Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Pandu Amir Kificho (kulia) akiwaeleza
jambo wajumbe wa bunge hilo walipohudhuria kikao cha 32 cha Bunge mjini
Dodoma jana.
Pendekezo la Rasimu ya
Katiba kuwa wabunge walau wawe na elimu ya kidato cha nne limetupiliwa
mbali na wajumbe wa Bunge Maalumu, baada ya Kamati karibu zote
kulikataa.
Kamati hizo zimependekeza kigezo cha elimu kuanzia
walau kidato cha nne kama sharti muhimu la mtu anayetaka kugombea
Ubunge kiondolewe, badala yake mgombea ama ajue tu kusoma na kuandika,
au ajue kusoma na kuandika Lugha ya Kiswahili au Kiingereza kama ilivyo
kwenye Katiba ya sasa.Mbali na pendekezo hilo, kamati hizo zimegawanyika
kuhusu Ibara ya 129 ya Rasimu ya Katiba inayowapa wananchi nguvu ya
kumuondoa mbunge wao madarakani kabla ya miaka mitano kumalizika.
Hayo yalijitokeza bungeni Dodoma jana, wakati
kamati hizo zikiwasilisha taarifa zake kuhusu Sura ya 9 na 10 ya Rasimu
ya Katiba iliyowasilishwa bungeni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz