Paul Makonda, Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Taifa, UVCCM
*******
KWA kipindi kirefu sasa vijana
ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) tumeshuhudia na kusikia kauli na
vitendo vya baadhi ya wanachama wa CCM vinavyoashilia ukiukwaji wa
makusudi wa maadili, miiko na kanuni za Chama. CCM katika uhai wake wa
miaka 37 baada ya kuunganisha TANU na ASP, imeendelea kukua na kushamiri
kutokana na misingi imara ya kikatiba tuliyojiwekea tangu mwaka 1977,
ambayo wana CCM wote kwa utashi na hiari tumeienzi na kuifuata.
Asiyetaka, ni ruksa kuondoka na kutuachia chama chetu.
Ni kwa njia hii tumeweza kuimarisha mshikamano ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kutuwezesha kushinda katika chaguzi mbali mbali, hivyo kuendelea kutoa uongozi katika ngazi zote za utawala nchini. Hivyo basi, kitendo chochote kile chenye mwelekeo wa kubomoa mshikamano ndani ya Chama, ni kitendo cha kutudhoofisha, hivyo kutuengua katika uongozi wa nchi. HILI KWA VIJANA WA CCM, HALIKUBALIKI!

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz