Saturday, September 28, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 28, 2013

DSC 0066 048af
DSC 0067 182bf

"SINA MIKOSI KAMA WATU WANAVYOENEZA MANENO MITAANI" AUNTY EZEKIEL

Stori: Mayasa Mariwata
STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amesema hana mkosi kama watu wasiomtakia mema wanavyoeneza maneno mitaani.
Akipiga stori na paparazi wa Ijumaa juzikati, Aunt alisema kuna baadhi ya watu wasioitakia mema ndoa yake wamekuwa wakieneza maneno kwamba ana mkosi ndiyo maana kila mwanaume anayekuwa naye hupatwa na balaa.
Staa huyo aliongeza kuwa haumizwi kichwa na maneno hayo kwa kuwa anaamini kila kinachotokea katika maisha yake ni mipango ya Mungu.
“Maneno yao ni imani potofu na siwezi kumfikiria mwanaume niliyewahi kuwa naye huko nyuma kabla ya kuolewa na mume wangu Demonte kwani hakuna baya lililomfika tangu tulipooana,” alisema Aunt.
-GPL

MMILIKI ARSENAL ASEMA WENGER ANABAKI ARSENAL

wenger 24bf5
CHIFU wa Arsenal, Stan Kroenke anataka kocha Arsene Wenger abaki katika klabu hiyo kwa muda mrefu na kuleta taji la Ligi Kuu ya Enland Emirates.
Mfaransa huyo amekuwa katika klabu hiyo kwa miaka 17 na The Gunners ikiwa inakabiliwa na ukame wa mataji kwa msimu wa tisa sasa, amekuwa akipigwa zengwe aondoke, hususan kutokana na Mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu.
Lakini mtu mwenye hisa nyingi za klabu, Kroenke hana shaka anataka Wenger abaki.
Mmarekani huyo amesema kwamba hafikiri kama kuna mwingine bora kuliko yeye na anaamini Wenger anafanya kazi nzuri.
Alipoulizwa kama mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 63 yumo kwenye mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo, Kroenke alisema: "Hiyo ni sahihi kabisa. Arsene anafahamu ambavyo tunahisi, falsafa zetu ni nini, nini tunataka kufanya na ninahisi tuko pamoja sana,".
Kufuatia klabu kuvuna rekodi yake ya usajili kwa kumsaini Mesut Ozil kutoka Real Madrid.
Kroenke alisema: "Kwa kweli namfurahia Arsene - safi sana, mweledi. Ana upeo mkubwa wa uongoza timu na klabu. Yuko sahihi katika hilio.
Kroenke pia amesema Wenger hastahili lawama kwa klabu hiyo la Kaskazin mwa London kumkosa mshambuliaji Luis Suarez, kwani ni Liverpool ndio hawakuwa tayari kumuuza nyota huyo kutoka Uruguay. Chanzo: binzubeiry

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA

wakuu_wa_usalama_ce362.jpg
Maafisa wakuu wa ujasusi wametakiwa kufika mbele ya kamati ya ulinzi ya bunge ili kuhojiwa kuhusu mashambulizi ya kigaidi dhidi ya jumba la Westgate mjini Nairobi.
Taarifa kwenye vyombo vya habari nchini humo zinaonyesha kuwa hali ya kulaumiana imeanza kuibuka huku mashirika ya usalama yakinyosheana kidole.
Watu 67 waliuawa kwenye shambulizi hilo huku zaidi ya miamoja sabini na tano wakipata majeraha mabaya. Shirika la Red Cross nalo linasema kuwa watu 61 wangali hawajulikani waliko.
Wataalamu wa uchunguzi wa mauaji wangali wanafanya uchunguzi wao wakitafuta miili na dalili za kilichosababisha shambulizi hilo.
Kamati ya bunge inataka maafisa wanaohusika na maswala ya usalama waweze kuwajibishwa.
Kundi la kigaidi la nchini Somalia, al-Shabab limedai kufanya mashambulizi hayo yaliyodumu siku nne kama hatua ya kulipiza kisasi kwa Kenya kujihusisha nchini Somalia kijeshi.
Hii leo ni siku ya tatu ya maombolezi kwa wathiriwa wa shambulizi hilo wakiwemo raia na wanajeshi.
Rais Uhuru Kenyatta amehudhuria mazishi ya mpwa wake na mchumba wake mjini Nairobi ambapo aliwahutubia waumini.
Walipuuza onyo?
Hatua ya kuwataka maafisa hao wa usalama kufika mbele ya tume ya bunge siku ya Jumatatu, inakuja kutokana na wasiwasi miongoni mwa wakenya kuhusu kiwango cha maafisa hao kujiandaa kwa tukio lolote la kigaidi sawa na lililotokea Westgate.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari mmoja wa maafisa waliotakiwa kufika mbele ya kamati hiyo ni mkuu wa shirika la ujasusi Michael Gichangi, anayesema alitoa taarifa za ujasusi kuhusu shambulizi hilo kwa polisi.
Lakini, afisaa mmoja mkuu katika idara ya polisi alikana kuwa taarifa hiyo ilitolewa kwa polisi.

