Rais Obama yuko mjini Brussels
ambapo atakutana na viongozi wa muungano wa Ulaya na shirika la kujihami
la NATO, kuzungumzia mzozo wa Ukraine.
Akizungumza mjini the Hague kabla ya kuelekea Brussel Rais Obama ameitaja hatua ya Urusi kutwaa eneo la Crimea kutoka kwa Ukraine kama ishara ya udhaifu.
Hatahivyo amesema bado kuna nafasi ya Urusi kusuluhisha mzozo huo kwa njia ya amani la sivyo ikabiliwe na vikwazo zaidi vya kiuchumi. Amesema japo huenda vikwazo hivyo vikaathiri uchumi wa dunia,Urusi ndio itakayoathirika zaidi.
Mkutano huo pia unatarajiwa kuzingatia maswala ya kibiashara na pia wasiwasi kwamba Marekani imekuwa ikichunguza kisiri shuguli za washirika wake kutoka nchi za Ulaya.Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz