Ripoti kutoka kaskazini mwa Nigeria zinasema kuwa watu kadhaa wameuawa
na mlipuko wa bomu karibu na mashine ya kutoa pesa ya ATM.
Walioshuhdia
walisema kuwa ,mwanamume mmoja alikaribia watu waliokuwa wamepanga
foleni kwenye mashine hiyo kwenye mji wa Azare ulio katika jimbo la
Bauchi .Walisema kuwa mwanamme huyo alikuwa amebeba bahasha ambayo baadaye ililipuka.
Siku ya Jumatano watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la Boko Haram walivamia kiwanda kimoja cha saruji ambapo walichukua baruti wanayotumia kwenye milipuko. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz