Yanga tayari ina wachezaji watatu wenye mikataba inayoendelea na kama
kanuni za VPL kwa wachezai wa kimataifa kuwa watatu zitatumika
wachezaji Haruna Niyonzima, Hamisi Kizza na Emmanuel Okwi ndio
watakaoendelea, hivyo uongozi uliomba mwongozo kwa TFF juu ya taratibu
zitakazotumika kwa msimu ujao kabla ya kuwasainisha Kavumbagu na Twite.
Awali uongozi wa Yanga ulikuwa kwenye mazungumzo na wachezaji hao
tangu mwanzoni mwa msimu wa 2013/2014 juu ya kuongezewa muda wa mikataba
yao ili waweze kuendelea kuitumika Yanga kwa ajili msimu mpya ujao
2014/2015.
Didier Kavumbagu na Mbuyu Twite ambao mikataba yao ilikuwa mwishoni
waliongea na uongozi tangu mapema mwaka jana mwezi wa Septemba juu ya
kuweka sahihi zao na kuendelea kuitumikia Yanga na kukubaliana mambo
yote ya msingi kikubwa kilichokuwa kinasubiriwa ni maamuzi ya TFF juu ya
usajili wa wachezaji wa kigeni msimu mpya wa 2014/2015 kwani Azimio la
Bagamoyo linapaswa kuanza kutekelezwa msimu huu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz