Tuesday, January 28, 2014

MWANAMKE ANASWA NA NGOZI YA CHUI...!!!

Mwanamke anaswa na ngozi za chui
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Mwajuma Hamisi, mkazi wa Yombo Vituka kwa kosa la kukutwa na ngozi mbili za chui kinyume cha sheria, zenye thamani ya sh milioni 11.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi wa kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema mwanamke huyo alinaswa Januari 18, mwaka huu katika eneo la Yombo Vituka, Wilaya ya Temeke.
Kova alisema mwanamke huyo alinaswa baada ya Ofisa Mhifadhi Wanyamapori mkazi wa Ukonga, kutoa taarifa kituoni hapo kwamba kuna mwananchi anauza ngozi za chui.
Alisema askari walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa na walipompekua chumbani kwake, walimkuta na nyara hizo za serikali.

Wakati huo huo, jeshi hilo limesema limemuua jambazi sugu la uhalifu wa kutumia silaha katika majibizano ya risasi na polisi.
Alisema awali polisi waliweka mtego ili kuyanasa majambazi hayo Januari 22 baada ya kufanya tukio la uporaji wa sh milioni 29 kwa mfanyabiashara wa Mtaa wa Kariakoo, anayejulikana kwa jina la  Shanys Abdalla, mkazi wa Mbezi.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 28.01.2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Tuesday, January 21, 2014

OBAMA AISIFIA BANGI NA KUIPONDA POMBE...!!

Obama 1 
Rais Barack Obama wa Marekani amesema kuvuta bangi ni salama zaidi kuliko kunywa pombe lakini akawasisitizia mabinti zake kwamba hilo sio wazo zuri pia ambapo kwa mujibu wa gazeti la The Mirror,  amesema anaamini uvutaji bangi hauna madhara au athari za hatari kwa mtumiaji binafsi.
Obama ambae aliwahi kuvuta kwenye enzi za ujana wake anasema “uvutaji sio kitu ambacho nachochea kifanyike, tambua ni upotezaji muda na inaathiri afya, bangi imehalalishwa kwenye miji ya Colorado na Washington kwa kura ya maoni na ilikuwa ni muhimu kwa ajili ya mataifa kumaliza uhalifu wa vijana wadogo wanaotoka kwenye familia zenye asili ya umasikini”
“tabaka la watoto wa kati hawafungwi kwa uvutaji bangi bali wanaofungwa ni wale watoto wa maskini, watoto wenye asili ya African -American na wa Kilatino wengi wao hawana uwezo wa kuwa rasilimali au misaada kuweza kuepuka vifungo vikali, hatupaswi kufunga watoto wetu au watumiaji binafsi vifungo virefu vya jela wakati baadhi ya hawa watunga sheria nao wamefanya uhalifu huo huo”
Bangi imebaki kuwa chini ya usimamizi wa sheria licha ya kwamba imehalalishwa kwenye miji ya Colorado na Washington huku serikali ikiwa haina nia ya kubadili msimamo wake.
Dawa hii ya kulevya iliingia sokoni Colorado na kusababisha foleni ndefu kwenye vituo mbalimbali vya uuzaji kuanzia Januari 1 huku na mji wa Washington ukitarajiwa kufuata.
Sentensi nyingine kutoka kwa Obama >>>  “ni muhimu kusonga mbele kwa sababu ni muhimu kwa jamii kutokuwa na hali ambayo sehemu kubwa ya watu kwa wakati mmoja au mwingine wamevunja sheria na ni wachache wanaoadhibiwa, wale ambao wanasema kuhalalisha bangi ni tiba na inatatua matatizo kijamii pengine (overstating) wanainua/wanakuza kesi.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 21, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.


.

Monday, January 20, 2014

AJALI YATOKEA MBALIZI MBEYA, MAGARI ZAIDI YA MATANO YAGONGWA

 Magari yakiwa yamegongwa Mbalizi Mbeya

MWANAJESHI FEKI AKAMATWA TANGA AKIMTAPELI DC

'Koplo' feki wa JWTZ akiwa ofisini kwa mkuu wa wilya.


 'Koplo' feki akijiandaa kupanda  kwenye gari kupelekwa kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi

SOMA SABABU YA MAWAZIRI MIZIGO KUACHWA KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI...!!!


RAIS JAKAYA KIKWETE.

SERIKALI imetoa kauli kuhusu tuhuma zilizokuwa zikiwakabili baadhi ya mawaziri, waliobatizwa jina la ‘Mawaziri Mizigo’, na hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa kukabiliana na kero zilizosababisha wapewe jina hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Ikulu Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Safue, alisema mawaziri hao walituhumiwa kutokana na changamoto zilizopo katika wizara zao; na si upungufu wao binafsi kama viongozi.

Mawaziri hao saba walitajwa katika ziara ya mikoani ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na baadae walihojiwa katika kikao cha Kamati Kuu cha chama hicho.

Baada ya kuhojiwa, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema Kamati Kuu ilimuachia Rais Kikwete jukumu la kuamua kuwafukuza kazi, kuwahamisha au kuwataka kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Miongoni mwa mawaziri waliohojiwa ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, ambaye sasa ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha.

HII NDIO THAMANI YA JINO MOJA LA NDOVU NA JINSI BIASHARA INAVYOFANYWA

  2013-04-28-TimphotobyCarlSafina.JPG
Yafuatayo ni kuhusu biashara ya meno ya tembo

Kwanza: Matumizi yake; meno ya tembo hutumika kutengeneza vitu vya urembo kama vile hereni , mikufu, mapambo kama vile sanamu na hata keys za keyboards za vinanda.
Vifaa vilivyotengenezwa kwa meno ya tembo hutumika nchini China kama sehemu ya kuonyesha ufahari, kwa mujibu wa Wikipedia.


Pili: Bei ya meno ya tembo

Bei inategemea na soko , hata hivyo kwa mujibu wa answers.com , jino moja la tembo huweza kuuzwa kwa dola za kimarekani mia saba (700).

Tuesday, January 14, 2014

MHUDUMU WA MOCHWARI 'AMCHIMBA MKWARA' WAZIRI...!!!


Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid. PICHA|MAKTABA 
*******
Mfanyakazi wa Kitengo cha Kuhifadhi Maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Eugene Vurugu amemtisha Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid kuwa ikitokea amefariki dunia akiwa mkoani Mbeya, basi maiti yake italazwa kwenye sakafu hospitalini hapo.
Akizungumza kwenye mkutano wa wafanyakazi na naibu waziri huyo mwishoni mwa wiki iliyopita, Vurugu alisema kitengo hicho kimezidiwa na wingi wa maiti zinazopelekwa hospitalini hapo.
Alisema kitengo hicho cha kina majokofu sita tu na hulazimika kuhifadhi miili kwa zamu ili angalau maiti zisiharibike.
“Hata wewe Waziri ukifa leo, hakuna pa kukuweka.
Utawekwa sakafuni kusubiri maiti nyingine zipoe halafu utaingizwa ndani kwa kuingizwa maiti mbili kwenye eneo la mtu mmoja,’’ alisema Vurugu.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

JAMBO TZ BLOG INAWATAKIA WAISLAM WOTE DUNIANI KHERI YA SIKUKUU YA MAULID

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 14, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC03476

DSC03460
DSC03463
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

CHRISTIANO RONALDO ATWAA TUZO YA FIFA BALLON D'OR 2013

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ameuvunja utawala wa miaka minne wa Lionel Messi wa Argentina anayechezea klabu pinzani ya Barcelona baada ya kunyakua tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa Fifa usiku wa kuamkia leo.
Ronaldo amemshinda pia Franck Rivery, Mfaransa anayechezea Bayern Munich.
Sherehe za tuzo hizo zilifanyika Zurich, Uswisi.
Nadine Angerer
Kwa upande wa wanawake, kipa wa timu ya taifa ya Ujerumani, Nadine Angerer ameibuka kinara mbele ya Marta (Brazil) na Abby Wambach (Marekani). Mdada huyo aliisaidia Ujerumani kutwaa taji ya Euro 2013 kwa wanawake akiokoa penati katika mechi yao ya fainali dhidi ya Norway waliyoshinda 1-0.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Monday, January 13, 2014

HODI TENA...!!! OPERESHENI TOKOMEZA YA PILI KUANZA KARIBUNI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
WAKATI hatua zaidi zikisubiriwa kuchukuliwa kwa watendaji waliohusika na ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa Operesheni Tokomeza, Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kutangaza kuanza kwa awamu ya pili ya Operesheni hiyo wakati wowote kuanzia sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alisema wakati wowote Rais Kikwete atatangaza kuanza kwa Awamu ya Pili ya Operesheni Tokomeza na itazingatia haki zote ikiwemo haki za binadamu.
Nyalandu alisema ingawa awamu ya kwanza kulikuwa na kasoro zilizojitokeza, awamu hii ya pili kasoro hizo zitafanyiwa kazi ili kuhakikisha rasilimali za Taifa zinalindwa.
Kusitishwa kwa operesheni hiyo kulikosababisha uteuzi wa mawaziri watatu kutenguliwa na waziri mmoja, kujiuzulu kwa mujibu wa Nyalandu, kulisababisha pia tembo 60 kuuliwa.
Mawaziri ambao uteuzi wao ulitenguliwa na Rais Kikwete mwishoni mwa mwaka jana ni Dk Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na Dk David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo) huku Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), akijiuzulu.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

