KOCHA mkuu wa Yanga SC, Mholanzi, Johannes Hans van der Pluijm anaamini Mrisho Ngassa atarudi katika kiwango chake cha zamani.
Pluijm alikiri wazi kuwa nyota
huyo ameshuka kiwango kwa sasa na ndio maana anaanzia benchi katika
mechi mbalimbali, lakini anaonesha juhudi kubwa mazoezini kitendo
kinachoonesha wazi ametambua alipo sasa.
“Kiwango cha Ngassa kimeshuka, lakini ni mchezaji mwenye akili, lazima atarudi katika kiwango chake”. Alisema Pluijm.
Kocha huyo anayependa soka la
kushambulia aliongeza kuwa kwasasa kikosi chake kimesheheni nyota wa
kiwango cha juu, hivyo inawalazimu wachezaji kufanya jitihada za
kumshawishi.
Moja kati ya mechi kubwa ambayo
Ngassa hakuanza chini ya Pluijm mwishoni mwa mwaka jana ni ile ya ligi
kuu soka Tanzania bara dhidi ya Azam fc iliyopigwa desemba 28 mwaka jana
uwanja wa Taifa ambapo timu hizo zilitoka sare ya 2-2.
Katika mechi hiyo, Ngassa
alichezeshwa dakika 7 tu kitendo kilishoashiria mchezaji huyo kipenzi
kwa Wana Yanga si mchezaji tegemeo tena katika kikosi cha Yanga. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.