BAADAYA KUTOSWA NA DIAMOND, MDOGO WAKE AIMBA NYIMBO YA KUMPONDA

HUU wimbo hatari tupu. Inaelezea maisha ya Diamond kabla hajatoka kimuziki. Dogo aloimba anadai Diamond ni ndugu yake wa damu na hakumbuki alipotoka. Duuh kaongea mambo mengi sana. Sina mbavu kwa kweli. Isikilize hapa Chini. Ni balaa tupu. Ni bonge moja la Ngoma.

ANGALIA VIDEO YA NDOA YA WATOTO WADOGO HUKO MJINI DODOMA



Vitendo vya ukatili wa kijinsia bado vipo katika jamii yetu, huko mkoani Dodoma ilishuhudiwa ndoa ya watoto wadogo kabisa, kiukweli ni ya kushangaza na hata huwezi kuamini, ila ndio mambo ya walimwengu hawa.


  ANGALIA VIDEO HAPO CHINI...

Friday, September 27, 2013

MJUE GAIDI SAMANTHA ALYEONGOZA AL-SHABAAB KUUA KENYA


Samantha20Lewthwaite-9559681 1f85a 
Adaiwa kuuawa Westgate
*Alifika Tanzania kwa Pasipoti ya Afrika Kusini
Ssamantha Lewthwaite, mwanamke wa Uingereza anayetajwa kuwa kiongozi wa ugaidi uliofanyika Nairobi, Kenya

WAKATI umwagaji wa damu katika kituo cha biashara cha Westgate ukiingia siku ya nne jana, Mwanamke ambaye ni raia wa Uingereza, Samantha Lewthwaite (29), anayetajwa kuwa ndiye aliyeongoza kundi la Al-Shabab kufanya shambulizi hilo, anahofiwa kuuawa.

Gazeti la Daily Mail la Uingereza, lilikariri vyanzo vyake vilivyoko ndani ya Jeshi na mfumo wa usalama nchini Kenya, ambavyo vimethibitisha kuwa mwanamke huyo ni miongoni mwa magaidi waliouawa na Serikali ya Kenya.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohamed, katika mahojiano yake na kituo cha habari cha PBS, hakusema kama mwanamke huyo ameuawa lakini alithibitisha kuwa miongoni mwa magaidi waliovamia Westgate ni mwanamke wa Uingereza ambaye hata hivyo hakumtaja jina.
Hatua hiyo iliibua tetesi kwenye vyombo vya habari vya Kenya ambavyo vilimtaja mwanamke huyo kuwa ni Samantha.
Hata hivyo kauli hiyo ya Waziri huyo inaonekana kupingana na ile iliyotolewa awali na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Kenya, ambaye alisema kuwa magaidi wote waliovamia kituo hicho walikuwa wanaume na kwamba huenda baadhi yao walivalia mavazi ya kike.

TAARIFA YA JKT KWA VIJANA WANAOTAKA KUAHIRISHA MAFUNZO

JKT1_4a456.jpg
Vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT awamu ya tatu na pia wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu, wambao wanataka kuahirisha mkataba wa JKT, wanatakiwa kuandika barua Makao Makuu ya JKT kuomba kuahirisha mkataba wa JKT.
1. Barua binafsi kuomba kuahirisha mkataba iwe na picha yake.
2. Nakala ya barua ya kucahguilwa kujiunga na chuo (Joining instructions)
3. Barua hiyo ieleze kuwa utajiunga na JKT baada ya kuhitimu masomo.
4. Barua zao zifike Makao Makuu ya JKT kabla ya tarehe 02 Kotoba, 2013.
ANGALIZO
Kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria ni lazima. Hivyo ni wajibu wa kila mhitimu kuhudhuria mafunzo hayo.
Agizo hili limetolewa na Jeshi la Kujenga Tafia, Makao Makuu.
---
Imetolewa kwenye tovuti: http://jkt.go.tz/mkataba-jkt.html

