Ndege na meli kutoka nchi mbali
mbali zinaendelea kuitafuta mabaki ambayo huenda yanatokana na ndege ya
Malaysia iliyopotea takriban wiki mbili zilizopita ikiwa imebeba
takriban watu 240.
Matumaini ya kutatua kitendawili hicho
yaliongezeka baada ya Australia kutoa picha za Satelaiti za vitu viwili
vilivyoonekana baharini vuikidhaniwa kuwa vifusi vya ndege hiyo. Hata hivyo hadi kufikia sasa hakuna cha maana kilichopatikana.
Afisa mmoja mkuu wa New Zealand amesema operesheni hiyo ilitatizwa na kuchafuka kwa bahari na kutoona vizuri.
Meli ya mizigo ya Norway ilitumia taa kuyatafuta mabaki hayo pasina kufanikiwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz