Papa
Francis ametumia sherehe za kuupokea mwaka wa 2015 kuzungumzia tatizo
la rushwa katika mji wa nyumbani wa Rome nchini Italia.
Akizungumza
katika Kanisa kuu la St. Peter Basilica, papa amesema rushwa ni
shumbulizi dhidi ya maskini na wasiokuwa na uwezo ambapo ametaka
mabadiliko ya kiroho na kimaadili katika mji huo.Papa ambaye ndiye Askofu wa Rome amefanya utetezi dhidi ya maskini kama nguzo muhimu katika uongozi wake wa upapa.
Maafisa wa polisi kwa sasa wanawachunguza maafisa wa Roma wanaotuhumiwa kujihusisha na kundi la Mafia na ufisadi dhidi ya fedha za umma zikiwemo zilizotengwa kwa ajili ya kituo wahamiaji. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.