TAARIFA YA CHADEMA KWA UMMA KUHUSU TUHUMA DHIDI YA M/KITI, FREEMAN MBOWE

TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU TUHUMA DHIDI YA MWENYEKITI WA TAIFA, FREEMAN MBOWE
Kama mojawapo ya mikakati ya baadhi ya watu wanaotaka kuhamisha mjadala wa makosa yanayowaandama ya utovu wa maadili na usaliti dhidi ya chama, hivi karibuni, Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe amezushiwa tuhuma zisizokuwa na ukweli wowote zikilenga kumchafua kwa nafasi yake ya uongozi na kuipaka matope taasisi anayoiongoza;

Tuhuma hizo ni pamoja na;

1.     Kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa mwaka 2005 eti alichukua fedha kutoka kwa Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono kiasi cha sh.Milioni 40 ili Mwenyekiti Mbowe asifanye kampeni katika jimbo hilo.

2.     Mwaka 2008, eti Mbunge Mkono alimpatia Mwenyekiti wa Chama Taifa, sh. Milioni 20 kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa
Tarime, kisha akazitoa kwenye chama kama mkopo na akalipwa.

3.    Mwaka 2010, wakati wa uchaguzi mkuu Mbunge Mkono eti alimpatia Mwenyekiti wa Chama Taifa sh. Milioni 200 kwa ajili ya kampeni za mgombea urais.

4.     Mwaka huo huo wakati wa uchaguzi mkuu, eti Mwenyekiti wa Chama Taifa, alipokea sh. Milioni 100 kutoka kwa Rostam Aziz kwa ajili ya kampeni.

Idara ya Habari ya CHADEMA, inapenda kusema yafuatayo;

1.    Hakuna ukweli hata mmoja katika tuhuma hizo. Ni uongo na uzushi uliopangiliwa kama moja ya mikakati ya watu wenye malengo ya kutaka kuilaghai jamii kwamba viongozi wa CHADEMA hawana tofauti na wale wa CCM na kwamba chama hiki kikuu cha upinzani kinachobeba matumaini ya Watanzania katika kupigania haki zao na kupinga kila aina ya ufisadi, kionekane hakina tofauti na chama kilichoko madarakani, ambacho kimepoteza ushawishi kwa wananchi.

2.     Matokeo ya uongo huo ni kutaka kuisaidia CCM na kugeuza mjadala.

3.    Idara ya Habari ya CHADEMA inapenda kuuambia umma wa Watanzania wote, hususan wanachama, wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na wapenda mabadiliko nchini kwamba,Mwenyekiti wa Chama Taifa, ameshawasiliana na mawakili walifanyie kazi suala hili kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria.

4.     Kwa uhakika tunapenda kuiambia jamii ya Watanzania wote, hususan wanachama, wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na wapenda mabadiliko wote nchini, kwamba; Chama wala Mwenyekiti wa Chama Taifa, mahali popote na wakati wowote, hajawahi kupokea msaada wa fedha hizo kutoka kwa waliotajwa kwa malengo yaliyosemwa.

5.     Tungependa kuwaambia waliozusha tuhuma hizo, ni vyema kama wanapenda kutunza heshima kidogo waliyobakiza katika jamii kutokana na kuelemewa na mzigo wa tuhuma za utovu wa maadili na usaliti dhidi ya CHADEMA, badala ya kugeuka kuwa mabingwa wa kupika uongo, wajibu masuala ya msingi yanayowaandamana kuhusu mikakati yao ya kuhujumu CHADEMA na viongozi wake, ambayo iwapo chama kisingeibaini na kuchukua hatua za kinidhamu, ingesababisha kuua ndoto na matumaini ya Watanzania kufanya mabadiliko ya kimfumo na kiutawala, kwa kuiondoa CCM madarakani.

6.     Taarifa kuhusu baadhi ya tuhuma katika mkakati huo ambazo zimemlenga Mwenyekiti wa Chama Taifa, kwa kuhusisha shughuli zake binafsi za uwekezaji, zitajibiwa kupitia taasisi husika.

Imetolewa leo Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...