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2g4C18z5v

KENYA YAMSAKA SAMANTHA LEWTHWAITE

nairobi c0494
Polisi wa kimataifa Interpol, wamemuweka mwanamke aliyeshukiwa kuongoza mashabulizi ya kigaidi nchini Kenya raia Muingereza Samantha Lewthwaite, kwenye orodha ya watu wanaosakwa sana duniani.
Hatua hii ni kutokana na ombi la serikali ya Kenya kwa Interpol.
Bi Lewthwaite, mwenye umri wa miaka 29, ni mjane wa mlipuaji aliyefanya shambulizi la kujitoa mhanga mjini London Uingereza mwezi Julai mwaka 2005
Anajulikana kama "white widow", na amehusishwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab nchini Somalia.
Polisi wa Interpol hata hivyo hawakuhusisha hatua ya kumsaka Samantha na shambulizi la kigaidi dhidi ya jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi lililowaua watu 67.
Hata hivyo, hatua hii ya kumsaka Bi Lewthwaite inakuja punde baada ya shambulizi hili la kigaidi nchini Kenya.
Al-Shabab ilikiri kufanya mashambulizi hayo yaliyotokana na kutekwa kwa jengo la Westgate na kisha kutekwa kwa raia wa kawaida waliokuwa ndani ya jengo hilo kwa siku nne.
Kwa mujibu wa polisi wa Interpol, mwanamke huyo anasakwa na serikali ya Kenya kwa kumiliki mabomu na kupanga njama ya kufanya mashambulizi kuanzia Disemba mwaka 2011.
Ikiwa mwanamke huyo atakamatwa katika nchi mwanachama wa Interpol, atazuiliwa na kusibiri kupelekwa katika nchi anayotakikana kwa kesi kufunguliwa dhidi yake.
Bi Lewthwaite anajulikana kwa jina bandia la, "Natalie Webb" –na alikuwa anasakwa kwa madai ya kumiliki hati bandia ya usafiri nchini Afrika Kusini.
Ni mjane wa Germaine Lindsay, mmoja wa washambuliaji wanne waliohusika na shambulizi la kigaidi mjini London ambapo watu 52 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa. 
Chanzo: bbcswahili

MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 27, 2013

DSC 0064 dad11
DSC 0065 8682d

Thursday, September 26, 2013

BAADA YA KENYA SASA AL-SHABAAB YAIGEUKIA TANZANIA....WATISHIA KUIVAMIA MUDA WOWOTE


*Yajigamba kufanya mashambulio muda wowote
*Watanzania wapewa mafunzo ya ugaidi nje ya nchi
*Polisi nchini wasema vyombo vya ulinzi viko macho
*Mtanzania akamatwa Kenya akihofiwa gaidi
 
WAKATI wananchi wa Afrika Mashariki wakijawa na hofu ya mashambulio yanayopangwa kufanywa na vikundi vya ugaidi vya Al Qaeda na Al Shabab, imebainika kuna Watanzania waliopewa mafunzo ya ugaidi wanaojiandaa kufanya maovu.

Hayo yamebainika siku chache baada ya wanamgambo wa kundi la Al Shabab kufanya mashambulio katika Jengo la Biashara la Westgate mjini Nairobi na kuua watu zaidi ya 70 na kuacha mamia wengine wakiwa wamejeruhiwa.

Mkuu wa Interpol Tawi la Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Gustav Babile aliyasema hayo jana katika mahojiano maalumu na MTANZANIA.

YAFAHAMU MAJINA YA ASILI YA BAADHI YA MASTAR WA BONGO MOVIES

 KWA kawaida binadamu yeyote huzaliwa na kubatizwa jina ambalo hulitumia katika masomo na hata kazi yake.

Tofauti na ilivyo katika fani nyingine, wasanii wamekuwa wakijibatiza majina ya ziada (a.k.a). Mbaya zaidi, majina hayo huwa yanaanza kama utani lakini inafika wakati msanii husika

analizoea jina hilo jipya na kulifanya kuwa kama rasmi. Leo Amani linakuletea orodha ya baadhi ya mastaa ambao majina waliyopewa na wazazi wao ‘yamekufa’, hawayatumii kabisa: LULU

Jina lake halisi ni Elizabeth Michael, Lulu lilizoeleka kupitia tasnia ya uigizaji. Alianza kulitumia wakati alipojiunga na Kundi la Sanaa la Kaole.

