Polisi mkoani Iringa wanawashikilia watu
watatu wakiwamo madereva wawili wa Kampuni ya Mwananchi Communications
Limited (MCL) kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi
alisema tukio hilo lilitokea jana saa 11 alfajiri katika kituo cha
ukaguzi cha Igumbilo mkoani hapa nabaada ya ukaguzi polisi walibaini
magunia mawili ya mirungi ndani ya gari la kusafirishia magazeti ya
kampuni hiyo.
Mungi alisema mirungi hiyo ilipakiwakatika eneo la
Chalinze mkoani Pwani na taarifa za awali zinaeleza kuwa ilikuwa
ikisafirishwa kwenda Zambia. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz