Tuesday, July 29, 2014

DR. BIRALI AWAONGOZA WATANZANIA SWALA YA IDD

20140729_074656_73ac8.jpg
20140729_074807_771af.jpg
Makamo wa rais Dr. Birali amewaongoza wananchi wa Jiji la Dar es salaam katika swala ya Idd iliyoswaliwa kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja leo asubuhi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na Mjengwa Blog

ISRAEL: TUTAJILINDA NA HAMAS

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Israel inatakiwa kujiandaa kwa ajili ya mpango wa muda mrefu katika Gaza.
Hata hivyo ameelezea msimamo wake dhidi ya kundi la wapiganaji wa Hamas. Netanyahu amesema Hamas wanapaswa kusambaratishwa na hilo ndilo lengo la Israel.
‘Tulijua kuwa tungekuwa na siku ngumu, hii ni siku ngumu na ya maumivu kutokana na mashambulizi haya, nguvu na malengo vinatakiwa ili kuendeleza mapambano dhidi ya kundi hilo, anasisitiza Netanyahu.
Wizara ya afya ya Gaza imesema kuwa raia 10 wa palestina wameuawa katika shambulio la makombora yaliyolenga uwanja wa mpira yakitekelezwa na Israel..

Kati ya waliouawa katika shambulio hilo ni watoto saba waliokuwa wakicheza uwanjani hapo ambapo walipigwa na kufa papo hapo.
Hamas imeilaumu Israel kwa shambulio hilo,huku msemaji wa Israel akidai kuwa shambulio hilo lilitekelezwa kwa bahati mbaya.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Monday, July 28, 2014

KATIBA MPYA: WASSIRA, LIPUMBA, LISSU 'WANYUKANA'


http://jambotz8.blogspot.com/
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uratibu na Uhusiano), Stephen Wassira akizungumza kwenye mdahalo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema) Tundu Lissu na katikati ni Mwenyekiti wa CUF,  Profesa Ibrahim Lipumba.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wassira akiwakilisha CCM, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, jana walitoana jasho katika mdahalo wa Katiba ulioandaliwa na East African Business and Media Institute.
Mdahalo huo uliohudhuriwa na watazamaji wapatao 500, ulikuwa na mada inayosema: ‘Nani anakwamisha Upatikanaji wa Katiba Mpya.’ Kila upande ulitumia fursa hiyo kutupa shutuma kwa mwingine huku jazba na kelele vikitawala miongoni mwa waliohudhuria.
Hata hivyo, suala la muundano wa serikali ndiyo uliochukua nafasi kubwa katika mdahalo huo huku Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ukiishutumu Serikali ya CCM kuwa ndiyo kikwazo cha upatikanaji wa Katiba Mpya nayo ikitupa mpira huo kwa Ukawa kwa kitendo chake cha kutoka katika Bunge Maalumu la Katiba. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 28, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC01214
DSC01216
DSC01217 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

PAPA AOMBA VITA VIMALIZWE

Pope Francis
Papa Francis ameomba amani kwa dhati katika hotuba ya kila juma katika medani ya St Peter's mjini Rome.
Aliacha kusoma hotuba aliyoandika kuomba vita vimalizwe na hisia ikisikika kwenye sauti:
"makaka na madada, hapana vita, hapana vita, nawafikiria hasa watoto ambao wananyimwa matumaini ya maisha ya maana, ya siku za mbele, watoto waliokufa, walioumia, watoto walioachwa na vilema, waliokuwa yatima, watoto ambao wanacheza na mabaki ya vita, watoto wasiojua kucheka.
Acheni kupigana. Nakuombeni kwa moyo wangu wote. Tafadhali, acheni sasa hivi!" Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...