Hadi leo hii, siyo rahisi kabisa mtu kutokea na kumuita jina la Elizabeth, wengi wanamfahamu kwa jina la Lulu.
RAY
Ray ndiyo jina ambalo limezoeleka na wengi. Vincent Kigosi alilopewa na wazazi wake ni kama limekufa. Kwa zaidi ya miaka kumi sasa tangu alipokuwa kwenye Kundi la Sanaa la Kaole hadi sasa.
Jina la Ray ndiyo watu wanalolifahamu zaidi ingawa hivi karibuni baadhi ya wasanii wenzake wamekuwa wakijaribu kumuita Vincent ili kurudisha uhai wa jina hilo.

JOHARI
Jina lake halisi ni Blandina Chagula. Johari lilizaliwa kwenye Tamthiliya iliyobeba taito ya jina hilo. Akiwa katika Kundi la Kaole, alianza kujiita Blandy, baadaye alibadilisha jina hilo na kuwa Johari walipoingiza tamthiliya hiyo ambayo pia ilizaa filamu.

MWANAFUNZI AMCHINJA MWALIMU WAKE DARASANI...!!!

KUSHOTO: Mwalimu Sun Wakang. KULIA: Damu ikiwa imetapakaa darasani muda mfupi baada ya tukio hilo.
Mwanafunzi wa China amemchinja mwalimu wake katika kulipiza kisasi baada ya simu yake ya mkononi kutaifishwa.
Mwanafunzi huyo, aliyetajwa kwa jila la Lei katika taarifa za habari za mjini humo, alibambwa na mwalimu wake, Sun Wakang akiwa anachezea simu wakati wa somo la Kemia katika shule moja mjini Fuzhou, mashariki mwa jimbo la Jiangxi nchini China.
Siku iliyofuata Lei alikwenda kwenye darasa analofundisha Sun ambako mwalimu huyo alikuwa ameketi akisahihisha mitihani, na kumchinja kutokea kwa nyuma.
Mwalimu huyo mwenye miaka 32 ambaye ni baba wa watoto watatu alifariki papo hapo huku mwanafunzi huyo akitokomea kusikojulikana.
Jana Lei alipiga namba ya simu ya dharura na kukiri kuhusika na uhalifu huo kabla ya kujisalimisha mwenyewe polisi mjini Shanghai.
Sun alifanya kazi kama mwalimu wa Kemia katika Shule ya Kati ya Linchuan No. 2 kwa miaka mitano kabla ya mauaji yake ya kutisha, ofisa wa shule Xiong Hainshuo alieleza.

NI AL-QAEDA, SI AL SHABAAB

westgate 870d9
  • Magaidi wa Marekani, Uingereza, Syria wahusika
SHAMBULIO la kigaidi lililofanywa nchini Kenya Jumamosi iliyopita na watu waliodhaniwa kuwa wafuasi wa Al- Shabab, sasa limeelezwa kutekelezwa na mtandao mpana zaidi wa kigaidi wa kundi la Al-Qaeda.


Baadhi ya wachambuzi na wachunguzi wa masuala ya kiusalama na kimataifa, wameyataja mambo matatu ambayo yanathibitisha pasipo shaka kwamba waliotekeleza tukio hilo la kuvamia, kuteka nyara na kuua watu wapatao 68 katika Kituo cha Biashara cha Westgate, ni wa aina ya kundi ambalo kinadharia na kimatendo linafanana na lile la kigaidi duniani la Al-Qaeda. Mambo yanayotajwa na wachambuzi na wachunguzi hao ni pamoja na mbinu, teknolojia na aina ya watu waliotumika kutekeleza shambulio hilo.
Katika uchambuzi wao, wameeleza kuwa mbinu iliyotumiwa na magaidi hayo kuvamia pasipo kujulikana mara moja na vyombo vya ulinzi na usalama vya nchini Kenya, lakini pia aina ya silaha walizokuwa nazo, inaonyesha kuwa kundi hilo limeamua kutumia kivuli cha Al-Shabab kufikisha ujumbe kwa dunia kwamba lipo licha ya uongozi wake kubadilika.
Kwamba mbali na mbinu pamoja na teknolojia, pia aina ya watu waliohusika kutekeleza shambulio hilo ambao wamebainika kutoka katika mataifa mbalimbali duniani, ndio ambao wamewafanya wachambuzi na wachunguzi hao waanze kupata shaka kwamba huenda kuna kundi kubwa zaidi lililotekeleza shambulio hilo, ambalo limejivika taswira ya Al-Shabab.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI SEPTEMBA 26, 2013

DSC 0054 223dc
DSC 0055 3bc8f

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...