alhamisi, mechi nyingine ya robo fainali itapigwa jioni, nayo ni kati ya Azam dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mechi hiyo inaaminika kuwa moja ya zile ngumu na safi za michuano ya Mapinduzi.
Yanga sasa itacheza mechi yake ya robo fainali dhidi ya maafande wa JKU.
Mechi hiyo itapigwa Alhamisi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Yanga inakutana na JKU baada ya kumaliza vinara wa kundi A wakiwa na pointi 9. Walipata pointi hizo baada ya kushinda mechi zote tatu katika makundi kwa kujikusanyia mabao tisa, wakiwa hawajafungwa hata moja.
Walikamilisha pointi hizo tisa baada ya kuifunga Shaba kwa bao 1-0 katika mechi tamu na ya kuvutia jana usiku.
Bao la mchezo huo lilifungwa na Mbrazil Andrey Coutinho. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
MATOKEO YA MECHI ZA JANA KOMBE LA FA ENGLAND HAYA HAPA… EVERTON YATOKA SARE
Tuesday, January 06, 2015
PROFESA SOSPETER MUHONGO AFANYA ZIARA SIMIYU KUKAGUA MIRADI YA UMEME
Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo kwa mtaalamu kutoka
kampuni ya Symbion iliyopewa kazi ya kujenga miundombinu ya umeme katika kijiji cha Nyamikoma kilichopo
wilayani Busega Bw. Steve Thomson
(kushoto)
Meneja wa Tanesco- Kanda
ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma, akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo na wananchi wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Busega
(hawapo pichani)
Mkazi wa kata ya
Ijitu iliyopo wilayani Busega
ambaye jina lake halikupatikana mara moja akitoa hoja yake
mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka
kushoto waliosimama mbele) mara Waziri
alipofanya ziara katika kijiji hicho na kusikiliza kero za wananchi
Diwani wa Kata ya
Ijitu iliyopo wilayani Busega Vumi Magoti akielezea kero za umeme katika kata yake mbele
ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka
kushoto), viongozi na wananchi (hawapo
pichani).
Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya
Ziwa na Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Profesa Muhongo
anafanya ziara katika mikoa ya Simiyu,
Tabora na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Taneesco. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
URUSI KURUHUSU ASKALI KUTOKA NJE
Urusi imeanza kuruhusu askari kutoka nje wenye utalaam ili kuingia katika jeshi lake.
Hata hivyo, wataalam wa Urusi wanasema hatua hiyo haina uhusiano wowote na mgogoro nchini Ukraine.Rais Vladimir Putin ameidhinisha sheria inayowawezesha raia wa kigeni kufanyakazi angalau kwa miaka mitano katika jeshi la Urusi ili mradi wanajua kuzungumza Kirusi.
Wataalam hao wanatarajiwa zaidi watatoka katika jamhuri za Asia ambazo awali zilikuwa sehemu ya muungano wa nchi za Soviet.
Wageni wa kujitolea, wakiwemo Warusi wamekuwa wakipigana nchini Ukraine. Hata hivyo Urusi imekuwa ikikana kupeleka majeshi yake huko.
Serikali ya Ukraine na nchi za magharibi wanasema Urusi imetuma silaha nzito na askari wenye utaalam wa hali ya juu kuwasaidia watu wanaotaka kujitenga mashariki mwa Ukraine. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
YANGA KUENDELEZA DOZI KOMBE LA MAPINDUZI...?!
HATUA ya makundi ya kombe la
Mapinduzi inatarajia kumalizika leo kwa mechi nne kupigwa viwanja viwili
tofauti hapa visiwani Zanzibar.
Mapema majira ya saa 9:00 alasiri
katika uwanja wa Amaan, Mabingwa watetezi wa kombe hilo, KCC ya Uganda
watachuana vikali na mabingwa wa Zanzibar, KMKM katika mchezo wa mwisho
wa kundi B.
Mabingwa watetezi wa Tanzania bara, Azam fc watahitimisha mechi ya kundi B kwa kuchuana na Mtende, uwanja wa Amaan.
Katika dimba la Mao Dze Tung, Taifa ya Jang’ombe itakuwa kibaruani kuhitimisha mechi ya kundi A dhidi ya Polisi.
Yanga wao watacheza mechi ya mwisho ya makundi kwa kukabiliana na Shaba majira ya saa 2:15 usiku.
Yanga wanaingia katika mechi hii
wakiwa tayari wameshafuzu hatua ya robo fainali kwani mechi mbili za
kwanza dhidi ya Taifa ya Jang’ombe na Polisi, zote walishinda mabao 4-0. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
SIGARA YAMPONZA KIPA ARSENAL
Mzee wa fegi, Wojciech Szczesny
GOLIKIPA wa Arsenal, Wojciech Szczesny ametozwa faini ya paundi laki mbili kwa kosa la kuvuta sigara bafuni baada ya mechi.
Bosi
wa kipa huyo mwenye miaka 24, Arsene Wenger aligeuka ‘mbogo’ alipomkuta
akipiga fegi baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Southampton siku ya
mwaka mpya.
Szczesny
alilazimika kuomba msamaha kwa tabia hiyo, lakini haijulikani kama
ataondolewa katika kikosi cha wiki hii kitakachoikabili Stoke kwenye
mechi ya ligi kuu England. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
STEVEN GERRARD AIBEBA LIVERPOOL FA
Steven Gerrard ameonyesha ubora na uongozi na Liverpool itamkosa mchezaji wa aina hii wakati atakapohama Anfield.
Ni
Gerrard aliyewainua mara mbili vitini mashabiki wa Liverpool
ilipoizamisha AFC Wimbledon mabao 2-1 katika michezo inayoendelea ya
Kombe la FA.Gerrard, akicheza mchezo wake wa kwanza tangu atangaze kuihama Liverpool katika msimu ujao na kwenda kukipiga Marekani, alionyesha pengo atakaloliacha atakapoihama timu yake aliyokulia na kupata mafanikio makubwa.
Nahodha huyo wa Liverpool ambaye atasherehekea miaka 35 katika siku ya mwisho ya Kombe la FA, tarehe 30 mwezi Mei aliiongoza timu hiyo kupata mafanikio na amefanya hivyo mara nyingi wakati timu ilipojikuta katika matatizo.
Gerrard alianza kuichezea Liverpool mwaka 1998. Gerrard amefunga magoli 182 katika michezo 696 aliyoichezea timu ya Liverpool.
Na katika mchezo mwingine Tottenham walitoka sare na Burnley kwa kufungana goli 1-1. Burnley ndio waliokuwa wenyeji wa mchezo huo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Subscribe to:
Posts (Atom)